Lazaro Nyalandu: Tatizo kubwa la CHADEMA ni Uongozi wa juu, CCM imejaliwa mfumo

Alimgalagaza Lissu watu wakasema huyu anaweza kuwa kama Lowasa tusimpe... Je Walioyasema Hayo Na Yeye Aliyemgalagaza Lissu Nani Alikua Sahihi Au Nani Tumuamini!!?
 
Mfumo wa fomu moja bila copy, ukitaka kugombea unafukuzwa huo ndiyo mfumo?
Nyalandu hana hata chembe ya akili. Hivi mfumo wa fomu moja tu nao ni mfumo?

Haya atwambie leo wagombea wa uenyekiti wa CCM Taifa juzi walikuwa wangapi? Kwa nini?
 
Nyalandu hana hata chembe ya akili. Hivi mfumo wa fomu moja tu nao ni mfumo?

Haya atwambie leo wagombea wa uenyekiti wa CCM Taifa juzi walikuwa wangapi? Kwa nini?
Chadema wagombea walikuwa wangapi wa nafasi ya urais shidi ya dictator mmoja ccm
 
Aelewe pia kwamba CCM viongozi wa juu wako safi lakini kule mikoani na wilayani, kuna watu wanakuponda kwa mawe kwa sababu tu wako CCM.
 
Majambazi yaliyofilisi mali za Watanzania yanaanza kurudi mmoja baada ya mwingine baada ya jiwe kufariki. Serikali ya Msoga mpeni cheo mwenzenu huyo karudi nyumbani kuendeleza uovu mlioufanya wa wizi wa mali za Watanzania
 
"..Nyalandu alipata 100 wajumbe walikuwa 30 nilipata kura zote Tundu Lissu alipata kura 24 nilimgalagaza kweli kweli" . Ebu nieleweshe hii hesabu.
Mpuuzi tu huyo. Kwanza Kamati kuu hachagui wagombea, inapendekeza majina... Na wote tunajua CDM walikua na majina 3....Bora angesema kuwa alidhulumiwa kura kwenye baraza kuu.

Hivi hao waandishi wa Habari hawajui kuuliza maswali au ndiyo upeo wao ulipoishia...!?
 
Nchi hii Dictator number 1 ni Freeman Aikaeli Mbowe huyu siku Mungu akimuita utazuka ugomvi mkubwa sana wa kugombea madaraka Chadema kati ya familia na ukoo wa Mbowe na wanaharakati uchwala kina Lissu na wenzake.
Na huko kwingine kuna nafasi haziombwi! Siku zikiombwa, tafakari kitakachotokea
 
Nchi hii Dictator number 1 ni Freeman Aikaeli Mbowe huyu siku Mungu akimuita utazuka ugomvi mkubwa sana wa kugombea madaraka Chadema kati ya familia na ukoo wa Mbowe na wanaharakati uchwala kina Lissu na wenzake.
Ni bora huyo dictator kuliko hao vinjaa njaa hebu pata picha Nyalandu leo hii angekuwa Mwenyeketi wa chama si tungekua tushauzwa mpaka wanachama wenyewe kama walivyouzwa TLP na NCCR

CCM inajaribu kubomoa CDM kwa sababu tayari wanaona ni chama ambacho kimeshakomaa mikiki yote na hila za kila aina choni ya MBOWE hivyo wanawasiwasi ukomavu huo soon utawang'oa madarakani
 
Kuna vitu unajiuliza sana kuhusu Watanzania

Nayalandu kama raia ana haki ya kushiriki siasa popote pale alipo bila kuulizwa lolote au chochote
Nyalandu alipohama CCM ilikuwa kwa matakwa yake binafsi

Kinachokera ni kwamba baada ya kurudi CCM sasa anakwenda kueleza katika vyombo vya habari mambo yasisyohusiana na haki yake kama Raia ya kushirikia siasa.

Nyalandu alikuwa na haki ya kueleza hayo akiwa katika chama halafu aondoke. Hili la kueleza baada ya kupokewa ambalo tunajua lina ahadi ni njia ya kujitangaza ili mkono uende kinywani.

Kukaa kimya kunamjengea mtu heshima, haya ya Nyalandu ni kujivua nguo hadharani
Ipo siku tutasikia pia akitueleza ya chumbani sidhani kama anaelewa haki, wajibu na stara.

This is too low Nyalandu, hata kaheshima ulikokuwa nako sidhani kama kapo tena.
Ukimuona alivyo nadhifu hutaamini ..

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Huyu kuna namna.. na Chadema wanamjua sana tu, asijione mwerevu. Ndio maana Mbowe alimkatalia msaada wake wa kumkodia Lissu ndege, wakati alipopigwa zile risasi.. Pengine wangemmaliza Lissu wa watu hawa. Wakina Mbowe wanamjua sana tu, asitake wamuongelee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…