Wakuu za mida tena,
Nimekuwa nikifutilia mijada mbali mbali kila kukucha kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mstakabali wa nchi yetu.ila kwa nataka leo nami niongelee busara za huyu jamaa anae jiita king of all social media LEMUTUZ nation.
Lemutuz nation maarufu kwa ku post picha za kujisifu na mabebez amekuwa akijiita mchambuzi wa siasa na kuuaminisha uma yeye ana fact na kupenda sana kusema yeye mawazo yake ndio uchunguzi na final say kwa kila jambo na sio opinions (mtazamo wake).
Lemutuz (William Malecella) mara kadhaa hujisifu na kubeza watu wengine alikuwa team membe mwanzon baadae akashindwa akakubali matokeo baada ya magufuri kushinda.
Leo natamani watu wajue busara zake humu ziko wapi?Na naona anazidiwa na mwigizaji wema sepetu kwa kile tunaita political tolerance maana yeye hapendi umpinge hoja yake aliyo weka instagram ukimpinga tu au ukitoa maoni yakuto mwambia unaakili kubwa ana kublock.
Mfano alitupia wiki iliyo pita kuhusu kushauli CHADEMA kuwa watanzania walitegemea ukombozi kutoka CHADEMA na watanzania waliamini sana CHADEMA kwa mabadiliko lakini wamemkaribisha lowassa wamewakosea watanzania.
Nikamjibu toka lini wewe Lemtuz ukawa mshauri wa CDM wakati tunajua wewe ni CCM damu kwanini unalialia wakati CCM hamtaki Lowassa hvyo tu et kaniblock.
Wadau je huyu hazidiwi uvumilivu na Wema Sepetu ambae kila sku anapigwa na kutukanwa na hamblock mtu?