Safi sana le Mutuz life circle yako ni yakipekee toka mdogo na unaexposure ya maana tu
- Thanks Boss, on a serious note watu hasa vijana wadogo wanatakiwa kusoma hii "TRUE STORY" of my life na kujitafakari wapi inawahusu nawajua watoto wengi wa Viongozi hapa Mjini wanaoranda randa no life, kisa walilewa na Majina ya Baba zao na sifa za watu wanafiki,
1. Sijawahi kujuta kukosa kuishi in power ya Baba yangu yaani UWaziri Mkuu na Makamu wa Rais, ingawa mara nyingi aliniomba nirudi nilimkatalia katakata, leo ninawaona Watoto wengi ambao alikulia kwenye power wanavyohangaika ninamshukuru sana Mungu, ingawa sio wote wapo ambao Baba zao walizitumia nafasi zao wapo sawa lakini sifurahishwi na maisha yao ya kujificha ficha kuogopa watu wasiwaseme kuhusu baba zao.
2. Enzi za utoto wangu ni Ubaharia na Soccer za Yanga na Simba ndizo zilizokua na impact za kutoboa kimaisha bila kusoma, lakini kwenye Ubaharia ilikua ni more fantasy than reality ambayo niliiona mwenyewe nikiwa baharini Mabaharia walikua wakirudi hawasemi hadithi yote kwa mfano mateso ya kuvuka "Bermuda Triangle" Mishahara midogo kumbuka kwenye ubaharia kulikua na Cheap Labor ya Wafilipino so malipo yalikua madogo sana ila kwa sababu walikua wanakaa muda mrefu bila kuchukua mshahara wakiwa safarini ndio maana walionekana wana pesa waliporudi ingawa pesa haikudumu sana kwa sababu tatizo halikua pesa ila akili ndogo za Mabaharia, nilitaka sana kuepuka kurudi namna hiyo and I did.
3. Nia na lengo langu kwenda ilikua kutafuta Elimu na Maisha bora zaidi nilipofika Majuu nikaishia kupata kitu muhimu sana ambacho sikukifikiria mwanzoni nacho ni "EXPOSURE" ndio maana leo ninawasumbua sana wabongo wenye akili finyu ni kwa sababu hiyo tu. Bongo kuna watu wana pesa lakini hawajui cha kuzifanyia, mimi sina pesa nyingi lakini ninajua what to with my little money. Wananishangaa kwa sababu wanaamini sina pesa sasa ninapofanya mambo yangu ya kipesa ambayo wao wanaamini wanatakiwa wayafanye wao ninawashangaza sana,
- Kuna siku mtu mmoja aliniambia kwamba "SIKU HIZI UNA PESA SANA" nikamuuliza kistaarabu sana ni lini aliwahi kuniona na pesa au nikiwa sina? hakuwa na jibu kwa sababu nilijifunza kwa Baba yangu kua pesa sio our thing,
4. Ninaomba kuchukua nafasi hii kusema bila kupindisha kwamba hii topic hapa imenishangaza sana kwa sababu ni kwa mara ya kwanza kua na mjadala unaonihusu humu JF ambao ni Fair toka nibadili ID yangu fake miaka mingi iliyopita na kua mimi mwenyewe. Nilipokua na Fake ID nilikua maarufu humu JF kuliko wote labda MWanakijiji tu ndiye tulikua level moja, lakini nilipobadili tu ID na kua mwenyewe siku zote imekua negative silalamiki cause ndiyo sababu leo ninakusanya Millions kutokana na Social Media kwa sababu nilianzia hapa JF. Nimefarijika sana kwamba kumbe sio Wabongo wote ni wajinga huu mjadala ukiusoma wote utaona Unbalance ya Negativity ambayo ni ndogo sana kulinganisha na Positive comments. Infact ni kwa mara ya kwanza nimeona watu wengi wakitetea my works in the Story,
- Ingawa pia ninaomba kuwashukuru sana Jamiiforums kwa kuamua kuibeba hii Story of my life, ninawashangaa sana wanaopinga kwa kushindwa kurekebisha wanachokipinga, ukisema hapa anasema uongo unatakiwa uuseme ukweli. Guys this is not about me it is about what I have faced in my life na jinsi nilivyopigana kufikia nilipo, binafsi sina wasi wasi na nilipo ni ninajua kua bila ya kwenda Majuu nisingekua hapa nilipo utajiri wangu mkubwa niliorudi nao ni AKILI KUBWAZZZ I am so proud of myself for that.
- Halafu Haters poleni sana maana bado ninataka kuandika Vitabu vingi, kuna "MY JF EXPERIENCE", "MY FACEBOOK EXPERIENCE", "MY INSTAGRAM EXPERIENCE" "MY BONGO'S EXPERIENCE" so mna kazi sana ya kupinga pinga bila Facts hahaha saty tuned!
le Mutuz Mobimba! Le Mutuz Nye! Nye! Nye!