- Hii picha nilipiga na wafanyakazi wa ICL Miezi 2 iliyopita siku nilipokwenda kusaini mkataba mpya na ICL ambao ndio handlers wa Cocacola, baada ya makubaliano wakaniomba nihudhurie party yao hii hapo juu. So nilianza mahusiano na Cocacola loong time ago hata kabla hawajafikiria kutengeneza makopo, na walipoamua kutengeneza makopo wiki nne zilizopita walinifahamisha na kwamba watanitengenezea kopo lenye jina langu as a sample na hatimaye watatengeneza ya kuuza tukakubaliana kwamba kopo la kwanza is no problem ila ya kuuza tutakaa chini kuhusu malipo yake separate, sasa nashangaa supposedly Mwanasheria wa Instagram, sijawahi kuona Mwanasheria akifanya mambo ya Sheria Instagram na kutukana watu asiowajua, kama alitaka kuwaonya wasanii wake angefanya hivyo lakini kutujumuisha wote that was wrong, sio yeye peke yake hapa mjini anayejua Sheria wapo Wanasheria wengi sana hapa mjini na besides kweli anaweza kunifundisha mimi my rights za kisheria? Are serious au unajichezea.
- Mwanasheria wa kwenda kutukana watu Instagram kwangu ni maajabu makubwa sana hili suala la Cocacola na makopo limeleta kizungu zungu sana mapaka ninajiuliza ni kweli ni tatizo la makopo au kuna zaidi ya makopo? Nimewaomba wale wote wanaohusika wawe wawazi kuhusu tatizo lao la kweli badala ya kujificha nyuma ya makopo!
- Tena tizama mkono wangu wa kushoto nimeushika mkataba wenyewe mkononi live!!
Le Mutuz