Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 70,785
- 186,690
Huyo ni Mshana jamani! Wapare tupo vyema upstairs when it comes to intellectual intelligence na washana ni walimu wazuri sana kwenye kumwaga nondo na unafundishwa mpaka unafurahia somo!Unajua tatizo letu tulishakuwa na mtizamo hasi sana kwamba siyo rahisi mtu akawa na tabia zile nzuri za kuwapendeza wengine katika kiwango cha juu. Hawa wanafunzi ni watu wazima na wana akili, na wanajua kuwa kwa kumpa zawadi mwalimu anayegawa marks, wanakuwa wanamchongea. Angekuwa anagawa marks wasingeweza kufanya hivyo, lazima wangekausha!
Mimi kwa muda huu bado niko convinced kwa kiasi kikubwa kabisa kwamba mwalimu huyu anaweza kuwa ana tabia nzuri na za kipekee sana na ndizo hizo zilizopelekea watoto hawa wakampa zawadi, na ninachokiona mini siyo kwamba anawapa alama nzuri bali huwa anawafundisha wanaelewa vizuri sana katika namna ambayo si walimu walio wengi wanaweza kuwaelewesha kwa kiwango hicho. Kwa hiyo kinachoweza kuwa kimepelekea mwalimu kupewa zawadi si alama nzuri kwa wanafunzi, bali ufundishaji wake pamoja na PR yake kwao.
Zaidi ni kuwa kawaida mwalimu unapendwa zaidi na wanafunzi hasa unapokuwa unafundisha darasa ambalo baadhi yao wana umri mkubwa kuliko wewe; hawa ndiyo huwa wanakuwa mahakimu wa kupelekea wengine wakufahamu vizuri namna utu wako halisi wa ndani ulivyo! Huwa siyo rahisi sana mdogo mmoja kuwaficha kitu wakubwa wengi
Tuko friendly sana ndio maana wanafunzi wamemkubali mchizi! I am Mshana too!