Jadda
JF-Expert Member
- May 20, 2019
- 30,567
- 86,748
Aiseee mbona na ngono za mitaani hamkemei kama mnavyokemea za vyuoni? Hao lecturers wanaowaharibu wanafunzi wa vyuo wana utofauti gani na wanaume wa mitaani wanaowaharibu mabinti wa mitaani?
Ni kipi kinachofanya muone kama wanawake wa mitaani ni sawa tu kuharibiwa ila wa mavyuoni na makazini ndiyo hawafai kuharibiwa! Au ndiyo kuwaonea wivu lecturers kwa kuwa huko mavyuoni na makazini ndiko kuna watoto wazuri!
Mimi nasemaga ukiona mwanaume anajifanya anatoa ushauri kwenye jambo lolote linalohusiana na jinsia ya kike ujue lina maslahi kwake mwanaume na si vinginevyo! Hakuna mwanaume anayeweza kutetea jambo lolote ambalo linamfaidisha mwanamke peke yake pasipo yeye mwanaume kufaidika kitu narudia hayupo sasa endeleeni kujidanganya!
Wengi wenu mnaosema eti kulea mabinti kazi ndiyo ninyi mnaoharibu mabinti za watu wengine huku mitaani ila kujifanya mnawasema lecturers eti wanawaharibu wanavyuo! Na ndiyo muone jinsi gani inauma kuharibia watu mabinti zao haijalishi ni wanavyuo au si wanavyuo!
Mngekuwa mnakemea uzinzi kwenye nyanja zote kuanzia mavyuoni, makazini, mitaani na majumbani kweli tungewaona wa maana! Ila hii ya kujifanya mnakemea kwenye baadhi ya nyanja tu inafanya muonekane wanafiki tu na hamna lolote zaidi ya kutetea maslahi yenu na kuvutia upande wenu!
Tena mbaya zaidi lawama zote mnawatupia wanawake kama kawaida yenu kana kwamba hao wanaume wanaowatongoza hao wanawake wako sawa tu na hawana makosa kabisa! Wengine wanatetea eti ni ngumu wanaume kuepuka vishawishi vya hao wanawake wa vyuoni!
Vishawishi kila jinsia inakutana navyo na inashawishika kwahiyo kusema eti wanawake ndiyo waache kushawishi bila kuwaasa wanaume nao waache inakuwa ni kazi bure sababu wanaume watajiona wanachofanya ni haki yao kwahiyo hata wanawake wakiacha wanaume bado wataendelea na kusababisha wanawake warudi tena mtegoni! Kila jinsia inatakiwa ibadilike kwa nafasi yake na siyo kutegeana!