Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Nilishauri mwanzo kabisa vijana wa miaka ya 90 wangekuwa wasomaji wangejifunza mengi kwenye huu uzi.

Hamna mtu anayemfananisha Nyerere na Mwinyi kila mtu katawala kivyake.

Unasema Nyerere alijaribu kuiweka nchi kwenye mstari vikaibuka vita vya Uganda siyo?

Nyerere kachukuwa nchi mwaka 1960 vita vya Uganda vimetokea mwaka 1978.

Hiyo miaka 18 alikuwa anafanyaje kwenye utawala wake?
 
kwahiyo miaka 18 unaona ni mingi sana. kumbuka anaachiwa nchi alikuwa hana wataalamu wakutosha mfano wahandisi madaktari hata upande wa kiusalama bado wataalam hakuwanao wakutosha.

na ujue waliokuwa wanamezea mate rasilimali za taifa hili walikuwa ni wengi ndani na nje ya nchi, ila mwl nyerere kwa hekima kubwa sana alihakikisha rasilimali ya taifa hili itawanufaisha wa tz na hakuwa na haraka nayo.
 
Nyerere kapewa nchi na wakoloni nchi ipo vizuri.

Vita vya vya miezi minane ndiyo viliifanya Tanzania kuwa masikini?

Unajua kama Tanzania walilipwa?
 
Nimeacha kwenda kulala kwa kusoma hii taarifa

sasa je nini kilichotokea bbada ya hapo?
Je hawa vijana walikuwa na uhusiano wowote na akina McGhee waliotaka kumpindua Juliasi au hizi zilikuwa 2 different incidents?
 
Ahsante malim...kwa kuweka bayana kuhusu mafanikio ya mwinyi hasa kuhusu uhuru wa vyombo vya habari
 
Nimeacha kwenda kulala kwa kusoma hii taarifa

sasa je nini kilichotokea bbada ya hapo?
Je hawa vijana walikuwa na uhusiano wowote na akina McGhee waliotaka kumpindua Juliasi au hizi zilikuwa 2 different incidents?
Akizungumza kupitia katika redio ya ndege hiyo, mmoja wa watekaji wa ndege hiyo alijitambulisha kwa jina la Luteni Wami, ofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.Alisema kuwa ni lazima Rais Nyerere ajiuzulu vinginevyo ndege hiyo italipuliwa. Dk Ouko alijaribu kujadiliana na mtekaji huyo, lakini alijibiwa: “Tayari nimeshaua abiria watatu na nitaendelea kuwaua wengine zaidi.”

Dk Ouko alistushwa na kauli hiyo. Ilimbidi amsihi mtekaji huyo akimwambia, “Usiendelee kuua zaidi.” Lakini ukweli wa mambo ni kwamba hakuna mauaji yoyote yaliyokuwa yametokea mpaka wakati huo.Kupitia mawasiliano yao ya redio ya upepo, mtekaji huyo alimwambia Waziri Ouko hivi: “Sasa namuua huyu rubani.” Rubani mwingine aliyekuwa akisaidiana na Kepteni Deo Mazula ni Oscar Mwamwaja (kuna vyombo vingine vya habari vya Ulaya vilimtaja kwa jina la Mwangala Jotham).

Lakini Dk Ouko akamjibu kwa kumwambia kuwa huo utakuwa ujinga kwa sababu “…rubani huyo atahitajika kuirusha ndege hiyo kwenda kwingineko.” Mtekaji huyo akajibu: “N’naweza kuendesha ndege hii mwenyewe. Mimi ni luteni wa anga.”Watekaji hao walitaka ndege hiyo ijazwe mafuta kwa ajili ya safari ya kwenda Saudi Arabia. Akiwa hana lingine la kufanya, Waziri Ouko alikubaliana na matakwa hayo.Wakati huo huo katika mji wa Dar es Salaam, kumbukumbu za kijeshi zilianza kuchunguzwa kutafuta jina la Luteni Wami. Jina hilo halikupatikana popote. Wala hakukuwa na cheo chochote cha uluteni wa anga katika jeshi la Tanzania.

Nikipata wasaa takumalizia...
 
Hahaaaaaaahaaaaa..mkuu unanchekesha sana..ingawa ilikuwa hali ngumu kipindi hiko
 
Ahsante malim...kwa kuweka bayana kuhusu mafanikio ya mwinyi hasa kuhusu uhuru wa vyombo vya habari
Inaposemwa mfumo wa vyama vingi ulirudi tena mwaka 1992, huenda vijana wadogo wanashindwa kuelewa. Ni kwamba Vyama vingi vilikuwepo hadi mwanzoni mwa miaka ya uhuru lakini Serikali ya Nyerere ikavifutilia mbali.

Serikali ya Mwinyi ndiyo iliyorudisha tena mfumo huo hata kama ni kwa shinikizo la Mataifa ya Magharibi. Karibu vyama vyote vikubwa vya Siasa vya Upinzani vilianza shughuli zao katika kipindi cha Mwinyi.

Mwinyi aliondoka madarakani mwaka 1995, miaka mitatu baada ya Mfumo wa Vyama vingi kuanza. Alikuwa ni baba wa mageuzi ya kisiasa, na baba wa Uhuru wa Vyombo vya habari.
 
Wengine wazazi wetu walifungwa kwa kudhaniwa kuhujumu uchumi eti wamekutwa na vyakula kutoka nje ya nchi!
Bro...kuna mzee mmoja nilikutana nae kule njombe ndani kuna kijiji.kinaitwa kidugala yeye alisema alikuwa tajiri sana nyakati hizo ilipofika suala la uhujumu uchumi lilimuathiri sana kwani ilimlazimu kuendesha matrekta na gari lake kwwnda kuyatupa mashambani ukiachilia kuwa alivimiliki kihalali nchi hii imetoka mbali
 
Nimeacha kwenda kulala kwa kusoma hii taarifa

sasa je nini kilichotokea bbada ya hapo?
Je hawa vijana walikuwa na uhusiano wowote na akina McGhee waliotaka kumpindua Juliasi au hizi zilikuwa 2 different incidents?
Two different incidents.
 
Braza...hapo kuna kitu mzee inabidi atufundishe inshallah..sasa tatizo.waandishi wa habari hawana la msingi la kumhoji huyu mzee zaidi ya kuuuliza kwa nini unaitwa mzee ruksa...mwaka jana huyu mzee tumetembea naye kilometa nyingi kwwny matembezi ya hisani yaliyoandaliwa na rotary yaan ana nguvu kubwa ametembea kwa spidi ile ile km nyingi sana...vijana wanakula chips walichemka wakati miaka yao ni kuzaliwa 95.
 
Mkuu tafadhali iongezee nyama hio habari nipate kuifahamu vizuri..
 
Kuruhusu kitimoto kuuzwa hadi karibu na misikitiki bila ya kubagua imani za watu
 
Ritz, naona na wewe umeamua kuandika historia mpya ya Tanzania baada ya uhuru kama yule kakayo naye alipoamua kuandika historia mpya ya Tanganyika kabla ya uhuru ha ha haa? Yeye anadai pororjo anazoandika alisimuliwa barazani na wazee wake wa Gerezani, je wewe nani alikusimulia hizi porojo unazowapa vijana?

Kama kawaida naona vijana wako nao badala ya barazani wamehamia JF kusikiliza porojo zako wanameza tu bila kuhoji. Nakutakia kila la kheri kwani hata humu limbukeni wapo kibao wamejaa tele.
 
Mkuu tafadhari endelea
 

Baki na hadithi yako ya kwenye gazeti la RAI miaka hio.
 


Unafiki ni nguzo kuu ya kuwa mwanachama wa CCM.

Je, hayo yote uliyoyataja kwa kumsifia Mzee Ruksa ambayo yanaenziwa na kupiganiwa na wanasisiemu wa leo wanaotamani kumtafuna yeyote anayeikosoa serikali?

Yote uliyoyataja ni ya kweli na ndiyo msingi wa utu na maisha bora kwa kila binadam lakini awamu hii ya tano inayaacha kwa kasi ya ajabu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…