Kutokana na hali ya kisiasa ilivyokuwa ikiendelea tangu kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika, kuna watu walioona kuwa hawaridhishwi na Serikali ya Mwalimu Nyerere, hasa vijana kiasi cha kujasiria hata kuteka ndege ya abiria kwa lengo la kuishinikiza Serikali kufuata matakwa yao. Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania, Boeing 737, ilitekwa mjini Mwanza na vijana watano wa Dar es Salaam.
Baadaye ilikuja kujulikana kuwa majina ya watekaji wale ni Musa Memba (25), Mohamed Ali Abdallah (26) na ndugu yake Abdallah Ali Abdallah (22), Mohamed Tahir Ahmed (21) na Yassin Memba (21). Kiongozi wao alikuwa Musa Memba.
Kama utakuwa na muda takupa dondoo kiduchu.