Legacy ya Rais Mstaafu Awamu ya Nne, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete

Huyu jamaa ndio aliowafanya CCM mafisadi wa CCM wahisi mali ya uma pamoja na rasilimali za taifa ni haki yao, na wakaanza kuchota bila ya kificho tena
Bado KIKWETE anabaki kuwa mmoja wa VIONGOZI very liberal, democratic, shortcomings zake haziwezi kumeza mazuri yake mengi kama kiongozi Mstaafu wa Taifa hili.


A)Leo anafungua hoteli ya kitalii nyota Tano Arusha, kesho TANROAD wanbomoa ukuta wa fance wa hoteli hiyohiyo ambao umejengwa reserved area.
Lakini hamna afisa wa TANROAD alyefukuzwankazi.


B) Kikwete msafara nwa magari yake yanazima ghafla kisa mafuta yaliyochakachiliwa, lakini hatukusika mtu Kufukuzwa kazi.

C) Anakabidhi mfano wa hundi inayotofautiana kiasi Cha pesa figure na maneno,lakini anakuwa mvumilivu hamna mtu Kufukuzwa kazi.

D) Anabidhi maamburace Ikulu kwa halmashauri mbalimbali, anakuja Mkurugenzi wa halmashauri aambaye amealikwa lakini halmashauri yake haimo katika list ya halmashauri za kukabidhiwa amburance.

E) A napewa ku sign muswada ambao Bado bungeni haujajadiliwa, unarudi Tena bungeni,lakini hakuna mtu kafukuzwa kazi.

F) Msafara wake UNASHAMBULIWA kwa mawe Mbeya, lakini anavumilia na anapeleka maendeleo Mbeya.

G) Anachorwa Katuni za kuudhi,zinaamdikwa makala za kumkosoa na kumpondea kupita kiasi, lakini hakuna gazeti ambalo lilifungiwa kwa ajili ya kumkosoa yeye personally au kama kiongozi.


MAMBO hayo yote KIKWETE, Mwinyi walivumilia ,lakini marehemu KAMBALE na Mama Kizimkazi hawawezi kuvumilia kukosolewa.

Mwacheni kikwete apewe maua yake akiwa hai.

Kuna Msemo wa Kiingereza una hivi
"GIVE ME FLOWERS 🌺 BEFORE I DIE" nipeni maua yangu nkabla sijafa.

Tumpe zake heshima sifa JAKAYA MRISHO KIKWETE akiwa hai.🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺
 
Makamanda walimwita Vasco da Gama na Mnyika alidiriki kumwita dhaifu, leo hii hao hao wanabadili gia angani, ha ha ha. Kua uyaone😎😎
 
"Sio kama sisikii yanayosemwa au siambiwi yanasemwa bali .........." by Mzee wa Msoga
"Sio kwamba sisikii, wala sio kwamba siambiwi yanayosemwa, au sijui kusema, au sina la kusema! La hasha! Sijafanya hivyo kwa sababu sioni faida yake"
 

Haya mambo mengi uliyoyaandika ni sifa mbaya za incompetent leader na sio sifa za kiongozi makini kushambuliwa na mawe ni failure ya intelligence na hayo mengine hayatakiwi kutokea. Kwenye uongozi imara, thabiti.
 
Hii ndiyo legacy halisi ya kikwete. Huwezi kuandika legacy ya huyu jamaa bila kuambatanisha na miufisadi yake. Legacy ya aina hiyo itakuwa mfu.
 
Hii ndiyo legacy halisi ya kikwete. Huwezi kuandika legacy ya huyu jamaa bila kuambatanisha na miufisadi yake. Legacy ya aina hiyo itakuwa mfu.
Na hapo ni kwa uchache tu yule mzee tabasamu lake huwa linaficha mengi sana. Kumbuka pia watu walikuwa wanaondolewa kimyakimya mpaka hata mawaziri wake. Kumbuka kilichomkuta waziri Mgimwa yaani kipindi chake ufisadi ulikuwa ni sehemu ya maisha na hata huduma maofisini zilitolewa kwa upendeleo mkubwa mno. Yaani ilikuwa ukiingia ofisi ya umma watu wanakuona kama kinyago tu wafanyakazi wa ofisi wako busy tu na smartphone.

Ni kweli viongozi wote au marais wote walikuwa na ubovu wao ila JK mi huwa naona ndo alikuwa rais mbovu kuwahi kutokea nchini maana hakuwa na uchungu kabisa na taifa hili.

Magu alipambana sana mzee wa watu na alikuwa na uzalendo mkubwa kwa nchi yake kilichokuwa kinamwangusha ni kukurupuka na kutokuwa na approach nzuri ya kushughulika na mfumocorrupt. Alijitahidi sana kuwatoa walioizoea ccm na ni katika kipindi chake ndipo hata mtoto wa Chitoholi huko Mtwara angeweza kupata nafasi nyeti serikalini bila kujuana sana na watu.

Sema kakuta nchi na hata usalama wa taifa ulikuwa unaamini katika rushwa na kubeba watoto wa wenye majina na mbaya zaidi akaanza kufanya maamuzi kingumbalu otherwise nchi ilikuwa inapiga hatua ndefu na za haraka katika maendeleo na nidhamu serikalini ilitamalaki ndiyo maana si rahisi kulitoa jina lake kwa watu wa kawaida ambao wanategemea huduma zitolewe bila upendeleo.
 
Ni wakati slogan ya chukua chako mapema iliasisiwa na kuishika Kasi
 
Kweli mzee apewe maua yake. Raisi wangu wa muda wote kwa sasa tz ni huyu.
 
Jikono Jandama aliuua sana uchumi - Sector ya ujenzi/Real estate ilianguka kipindi chake....Nakumbuka enzi za Jeikei ukitangaza kuuza kiwanja haizidi wiki mbili unapata mteja tena bei nzuri tu.
 
Ufisadi wa kihistoria wa taifa hili umeasisiwa wakati wake.

watu walikua wanaiba pesa, wanasema hela ya mboga na hawachukuliwi hatua yoyote, utasema yule alikua kiongozi kweli?
 
Ukiwa mpiga mapambio huwezi kuuona uhalisia

Rais alieongoza kwa kashfa za ufisadi kuliko rais yeyote, na kuzitetea hadharani eti ni nafuu?

Itakua unatania.
Wewe una TATIZO MOJA KUBWA ,unakosa analytical skills, kama huna analytical skills, huwezi kuwa na uwezo wa kuchanganua, kupambanua issue, ideas na kufanya proper comparison.

Samia ni DALALI wa maliasili bza nchi, utawala bora democracy kwake ni shida.

Ufisadi wa KUTISHA kuliko awamu yoyote ile ile,ndo maana bungee limezuiwa kujadili kwa uwazi report wa wizi wa Fedha za Serikali.

Miaka yake takriban mitatu amekopa beyond, amefikisha deni kubwa kuliko awamu zote zilizotangulia.

Utawala bora kwake ni shida, akili yake ipo kwenye urais, yeyote ambaye anaonekana threat kwenye URAI kwake huyo anastahili KUFA.

Ni aibu kwa RAIS WA nchi kukimbia kuhudhuria UNGA United Nations General Assembly,baada bya kuropoka kuhusu mabalozi na nchi zao, mauaji na kutekwa watu, anakimbia anaogopa mabango na maswali ya wanahabari wa Ng'ambo na wanaharakati, badala yake anaenda kufanya ziara ya ndani,kuliko kikao kikubwa mara moja kinachokutanisha wakuu wa nchi na kujadili very potential Cross cutting issues za mustakabali wa Taifa.

Kiongozi fisadi ni yule anayeidhinisha Viongozi KULA KWA UREFU WA KAMBA, then baadae anawatukana STUPIDY 🤣😅🤣😅

Wewe nikikuita BUMUNDA nitakuwa nimekosea??BUMUNDA tu ndo haliwezi kuona utawala hovyo wa HANGAYA.
 
Ni katika kipindi chake ndiyo vijana wengi wasiokuwa na kitu waliibuka na kupata ubunge.

1. Masele.
2. Mnyika.
3. Zitto.
4. Mwita Waitara.
5. Kafulila.
6. Mdee.
7. Bulaya.
N.k.
 
Haya mambo mengi uliyoyaandika ni sifa mbaya za incompetent leader na sio sifa za kiongozi makini kushambuliwa na mawe ni failure ya intelligence na hayo mengine hayatakiwi kutokea. Kwenye uongozi imara, thabiti.
Kwa nchi na Viongozi wanaojitambua kama JK , katika democratic arena ni kawaida.

Marais, wafalme, kuchorwa vikatuni, kutupiwa mayai mambovu na nyanya zilizoooza,na kwenda kubadili mavazi na kurekebisha mambo kwa utawala kama walikengeuka katika jambo.
 
Kabisa Kikwete alikuwa rais bora kabisa pengine kuliko hata Nyerere!
 
Uongo tupu, hasa number 9, mahakama zilitengua Kesi majimbo mengi ya CCM, na kupewa ushindi upinzani hasa CHADEMA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…