1. Ikiwa ni msomaji wa Neno utaelewa nisemacho kuwa, baada ya Yesu kufufuka, makaburi yalifunguka, wafu waliokufa katika Imani ya Mungu,walirudi Toka Paradise na kufufuliwa na kupaa naye mbinguni, wapo huko wakisubiri siku ya mwisho,na hao ni WATAKATIFU hawahukumiwi, watahukumu wenye dhambi pamoja na Kristo, YESHUA aliwambia wanafunzi wake direct juu ya wao kuhukumu Hadi Malaika waasi.
Imeandikwa Yesu atakuja kuhukumu Ulimwengu akiambatana na WATAKATIFU wake, ndio hao nisemao walipaa Mbinguni baada ya kufa na hawakai kaburini, na hawahukumiwi hao.
2. Mavazi machafu, imeandikwa baada ya wateule kunyakuliwa, watabaki walioachwa, wengine ni wakristo waamini lakini hawakuacha dhambi, anasali lakini Bado mwongo, Mwizi nk nk. Hawa wanalo vazi ila chafu sababu ya DHAMBI, wengine ni Waisrael,wao wanalo AGANO na Mungu la kuokolewa, Hawa watapita katika dhiki kuu na kuteswa na shetani na mapepo lakini kamwe hawatakubali KUPIGWA chapa ya mnyama, watauwawa Kisha watakaa kaburini kusubiri siku Yesu arudipo awafufue na kuondoka naye. Hapo utaona Unyakuo ufanyikapo, Yesu hatokanyaga ardhi, atawanyakua akiwa juu, kipindi Cha dhiki kuu, atakuja akiwa na jeshi na walionyakuliwa na wale wengine ambao tayari wapo Mbinguni WANADAMU WATAKATIFU Kisha watajumuika na waliokatwa vichwa kwenye dhiki kuu.
3. Ndio shetani atarudi tena kuwadanganya WANADAMU. Ni hivi, hapa tulipo, shetani amefungwa kuzimu, lakini Kwa kuwa kuzimu alikofungwa ni sehemu mojawapo ya Dunia hii, na Kwa kuwa shetani ni Roho, ujue kuwa kifungo chake ni katika mipaka ya kufanya KAZI, ni kama tu aliyefungwa kifungo Cha nje.
Kufungwa Kwa shetani ni Kweli kafungwa, lakini hajanyanganywa nguvu zake, anazo na huko alikofungiwa amepewa kujitawala katika gereza lake na ameruhusiwa kuwajaribu WANADAMU na kuwatesa akiwa gerezani,kifungo chake Kiko katika limits.
Utaona shetani akiomba ruhusa kumjaribu Ayubu, na aliporuhusiwa, aliambiwa, nenda, mjaribu ila usimuue, hapo utaona shetani katika kifungo chake, amepewa mamlaka kiasi lakini chini ya uangalizi.
Limit ya nguvu za shetani imewekwa na Mungu sababu sisi watu wa Mungu tunaishi duniani, baada ya Unyakuo, shetani ataruhusiwa kuitifua Dunia na wakaao ndani yake, ndicho kipindi kiitwacho DHIKI kuu, hapo Dunia itatikiswa Hasa, shetani atawapiga waliomkataa Yesu Kwa mapigo mabaya sana, ndio maana ya kufunguliwa, yaani hatawekewa mipaka, Malaika watamwacha ajitanue Kwa muda. Kipindi hili shetani atakuja live, Si Kwa kificho kama sasa, mapepo yataonekana live na Majeshi ya kuzimu yatakuwa on, ni hatari kuwepo duniani wakati huo.
4. Miaka 1000 ni hesabu ya kidunia. Katika hesabu za kinabii, mwaka 2000 ni mwaka wa elfu SITA, siku ya SITA. Na mwaka huu 2024 maana yake tayari tupo mwaka wa ishirini na nne ndani ya ya miaka 1000 iliyobaki.
Kwa maana ingine, Unyakuo utatokea miaka michache ijayo, Si mingi, utaona maandalizi ya kuanza utawala wa shetani duniani, na kuanza Rasmi utawala huo, lazima kwanza Unyakuo utokee. Angalizo weka na tofautisha, DHIKI na DHIKI KUU. Hapa tulipo tupo katika DHIKI, dhiki kuu Bado.
Ndani ya miaka hii hii kuanzia 2024 Hadi 2099. Yaani Dunia haitafika mwaka 3000 kabla kufanyika Unyakuo na kabla Dunia haijatupwa JEHANUM.
Ni katika kipindi hiki umekaribia Kutokea Unyakuo Ili uanze utawala wa shetani duniani Kwa muda mchache, Kisha shetani na Majeshi yake watakapojikusanya Kwa vita ya ARMAGEDDON, vita hii Si ya WANADAMU, ni Majeshi ya Pepo, mashetani, watu nusu mtu nusu shetani, wachawi nk nk ambao watakuwa wamebadilika kuwa na miili ya kiroho kuja Kupambana na Majeshi ya Mungu na Wachache ambao wamekataa chapa ya Shetani, hapo Yesu atashusha moto na kuwateketeza, ni kabla ya mwaka 3000. Baada ya kuteketezwa, ndio miaka hiyo 1000 ambapo Kwa hesabu tulizopo, miaka hiyo imeshapungua maana Unyakuo haujatokea Hadi sasa. Hivyo kutawala na Kristo miaka ni hii iliyobaki kabla ya kutimia mwaka 3000 ambao Dunia itakuwa imeshaangamizwa na siku ya Saba yaani mwaka 3000 na kuendelea ni mwaka wa umilele, hapakuwa na time tena au muda na miaka ya kuhesabika, watachomeka milele JEHANUM, na wengine watatawala milele katika Jerusalem mpya, ambayo Yesu anaendelea kutuandalia.
5. Kweli, wapo walioandikiwa motoni tangu kuumbwa Dunia. Lakini wewe
undercover Si mmoja wao wa walioandikiwa moto. Uliandikiwa uende Mbinguni iliko asili Yako, umeletwa duniani Kwa special mission, usikubali shetani akutoe kwenye mission Yako, utaona kuwa wewe unepewa uhuru wa kuamua uende Mbinguni iliko Toka, au uende JEHANUM alikopangiwa aende shetani na Malaika zake waovu wenzie.
Ni hivi, shetani na mapepo na waliokuwa Malaika na wakaasi, hawana nafasi ya kutubu, hivyo wanajua destiny Yao ni JEHANUM.
Pili, walioandikiwa JEHANUM direct ni mapepo yaliyo katika form ya mwanadamu, Hawa wapo wengi na tunaishi nao,
Na Hawa wanajitahidi kuchanganya uzao wao na uzao wa Adam, unakuta shetani anamwingilia mwanamke mchawi na kuzaa mtoto ambaye ni Pepo ambaye baba ni shetani , mama mwanadamu. Sasa watoto na uzao huu, Mungu haxhangamani nao, Hawa hata uhubiri asubuhi Hadi jioni hawezi kuokoka Wala kupenda au kutenda ya Mungu, asili Yao ni kuzimu, huyatimiza mapenzi ya baba Yao shetani.
Nadhani sasa unaanzaje kupata mwanga.
Wapo pia WANADAMU ambao asili Yao ni Mbinguni tunaishi nao,
Yohana Mbatizaji, Elia, Henoko, na manabii wengi walitoka Mbinguni Kisha kuletwa duniani Kwa mission maalum,
Mfano Mimi
Rabbon, hata iweje, ndani yangu na asili yangu Toka Mbinguni always hunikumbusha na kunirejeza kwenye mstari Ili kutimiza kusudi la Mungu duniani.
Jitahidi kuwafahamu wanaokuzunguka ikiwa ni uzao Toka juu Mbinguni au uzao Toka chini, mbegu ya kishetani,
Makinika, Si Kila umwonaye ni mwanadamu, wengine ni mapepo, wengine Malaika, wengine mashetani, wengine nusu mtu nusu Pepo, wengine majini nk nk.
Ubarikiwe