Legacy ya Rais Mstaafu Awamu ya Nne, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete

Legacy ya Rais Mstaafu Awamu ya Nne, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete

Nachukua fursa hii kusema yafuatayo kuhusu Rais Mstaafu Awamu ya 4 Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.

1. Aliishi Katiba na Demokrasia kwa vitendo.
2. Alistawisha demokrasia ya vyama vingi.
3. Aliamini katika checks and balances mahakama na bunge vilikuwa huru.
4. Aliboresha mishshara ya watumishi wa umma kuliko awamu zote na itakuwa hivyo milele na milele hakuna kama Kikwete.
5. Aliishi cheo cha Urais kwa Busara, Hekima, Ukomavu, Usikivu, na utulivu.
6. Alijua kutukanwa, kejeli dhidi yake si chochote na hapungukiwi kitu.
7. Alikuwa ni Rais ambaye aliheshimu wasaidizi wake.
8. Alifahamu na anafahamu katika nchi Siasa na Demokrasia sio Uadui.
9. Ni Rais ambaye aliamini katika uwezo na ushauri wa wasaidizi wake.
10. Awamu yake Bunge lilikuwa bunge kweli na Uhuru wa Mahakama tulishuhudia rufaa kadhaa za kutengua ushindi wa wabunge wa CCM.
11. Awamu ya 4 ndio wakati ambao Tanzania ilikuwa nchi ya multiparty democracy, good governance, na katiba ikiheshimika.
12. Hakuwa Rais aina ya Mfalme na hakuvimba kuwa Rais wa nchi.
13. Utawala wa Kikwete uliishi bayana mipaka ya Serikali, Bunge na Mahakama.
14. Alidumisha heshima ya Tanzania kama peaceful and diplomatic state

Kwa dhati ya moyo wangu namshukuru kwa hayo namuombea maisha marefu sana.

Nukuu ya siku "Asiyesikia la Mkuu huvunjika Guu"

Wadiz
nimeamini shilingi ina pande mbili, leo mnataja mema yake ila mababaya yake hamsemi
 
Tutamkumbuka kwa kupitisha muswada kwa hati ya dharura kuhusu gesi. Enzi za JK kulikuwa na upigaji uliokithiri. Ujanja aliofanya ni kugundua kuwa wapinzani nao wanachotaka ni kuingia ikulu na kujichotea rasilimali za nchi hivyo akawapumbaza na demokrasia. Zile chai za ikulu walizifurahia sana.
Hujui kitu kuhusu Kikwete kaa kwa kutulia huyo ni Iconic figure ya Tanzania
 
Merermeta,IPTL,mapesa ya gadafi,kuuza gesi yetu ya mtwara Kwa mabeberu na sisi wananchi kuuziwa bei ya juu zaidi ya mara saba ya bei wanavyonunua mabeberu,kugunduliwa Kwa mafuta Zanzibar na kuyatoa kwenye masuala ya muungano ili Zanzibar inufaike peke yake,kuuza shirika reli Kwa wahindi na baadae magufuli kuliokoa,kuua shirika la ndege na kubakiza Moja mikweche,kuongezeka Kwa wauzaji wa madawa ya kulevya na madudu mengine mengi
 
Nachukua fursa hii kusema yafuatayo kuhusu Rais Mstaafu Awamu ya 4 Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.

1. Aliishi Katiba na Demokrasia kwa vitendo.
2. Alistawisha demokrasia ya vyama vingi.
3. Aliamini katika checks and balances mahakama na bunge vilikuwa huru.
4. Aliboresha mishshara ya watumishi wa umma kuliko awamu zote na itakuwa hivyo milele na milele hakuna kama Kikwete.
5. Aliishi cheo cha Urais kwa Busara, Hekima, Ukomavu, Usikivu, na utulivu.
6. Alijua kutukanwa, kejeli dhidi yake si chochote na hapungukiwi kitu.
7. Alikuwa ni Rais ambaye aliheshimu wasaidizi wake.
8. Alifahamu na anafahamu katika nchi Siasa na Demokrasia sio Uadui.
9. Ni Rais ambaye aliamini katika uwezo na ushauri wa wasaidizi wake.
10. Awamu yake Bunge lilikuwa bunge kweli na Uhuru wa Mahakama tulishuhudia rufaa kadhaa za kutengua ushindi wa wabunge wa CCM.
11. Awamu ya 4 ndio wakati ambao Tanzania ilikuwa nchi ya multiparty democracy, good governance, na katiba ikiheshimika.
12. Hakuwa Rais aina ya Mfalme na hakuvimba kuwa Rais wa nchi.
13. Utawala wa Kikwete uliishi bayana mipaka ya Serikali, Bunge na Mahakama.
14. Alidumisha heshima ya Tanzania kama peaceful and diplomatic state

Kwa dhati ya moyo wangu namshukuru kwa hayo namuombea maisha marefu sana.

Nukuu ya siku "Asiyesikia la Mkuu huvunjika Guu"

Wadiz
Well.

The same ana regancy ya mambo yafuatayo.
- aliasisi siasa za vurugu,kejeri,na kukomoana
-mafisadi mlipata uhuru haijawahi na haitatokea
 
Mnazi bay ni eneo moja, gesi mtwara inachimbwa maeneo mengi. Ndio wanaosema imeuzwa sababu hatuna umiliki maeneo mengi, mm sipendi kusema imeuzwa sababu hatuna uwezo wa kufanya tafiti wala kuchimba
Maeneo mengi mengine yapi?..kampuni gani inachimba huko
 
Merermeta,IPTL,mapesa ya gadafi,kuuza gesi yetu ya mtwara Kwa mabeberu na sisi wananchi kuuziwa bei ya juu zaidi ya mara saba ya bei wanavyonunua mabeberu,kugunduliwa Kwa mafuta Zanzibar na kuyatoa kwenye masuala ya muungano ili Zanzibar inufaike peke yake,kuuza shirika reli Kwa wahindi na baadae magufuli kuliokoa,kuua shirika la ndege na kubakiza Moja mikweche,kuongezeka Kwa wauzaji wa madawa ya kulevya na madudu mengine mengi
Gas gani ya mtwara imeuzwa wazee?.. mbona mnaimba vitu kikasuku?
 
Ni katika kipindi chake pia ambapo
1. Dr Ulimboka aliuawa
2. Mwangosi aliuawa
3. Wanyama wakiwa hai walisafirishwa kwenda nje ya nchi
4. Tanzania ilikuwa hub ya madawa ya kulevya duniani
5. Mabomu yalilindima na kuua watu kadhaa huko Olasti Arusha
6. Wageni walijichotea rasilimali za taifa walivyoweza.
7. Ni wakati huohuo ambapo tembo na wanyama wengine wakubwa walipata shida sana.
8. Wizi mkubwa wa rasilimali za nchi ulifanyika kupitia Meremeta, Tangold, Escrow, Richmond, Kagoda nk nk nk
9. Ni wakati huohuo pia ambapo kama mtu hukuwa na pesa usingeweza kuipata haki yako popote.
10. Ni wakati huohuo ambapo mawaziri walitumia rasilimali za nchi hii kutibisha vimada wao ulaya.
11. Na mengine mengi mabaya yalifanyika kipindi hicho.

Tunatakiwa tufike mahali kama taifa tujue CCM haiwezi kuwa na mema kwa taifa hili kuna haja ya usalama wa taifa wa taifa hili kutafuta kiongozi ambaye atakuja kufumua utaratibu huu mbovu wa kuwapata viongozi wa nchi hii. Na ikiwezekana angalau kuwe na vyama viwili vitakavyopokezana uongozi wa nchi hii na vyote viwe treated equally. Huu utaratibu wa sasa haujakaa kikulisaidia taifa bali upo kwa ajili ya kutukuza mfumo fulani wa uongozi na tunakoelekea hata idara zetu za kulilinda taifa zitakuwa zimemezwa na ccm kitu ambacho ni hatari sana kwa ustawi wa taifa.

Tanzania itaishi milele sisi sote na vizazi vyetu tutatoweka lakini inapendeza sana taifa litakapokuwa na misingi bora na imara ili hata vizazi vitakavyokuja baada ya mwaka 3000 vijue kuna mababu waliwahi kuishi nchi hii walilitendea vyema taifa ndiyo maana leo hii Tanzania inaongoza kiuchumi duniani maana you never know maisha haya yanabadilika na Mungu anabariki taifa linalokuwa na maadili yanayompendeza.

Ahsante.
Bora ume Wakumbusha mkuu hawa wapumbavu!

Magufuli pamoja na ukali wake hakuwahi kutumia mabomu ya kivita ila JK aliyatumia pale Olasiti Arusha
 
Maeneo mengi mengine yapi?..kampuni gani inachimba huko
Zipo kampuni nyingi zinachimba gesi huko. BG, ophir, Exxon n.k
Tpdc ananunua kwao, alafu tpdc anaiuzia tanesco. Tanzania haina umiliki sababu haikuwekeza kwenye utafiti na uchimbaji.

Kama unavyoona gas ya lindi ambayo tunataka tuwape Exxon, mradi gharama yake ni Trillion 100. Hiyo pesa hatuna ndio tunawapa hao, wanatafiti wanachimba wakianza uzalishaji wanatuuzia sisi na wanauzia wengine. Kwa kifupi hatuna uwezo wala pesa
 
JK ni mfano wa mtu wa kuigwa kuvumilia maneno pinzani na kujikita kutimiza wajibu bila kumuumiza mpinzani.

Hakuna mkamilifu dunian, JK apewe heshima yake.
Mwanahalisi washawahi andika "Vasco Dagama" safarini ughaibuni, na halikuwahi kufungiwa!!! Jamaa ni mvumilivu na anajua sana Siasa!! Diplomasia!!
 
Ila chama kilikua kina karibia kuteketea mikononi mwake na kwa mara ya kwanza tulikua tunakaribia civil unrest.

Kama yale yaliyokuwa yanaendelea kwake yangeendelea kufanyika kwa miaka mingine mitano tu, watu wangeingia barabarani.

Matajiri walikua wachache wenye ukwasi mkubwa sana na rundo la maskini wasiokuwa na future.

Falsafa ya Magu ilipoza hasira za wanyonge na kutengeneza hali ya usawa mambo yakapoa kidogo.

Samia nae akisema aige staili yake naamini baada ya muda raia watashindwa vumilia.

Cha kufanya kwa Samia, achague kuwa karibu na wananchi, ziara kama hizi za mikoani aziongeze watu wamuelewe.

Asijifungie ndani tu na kukutana na hao mabwanyenye, aende kwa watu wa chini.
 
Back
Top Bottom