Legacy zinavyopotea haraka, nahisi huruma

Nini kinawafanya mumuite Magu shujaa wa Afrika?
Walijaribu kulazimisha lakini imekataa. Huko bungeni nako akina Jah people, Kibajaji na Msukuma darasa la 7 B, wamejaribu kuweka pambio la kumtukuza JIWE kwa nguvu, naona wabunge wenye akili kubwa ndani ya CCM humo humo wamewabeza. Eti wanalazimisha mama aendeleze ya JIWE. Ni kama vile mama hana uwezo wa kupanga nini kitawafaa waTanzania. Kila kitabu na zama zake, aachwe Mama Samia aandike KITABU chake.
 
Juhudi ya 16% ya watanzania haiwezi uwa legacy ya JPM

Magufuli ndio kwanza anachipua na kuchanua katika mashina ya watanzania zaidi ya 84%

JPM aliishi, anaishi na ataendelea kuishi...... mnaoumia na kupambana asahaulike mtakufa kwa kihoro
Lilikuwa jizi la kura, hiyo 84% sio watanzania, bali kapewa na vyombo vya dola vilivyokuwa vinamsujudia.
 
Unajitahidi kujifariji kwamba JIWE litakuja kukumbukwa kwa mazuri? Jiulize, kwa nini hiyo Legacy inalazimishwa?

Inalazimishwaje kijana!!!

Hata ukimtukana jk nyerere saa hizi utakamatwa,huko ni kulazimishwa!!!!
 
walisema nchi haitaenda bila yeye,ila naona siku zinayoyoma tu...
 
Umemaliza 🙌🙌👏👏!!
 
Ni kweli, ila sio kwa Level ya jiwe.

sijui umepimaje!!!

ila enzi za nyerere kuna watu walitamka hadharani kwamba nchi iko mifukoni mwao,hicho ni kiwango cha juu zaidi kupuuza nguvu ya rais.
 
Kwani legacy ni lazima iwe nzuri tu? Unamaanisha tutashindwa kumkumbuka hata kwa kuingiza mfumo mpya wa watu wanaomkosoa Rais kupotezwa, kuuawa au kushambuliwa kama alivyofanyiwa Lisu?
 
Amelaaniwa kabisa!! Umri huu nilikuwa sijawahi ona mtu akifa watu wanafanya sherehe.. nimeona kwa huyu mwendazake

Kristu alikufa miaka 2000 iliyopita na kifo chake ni sherehe pia.

Ishu hapa unasherehekea ukombozi!!au unasherehekea umasikini ulio nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…