Lema amekua Panya sasa, anang'ata na kupuliza

Lema amekua Panya sasa, anang'ata na kupuliza

Rungwe88

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2013
Posts
353
Reaction score
722
Nimesikiliza baadhi ya tuhuma, ushauri, mtazamo n.k alivyotoa Lema kuhusu mambo, vitu, watu n.k ila kwa kifupi ni kwamba maongezi yake ni dhaifu sana ikizingatiwa yametolewa na mtu kama yeye aliye kwenye siasa kwa miongo kadhaa.

Nitaelezea badae udhaifu wake ila kwa sasa nitakazia hoja yangu kwamba Lema ameshageuka kuwa Panya mharibifu ndani ya Chadema, sasa anang'ata na kupuliza.
Watu wenye akili ndani ya Chadema wanasubiri mda na njia sahihi ya kumtoa Panya ili wasije kuchoma Nyumba sababu ya Panya mmoja.

Mtazamo au ushauri wangu ni mmoja tu kwa Lema sasa, chagua moja kuwa ndani au nje ya Chadema sababu uliyoongea yanakiuka katiba na taratibu za Chadema katika namna nyingi.

Lema umeamua kufanya siasa chini ya uongozi wa Mwenyekiti Lisu hivyo siasa za udalali mlizozoea kufanya hazina nafasi kwa sasa, ukitaka hizo siasa subiri Lisu amalize awamu yake ugombee kuwa Mwenyekiti na kushinda ndio ufanye siasa za udalali, ila hakika wana Chadema hawatokupa hiyo nafasi sababu siasa unazotaka kufanya ndio zilizomuondoa kaka Yako Mbowe kwenye nafasi yakuwa Mwenyekiti Chadema.

Yafuatayo ni madhaifu ya hoja zako
1. Kuhusu Mange Kimambi kwamba anakutuhumu uongo kwenye uhusika wako kukihujumu Chadema.
Naweza kusema Mange Kimambi ni mtu wa haki, endapo ikikosekana CCM ataitafutia upande mwingine, hivyo udhaifu wako ni kutumia jukwaa la kofia ya Chadema kumuongelea Mange huo ni udhaifu sababu Mange hajawai kuwa mwanachama wa Chadema Bali ni mwanaharakati huru, kuihusisha Chadema na utofauti wako na Mange ni kutaka watu wa Chadema wamchukie Mange kwa sababu ya Mange kuongea dhidi ya usaliti wako kwa Chadema na baadhi ya wana Chadema.

2. Udhaifu wa pili ni kuhusu jambo la Joseph Mbilinyi kukata tamaa na uongozi ndani ya Chadema.
Hiyo unataka kuwaaminisha watanzania kwamba Chadema ya sasa chini ya Lisu ina matatizo kuliko Chadema ya udalali chini ya Mbowe?
Huo ni udhaifu wako wewe Lema na huyo mwenzio sugu sababu kama Kuna watu walitakiwa kukata tamaa basi ni Heche na Lisu ambao wanapata hekaheka kila siku kutoka kwa mafisadi, majizi, wauwaji n.k Toka CCM
Nafikiri unajua sababu ya Lisu kutokuweka kuwa sehemu ya mashahidi katika kesi yake.

3 . Udhaifu wa tatu ni wewe kuungwa mkono na watu wa CCM baada ya kuongea kwenye hiyo press conference yako.
CCM wanajua hiyo move Yako ndio maana wamekua wakikutetea kuanzia hapa JF Hadi kwenye vyombo vya habari tofauti.

4. Udhaifu mwingine kwenye press conference yako ni kutokemea matendo yaliyofanywa na CCM ikiwemo mauaji, utekaji, ufiraji n.k dhidi ya watanzania ila lawama umemtupia Mange Kimambi aliyehamasisha maandamano ya kudai haki za watanzania,
Wewe unataka Mange Kimambi aje kuzika watu waliouwawa na CCM, je ina maana haujui kwamba wapigania haki wengine kama Mange Kimambi akiwemo Polepole, Mdude, Kibao n.k wako wapi sasa?
Lema wewe ni kabila la wachaga ila sitaki kuamini kwamba wachaga wote hawaaminiki, wanatamaa, matapeli n.k kama ulivyo wewe na kaka Yako Mbowe.
N.k
Nitaelezea zaidi ila kwa sasa wewe Lema ni Panya unaeng'ata na kupuliza ila Bado unataka kuigiza kama mzalendo ndani ya Chadema
 
CCM imeshatafuta namna ya kukitawanya chama. Na watz tulivyo wazembe kuichakata taarifa lazima uingie mkenge tu. Hakuna mtu ambaye ana tamaa za kibinadamu hawezi I kuingia kwenye mfumo, na mange mwenyewe alisema, soon tunakwenda kuona haya yakitokea.

Watanzania kweli hatuna hata uwezo wa kukaa nje ya drama na kuangalia logic ya maneno? Ukakasi na manipulation ndo imekuwa nyenzo za KUWAPUMBAZA taifa lenye watu illiterate
 
Umeongea ukweli mtupu. Sijui Lema alilenga Nini kwenye Press yake ya Leo.
Nilitarajia mambo yenye upeo mkubwa hata kama yangewaumiza Chadema ila chakusikitisha ni kwamba kaongea mambo mepesi ambayo hata mtu wa shule ya msingi anaweza kuongea.
Ila chakufurahisha ni kwamba amejipambanua uhalisia wake kabla hajaleta hasara kubwa ndani ya chama, hivyo hiyo ni faida kwa uongozi wa Chadema sasa chini ya Mwenyekiti Lisu na makamu Heche
 
CCM imeshatafuta namna ya kukitawanya chama. Na watz tulivyo wazembe kuichakata taarifa lazima uingie mkenge tu. Hakuna mtu ambaye ana tamaa za kibinadamu hawezi I kuingia kwenye mfumo, na mange mwenyewe alisema, soon tunakwenda kuona haya yakitokea.

Watanzania kweli hatuna hata uwezo wa kukaa nje ya drama na kuangalia logic ya maneno? Ukakasi na manipulation ndo imekuwa nyenzo za KUWAPUMBAZA taifa lenye watu illiterate
Watu wameshajua mbivu na mbichi ni vile tu hawajashika mpini ndugu,
Ni kwamba Kuna watu ni smart sana na wengine wapo CCM wanamuona Lema hamnazo tu.
 
Back
Top Bottom