Lema amuomba Rais Samia kurejesha biashara ya Tanzanite Arusha

Lema amuomba Rais Samia kurejesha biashara ya Tanzanite Arusha

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
329f5f801f0c33f946caacdc68e9c92b--tanzanite-earrings-color-charts.jpg
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema amemuomba Rais Samia Suluhu kurejesha biashara ya madini ya Tanzanite ili ifanyike katika Jiji Arusha.

Lema amesema hayo leo Machi 4, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa lengo ni kukuza uchumi, ajira na biashara ya madini hayo

Mbunge huyo wa zamani wa Arusha Mjini amesema kuwa kuzuia kuuzwa nje ya Mererani madini ya Tanzanite ni kinyume cha sera ya biashara huria lakini pia kunadhofisha biashara hiyo.

“Mimi ushauri wangu ni kwamba, madini ya Tanzanite yauzwe kokote duniani na isionekane ni aina ya madini yanayonunuliwa na wazungu pekee”.amesema Lema.

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa Julai 7, 2021 wakati akizindua Kituo cha Tanzanite -Magufuli Mererani, alitangaza biashara ya Tanzanite kufanyika Mererani pekee ikiwa ni mkakati wa kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo.
 
Madini ni ya mrerani, yakiuzwa mererani Lema inamuuma nini? Arusha wana utalii, okalie utalii Tanzanite aiache Mererani.

Mbona hasemi Dhahabu ya Geita ikauzwe Singida?

Lema anapaswa kuchunguzwa, wa canada inawezekana wameshafanya yao wazungu sio watu wa masihara.
 
Dalali wa majangili ya Tanzanite kaanza rasmi kazi
 
Back
Top Bottom