PreGE2025 POTOSHI Lema asema Gwajima alitakiwa kupewa kesi ya uhaini, asema amefanya kitu kibaya hauwezi kuchanganya siasa na dini

PreGE2025 POTOSHI Lema asema Gwajima alitakiwa kupewa kesi ya uhaini, asema amefanya kitu kibaya hauwezi kuchanganya siasa na dini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1

Screenshot 2025-06-04 125945.png
 
Tunachokijua
Godbless Lema ni mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa chama hicho kanda ya Kaskazini.

Lema alifanya mahojiano na Jambo TV pamoja na Habari Digital, ambayo yalichapishwa katika mtandao wa youtube Juni 03, 2025 akizungumzia taarifa ya kufungiwa kwa kanisa linaloongozwa na kanisa la Askofu Josephat Gwajima

Ikumbukwe kuwa tarehe 24 Mei, 2025 Gwajima alifanya mkutano na waandishi wa habari ambapo alisema kumekuwa na mlolongo wa matukio ya watu kutekwa pamoja na kupotea hivyo kutokana na hayo, aliamua kuitisha mkutano na waandishi wa habari kuongelea kuhusu suala hilo na kisha kutoa ushauri wa namna ya kudhibiti matukio hayo.


Video iliyochapishwa mtandao wa TikTok kuhusu Lema

Kupitia mtandao wa TikTok, mtumiaji anayetumia jina la 'Mapinduzi 64' alichapisha kipande cha video kinachomuonesha Lema akisema 'Gwajima alitakiwa kupewa kesi ya uhaini, amefanya kitu kibaya sana na kitu cha laana sana'

Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?

Kupitia marejeo ya video ya mahojiano ya lema, Juni 03, 2025, JamiiCheck imejiridhisha kuwa taarifa hiyo imepotoshwa kwani inakinzana na uhalisia uliopo katika chanzo halisi cha video hiyo.

Video imehaririwa kwa kukata vipande kutoka video iliyowekwa mtandao wa Youtube ya Habari digital na kuviunganisha isivyostahili hatimaye kupotosha ujumbe ujumbe uliokusudiwa na Lema."

Sehemu ya mahojiano hayo Lema alisema

"Ni kiongozi wa kanisa, ila kanisa lina utaratibu wake, kanisa ni taasisi, maana yake kuna mchungaji msaidizi. Kama Gwajima kuna makosa ameyafanya yanayotosha kufungiwa kanisa, maana yake katika maneno yake kuna uhalifu. Sasa uhalifu, anashitakiwa kwa maneno yake anapelekwa mahakamani."

"Sasa unafungaje kanisa unamuacha Gwajima, Kama umepata kesi ya kufunga kanisa maana yake umepata kesi nyingine mbaya zaidi, uhalifu mwingine, mbona hamumkamati, hamumpeleki polisi, hamumpeleki mahakamani, hamumshtaki. Yaani Kama unaweza kulifunga kanisa kwa makosa aliyofanya Gwajima cha kwanza ilikuwa unamshtaki Gwajima kwa makosa aliyofanya, kama ni maneno ameongea, na hayo maneno yamehatarisha hicho unachokisema kwamba amechanganya siasa na dini maana yake atakayeenda kufafanua hiyo siyo msimamizi."

"Maana yake ni kwamba polisi itamkamata, itapeleka kesi kwa mwendesha mashtaka wa serikali alafu ataipeleka mahakamani, mahakama itaamua inaweza ikaona hii taasisi ni hatari. Mfano Askofu Bagonza anaikosoa serikali kila mara juu ya haki za binadamu, katoliki wanaikosoa kila mara serikali juu ya haki za binadamu, serikali hii inaweza kulifungia hilo kanisa?"


"Katika maneno ya Gwajima kama ni maneno 'strong' kwa kiasi hicho mpaka kanisa lifungwe maana yake Gwajima alitakiwa apewe kesi ya uhaini. Nimesikia anakemea mauaji, nimesikia anakemea utekaji, nimesikia anataja idadi ya watu waliotekwa wakiwemo wanachama wetu, hajasema uongo."

"Huyu mtumishi wa Mungu anasema haya mambo yakome na polisi msiwe 'comfotable' vyombo vya ulinzi na usalama msiwe 'comfotable' huyu amehuiri neno la Mungu kwa wakati sahihi actually amechelewa.. niliongea nae nikamwambia nakushukuru umepiga kelele lakini nikamwambia nakulaumu pengine ungeongea miezi nane iliyopita Mdude asingeuawa"

View: https://www.youtube.com/watch?v=KZIhhRvFzis&t=866s
​
Kukemea Maovu kwenye tawala kama ya Roman Empire ilikuwa ni Kosa hata Yesu aliuwawa baada ya Tawala kusikia Yesu ni Mfalme wa Wayahudi.. japo hawakuona kosa lake wakamsurubu msalabani.

Gwajima akiponyoka sijui kama nae atafufuka baada ya siku ya tatu.. let us watch.. Madking yalimkuta katika Historia ya Uited Kingdom
 
Kama umeshawi kusikia ikisemwa mtu huyu ana Akili ndogo, na unahangaika kujua wanajuaje kwamba mtu Fulani ana Akili ndogo..!?

Majibu yapo hapa hapa, aliyebandika hili bandiko ana Akili ndogo sana.
 
Back
Top Bottom