Kwa ujumla nchi hii ina umaskini mkubwa sana. Kuna maeneo ukienda, unajiuliza maswali mengi bila kupata majibu.
Waafrika wengi wanaishi katika umaskini mkubwa wakiwa wameridhika kwa sababu hawana exposure, hivyo wanafikiri watu wote Duniani wanaishi kwa namna hiyohiyo au inayokaribiana na hiyo.
Kuna wakati, nakumbuka tulikofi ndege kwaajili ya kufanya airborne survey, tulipotua kijiji kimoja, wale wazungu ambao ilikuwa mara yao ya kwanza kuja Afrika, walisema kuwa japo hawakuwepo wakati wa karne ya 18, lakini kwa kupitia maandiko ya kihistoria, ni dhahiri maisha ya barani kwao wakati wa karne ya 18 yalikuwa bora maradufu kuliko yale waliyokuwa wanayashudia kwenye vijiji vingi vya Tanzania.
Kuna baadi ya mikoa, vijijini ni balaa kubwa. Mpaka leo watu wanaishi kwenye tembe, nyumba za tope au mabanda ya miti na nyasi. Niliwahi kwenda hifadhi ya Kigosi, huko Ushirombo, nilichokiona kwenye vijiji vya njiani ilikuwa ngumu kuamini. Watu wanaishi kwenye mashimo. Banda linakuwa halina ukuta, paa linasimama juu ya ardhi. Katikati ya hilo paa la nyasi na miti wanachimba shimo. Hilo shimo ndiyo nyumba..