Godbless Lema ni mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa chama hicho kanda ya Kaskazini.
Lema alikuwa ni miongoni mwa wanachama waliompigia chapuo
Tundu Lissu wakati wa uchaguzi mkuu ndani ya chama hicho uliofanyika Januari 2025, ambaye vilevile amekuwa akitaka kusimamiwa kwa haki kuhusu kesi ya uhaini na kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii wa X inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu inayotarajiwa
kuendelea Juni 16, 2025.
Video ya Lema inayosambaa mtandaoni
Katika mtandao wa Facebook ilichapishwa
video inayomuonesha Lema akisema Heche na Lissu ni waropokaji, na wamtaka Lissu apumzike kwa sababu amechoka.
Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search na marejeo ya video, umejiridhisha kuwa kipande hicho cha video ya Lema kimepotoshwa kwa kukata vpinde na kuviunganisha isivyostahili, jambo lililosababisha kupotosha ujumbe halisi wa Lema.
Video iliyochapishwa na
Mwanzo TV Plus inarejea Video ya matangazo mbashara yaliyorushwa na
Jambo TV tarehe 19 Januari 2025 ambapo wenyeviti na makatibu wa mikoa wa CHADEMA waliokuwa wanamuunga mkono Tundu Lissu wakati wa uchaguzi wa chama hicho, wakizungumza na waandishi wa habari, ambapo pia Lema alipata nafasi ya kuzungumza na ndipo kipande hicho kilichopotoshwa kimetolewa.
Katika hotuba yake Lema alikuwa akimnadi Lissu alipokuwa mgombea nafasi ya uenyekiti dhidi ya Mbowe akiweka bayana kuwa
hawamchukii Mbowe, bali wanampenda ndiyo maana walihitaji apumzike, hivyo aliwataka wajumbe wamsaidie kwa kumnyima kura wakati wa uchaguzi mkuu wa chama hicho wa Januari 2025.
"Hatumchukii Mbowe, tunampenda ndiyo maana tunataka apumzike. Mtu akichoka ukiona amechoka unamsaidia kumshauri apumzike."
Pia alionesha kukerwa na kujenga utamaduni wa kuona ubaya kuwa jambo la kawaida na kuwashangaa wale wanaotishika kuhusu Heche na Lissu kusimamia ukweli, huku akiwataka viongozi wa chama hicho kujitofautisha na Chama cha mapinduzi (CCM).
"Uimara wetu unatokana na tabia na value zetu tulizonazo, kama hatuna tofauti na tabia zetu na Chama cha Mapinduzi, tofauti yetu na chama cha mapinduzi inakuwa ni rangi za nguo. Na neno la Mungu linasema mtu mwema akikaa kimya uovu unafanya nini? (anajibiwa 'unatawala') Sasa na wewe ukiingia kwenye mapambano unajikuta na wewe unajifunza tabia mbaya, Hatari yake ni nini, tunajenga utamaduni wa kuona ubaya ni jambo la kawaida.
Ilifika mahali nimesikia mtu akisema 'Tatizo la Lissu na Heche, hawana shida nyingine, tatizo lao kubwa ni wakweli sana' kuwa mkweli siku hizi ni tatizo? Yaani mtu anasema hawa hawana shida, tatizo lao kubwa ni wakweli sana. Sasa ukishaharibu culture ya watu wanaona uovu ni kitu cha kawaida, hata nyie mkishika madaraka hamtabadilisha nchi hii"
View: https://www.youtube.com/live/ayxulwI31K4?t=740s