Lema: DW wametumiwa na CCM kufanya propaganda

Lema: DW wametumiwa na CCM kufanya propaganda

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200
"...DW wametumika kufanya propaganda kwa kuchelewesha kwa makusudi kurusha hewani kipindi cha mahojiano ya mwandishi wao na Rais Samia na ajabu baada ya kikao cha Tundu na Rais Samia ambacho kilikuwa cha siri na eti wao pia wakaachia ile video clip."

"...alianza Kikeke kutumika na sasa DW nao wamekuwa sehemu ya."

"...tukifanya mchezo CCM watamvalisha nguo za orange Mbowe.Hawa watu wamedhamiria kumfunga!"

"...Watanzania wengi mliopo huku ng'ambo mmejaa unafiki kwa sababu mmeshindwa kuandamana kuidai haki inayoporwa na CCM na ajabu tunazidiwa na Warundi na Waganda."

Amesema Lema.
 
Kwanza tujue hicho kipindi kilirekodiwa lini na kikarushwa lini? kwa wale wenye uelewa wa hayo mambo hiyo kazi huchukua siku ngapi?

Inawezekana madai ya Lema yakawa sahihi au yasiwe sahihi, japo kimsingi kwa ujumla wake haipingiki kwamba serikali ya Samia imedhamiria kwa makusudi kumfunga Mbowe kama asipoomba msamaha.
 
"...DW wametumika kufanya propaganda kwa kuchelewesha kwa makusudi kurusha hewani kipindi cha mahojiano ya mwandishi wao na Rais Samia na ajabu baada ya kikao cha Tundu na Rais Samia ambacho kilikuwa cha siri na eti wao pia wakaachia ile video clip."

"...alianza Kikeke kutumika na sasa DW nao wamekuwa sehemu ya."

"...tukifanya mchezo CCM watamvalisha nguo za orange Mbowe.Hawa watu wamedhamiria kumfunga!"

"...Watanzania wengi mliopo huku ng'ambo mmejaa unafiki kwa sababu mmeshindwa kuandamana kuidai haki inayoporwa na CCM na ajabu tunazidiwa na Warundi na Waganda."

Amesema Lema.
Kwani si tulikubaliana kuwa Mbowe ni Mandela wa Tanzania, akifungwa atakuwa amekipaisha sana chama na hatimae kuja kuwa Rais kama Mandela halisi au yule Mandela wa Zambia?
Kaka Godbless hofu ya nini tena?
 
Huyu Lema naye analialia mno sasa, Hakuna redio ya kimataifa inayorusha habari za upinzani na mijadala yao kama DW...

Halafu anavyosema watanzania wote walioko Ulaya ni Wanafiki kisa hawajaandamana ana uhakika gani kama wote ni Chadema.

Binafsi naona yeye ndio mnafiki zaidi maana amekimbia yeye na familia yake halafu anasakizia wenzake kuandamana.

Kama mpinzani wa kweli arudi nchini sio kupiga kelele tu akiwa nchi za watu.

Hizi ni dalili za kuchanganyikiwa na kukata tamaa...
 
Je kuna ukweli wowote kuhusiana na hilo alilosema Lema?

Je wewe kwa upande wako, tafakari yako na mtazamo wako ni upi? Tushirikishe ili tujadiliane.

Ahsante
...huenda.

Lakini ukimsikiliza kwa makini bwana Lema unaohisi kabisa yeye na Viongozi wenzake ndani ya chama wamekata tamaa na pengine wameshazidiwa na Samia kimkakati.

Ikumbukwe lengo kuu la Chadema lilikuwa ni kumdhoofisha Samia ili asiweze kutawala ki-utulivu ndani ya kipindi chake chote cha uongozi ili iwawie rahisi wana Ufipa kuendelea kujiimarisha kisiasa na kukikuza Chadema zaidi ya hapo kilipo.

Sasa Rais Samia aligundua mapema mno janja ile na kama tufahamivyo ukitaka kumuua nyoka gonga kichwa chake na hapo ndipo ilionekana nyoka ni Mbowe-akagongwa!
 
Hawa jamaa kiboko yao alikuwa Magu

Jamaa alijifanya mjanja baada ya uchaguzi wa 2020 akarudi Ubeberuni…alipofika German wazalendo wakachukua hati yake ya kusafiria na kuirudisha 'zizini' baada ya hapo akajikuta yupo Mahabusu ughaibuni

Sasa hivi wanamzulia uongo JK wakati ni wao waliposhauriwa wafanye kama walivyofanya Masheikh wa Uamsho ili jambo lao limalizwe kwa usalama wakakataa
 
[emoji871]#Lema anapaswa kujua kwamba wao ndio walikosa busara ya Subira.

[emoji871]DW-Swahili pia wanao utaratibu wao wa kuratibu vipindi,yeye Lema asiwapangie.

[emoji871]Lissu hakutumia busara maana ndani ya masaa 48 tangia alipotoka kuongea na Rais Samia.

[emoji871]Yeye alimaliza media zote akitafuta umaarufu,kwa kutangaza walichokiongea na Mh Rais Samia.

[emoji871]Pia...pamoja na Samia kuhojiwa na DW-Swahili,bado hakuongelea chochote kuhusu opinion yake.

[emoji871]Ni Lissu aliyepyuka siri zote walizoongea ili apate Credit kwa mataifa yanayomfadhili.

[emoji871]Lissu aliyageuza maombi yake kuwa kama maelekezo au amri kwa Rais Samia.

[emoji871]Alishindwa nini kusubiri Mh Raisi arejee nyumbani na kutulia kwanza ili aone atachukua hatua gani?

[emoji871]#Lema nae aelewe sio kila mtanzania aliyeko Ulaya au Marekani amefuata au anataka siasa.

[emoji871]Diaspora wengi wa Tanzania walioko huko wamekwenda kwa juhudi zao binafsi na wanao utashi wa kuamua nini kinawafaa au hakiwafai.

[emoji871]Wako huko kutafuta maisha na kuzisaidia familia zao.Hawakwenda huko kama wanaharakati.
Kama ilivyo kwa lema na Lissu.

[emoji871]Wengine huenda wanaweza hata kupoteza ajira zao endapo wataonekana kufanya siasa.

[emoji871]#Lema aelewe kwamba sio kila Diaspora wa Tanzania[emoji1241] aliyeko European Union[emoji1099] na America [emoji631] .

[emoji871]Kwamba wote wanaichukia CCM.
Aelewe siasa kila mtu anao mtazamo wake hivyo asiwalazimishe u-Chadema.

[emoji871]Tunaandika humu kuhusu Chadema kutotumia Busara katika baadhi ya maamuzi.ila huwa tunaambulia matusi tu.Ila ukweli unawaumbua.
 
Ukiona chama tawala kinathubutu kumtuma Meya wake akakiwakilishe katika sherehe za mashoga, basi ujue kuna tatizo kubwa sana la kimaadili ndani yake.
 
"...DW wametumika kufanya propaganda kwa kuchelewesha kwa makusudi kurusha hewani kipindi cha mahojiano ya mwandishi wao na Rais Samia na ajabu baada ya kikao cha Tundu na Rais Samia ambacho kilikuwa cha siri na eti wao pia wakaachia ile video clip."

"...alianza Kikeke kutumika na sasa DW nao wamekuwa sehemu ya."

"...tukifanya mchezo CCM watamvalisha nguo za orange Mbowe.Hawa watu wamedhamiria kumfunga!"

"...Watanzania wengi mliopo huku ng'ambo mmejaa unafiki kwa sababu mmeshindwa kuandamana kuidai haki inayoporwa na CCM na ajabu tunazidiwa na Warundi na Waganda."

Amesema Lema.
Yule hurulaini aliyetekwa na kuteswa Unguja si alikuwa mwandishi wa DW? Unasema vipi DW wanatumiwa na CCM?
 
Back
Top Bottom