Najua inajikosha tu na huna hata chembe ya huruma na wananchi ndio maana kwa mbowe unabwabwaja lakini zilitengwa bil. 700 za kununua magari unsfyata mkia maana unaogopa kutekwa na kupotezwa kwa sababu ya kusema ukweli .
Hakuna mtu anayekataa viongozi wa juu kupewa zawadi na wananchi wao .
Pesa zinazotoka mifukoni mwa wanachama ni kama sadaka zinazotolewa tu. Kwa hadhi na heshima ya Mbowe kama kiongozi wa juu wa chama anapaswa kupewa heshima kubwa .
Tofauti na kukaa bungeni kisha kutenga bil 700 za kununulia magari ya kifahari kwa watendaji wa wizara tu .Huo ni uhuni wa kijinga . Bil. na 700 zinatosha kujenga barabara ya mpya kutoka Dar es salaam mpaka Arusha na kupunguza ajali zinazotokana na uchakavu na ufinyu wa barabara hiyo iliyojaa mashimo.
Siku zote hakina mtu aliyewahi kupinga magari kwa viongozi wa juu wa umma .
Magari ya kifahari kwa :
Mh.Rais
Makamu wa Rais .
Waziri Mkuu.
Naibu waziri mkuu
Spika wa Bunge,
Jaji Mkuu
Karibu kiongozi
CDF
IGP
DGP
Manadhimu mkuu wa majeshi .
n.k.
Watu wasiozidi 50 tu hao ndio wanaostahili kununuliwa na kupewa yenye hadi ya juu zaidi.
Lakini huu ufisadi wa kupeana magari kama mchongo tu wa kuagiza magari kwa sababu ya 10% ni uhuni na hasara kubwa na yanapata ajali sana kutokana na miundombinu mibovu isiyoendana na hali ya magari hayo na speed yake kubwa 260KPH .
Mbowe amekaa madarakani kwa miaka 20 leo ndio anapewa gari kwa michango ya watu ubayo upo wapi kama sio uchawi wa machawa wa CCM . Bunge kila mwaka wanaletewa bajeti ya magari ya kifahari ya serikali wakati shule zote za serikali hazina hata Lory la kubeba mahindi .
Tena huo ndio mfano wa kuigwa . Hata Nyerere aliyekaa madarakani kwa miaka 25 hakujillimbikizia mali wala kujenga majumba huko nje wala kula mkoa kama walimfuata lakini zlijengewa nyumba moja tu wakati wa kustaafu kwa heshima ya uzalendo wake waliokaa miaka 10 na wengine huko Oman miaka 4 lakini ni matrilionea .
Ni mfano wa kuigwa tofauti na wale mafisadi waliostaafu wakiwa matrilionea lakini bado zinatolewa kodi za wananchi wanajengewa majumba ya ziada ya kifahari na magari ya kifahari na mishahara 75 % ya anayekua madarakani . Huu ndio ubadhirifu wa fedha za umma. Hospitali hazina pamba na nyembe kwa akina mama kujifungulia .
Michango ni hiyari na sio bajeti ya Chama chao . Lema ni mtu safi mwenye nia na dhamira safi kabisa sio wale mafisadi wanaopitisha bajeti ya kulipa mpaka wenza wa wakubwa ili hali nchi haina uwezo hata wa kutunza vyombo vyake vya ulinzi mpaka wakafie huko Kongo wakipigania uporaji wa madini wa Mabeberu ndipo waboreshe maisha yao nao waishi vizuri. Ufisadi wa fedha za umma tutaupinga bila kupepesa macho maana serikali inashindwa hata kulipa stahiki kwa watumishi wake ambao hawafiki hata 4% ya watu wote kwenye rasilimali nyingi.
Siku Afrika itakaposhtukia mchezo wa Marekani ndio utakua mwisho wa watawala mafisadi maana vita vya Kongo vinavyogharamikiwa na Mabepari kwa ajili ya kulba dhahabu huku wakiwa wanalipa majeshi ya UN kama walinzi wao ,vita hivyo siku vikiisha nchi zote zitarejesha wanajeshi wake na watakua na maisha magumu ndipo watakapoanzisha vuguvugu la kuwatoa majizi madarakani na kupiga mnada mali zao zote na kununua gloves hospitaliini.
ya Kauli ya Lema kuwa wamnunulie Mbowe gari kama zawadi kumuaga ni kauli ya hovyo na mawazo haya ni ya kipuuzi sana kuwahi kusikika duniani.. Yaani ikifikia kumnunulia gari Mbowe basi ghafla hamuwezi kubadilisha hela za kununua gari kuwa zinatosha kujenga madarasa au vipi?
Watanzania mnatakiwa kujua kuwa watu hawa ni wajinga na hakuna siku wamewahi kuwapigania watanzania na hakunaiku wamewahi kuwa na nia ya dhati ya kuwaondoa kwenye shida zenu na umasikini ndiyo maana wakishika nafasi za uongozi wanachowaza ni kujilimbikizia mahela na si vinginevyo.
Soma Pia: Lema: Tumuage M/kiti Mstaafu Mbowe kwa heshima, tumtafutie gari
Halafu huyu ndiyo alikuwa mbunge wa Arusha! Sina uhakika kama ni watu wa Arusha hawana maarifa au huyu ndiyo hana maarifa mpaka akaonekana ndiye anafaa kuwa mbunge waoewr