Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema, amesema anapanga kuweka hadharani majina ya vigogo wanaodaiwa kuwa nyuma ya pazia la sakata la G-55, akibainisha kuwa baadhi yao wamekuwa wakinufaika kifedha kupitia mradi huo huku wengine wakitumika kama “bidhaa” bila kujua.
"Hii project ina pesa nyingi, wachache wanaoingoza kwa nyuma ni wanufaika wazuri sana pamoja na watu wao walioko upande wa pili," alisema Lema na kuongeza kuwa baadhi ya wanaojitokeza hadharani kuunga mkono G-55 hawajui kama wanageuzwa kuwa bidhaa.
"Wakijua, watakuja kukiri na kuomba msamaha kwa machozi ya damu. Nitanyoosha rula, yaliyofanyika darini yatawekwa hadharani,"alisema kwa msisitizo.
Soma:
Ukimya wa Mbowe; Je, yupo nyuma ya G55? Kwanini haungi mkono harakati za Lissu na Chadema hivi sasa?
Andiko la Lema kupitia X linakuja wakati mjadala kuhusu kundi la wabunge 55 wa CHADEMA linaloelezwa kuibuka na msimamo tofauti ndani ya chama ukiendelea kushika kasi.
View attachment 3295516