PreGE2025 Lema kuanika hadharani majina ya vigogo waliopo nyuma ya pazia sakata la G-55

PreGE2025 Lema kuanika hadharani majina ya vigogo waliopo nyuma ya pazia sakata la G-55

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Lema hajawahi kuwa na akili nzuri.Lissu kupitia ushauri wa mjinga Lema atakwenda kuizika CDM soon.

Lema ana hulka ya kukosa busara, mihemuko, kuropoka na kutukana hovyo. Lakini ndiye mshauri mkuu na msemaji mkuu wa chama kwa sasa.

Naibu katibu bara naona ametulia zaidi. Lema aachiwe kuongoza tonetone lakini sio kuwa msemaji mkuu anavikiruga zaidi chama, hana utulivu.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema, amesema anapanga kuweka hadharani majina ya vigogo wanaodaiwa kuwa nyuma ya pazia la sakata la G-55, akibainisha kuwa baadhi yao wamekuwa wakinufaika kifedha kupitia mradi huo huku wengine wakitumika kama “bidhaa” bila kujua.

"Hii project ina pesa nyingi, wachache wanaoingoza kwa nyuma ni wanufaika wazuri sana pamoja na watu wao walioko upande wa pili," alisema Lema na kuongeza kuwa baadhi ya wanaojitokeza hadharani kuunga mkono G-55 hawajui kama wanageuzwa kuwa bidhaa.

"Wakijua, watakuja kukiri na kuomba msamaha kwa machozi ya damu. Nitanyoosha rula, yaliyofanyika darini yatawekwa hadharani,"alisema kwa msisitizo.

Soma: Ukimya wa Mbowe; Je, yupo nyuma ya G55? Kwanini haungi mkono harakati za Lissu na Chadema hivi sasa?

Andiko la Lema kupitia X linakuja wakati mjadala kuhusu kundi la wabunge 55 wa CHADEMA linaloelezwa kuibuka na msimamo tofauti ndani ya chama ukiendelea kushika kasi.

View attachment 3295516
Tunasubiri
 
Lemma atueleze, hela ya tone tone imeenda wapi, na kwa nini amemfukuza ofisini muhasibu wa chama na kumnyanganya majukumu yake
 
Huyu jamaa ana tofauti gani na Makonda? Badala ya kujibu hoja zao yeye anajikita kwenye uchafuzi. Yaani watu kama Mrema, Ruge, Suzan hawawezi kujiamulia kitu mpaka watumwe?!!! Ovyo sana.

Amandla....
Aliyewatuma anajulijana na atafeli tu
 
LAKINI ALISEMA FOR SURE KUWA NIKISHINDWA NAKWENDA KUFANYA BIASHARA ZANGU KUTAFUTA MAPEKECHEE................... You have a point, though........DEFINITELY HATUKUTEGEMEA AWE KIMYA NAMNA HII
'Movement' kama hizi za kina G55 ndani ya Chadema, Mbowe alikuwa hodari mno wa kuzidhibiti bila kuvuruga chama, ila kwa Lissu sijui itakuaje..

JokaKuu zitto junior
 
Lema hajawahi kuwa na akili nzuri.Lissu kupitia ushauri wa mjinga Lema atakwenda kuizika CDM soon.
Ni faida kwako na ccm. Kila siku chadema imekufa na itakufa ila bado mnatumia policcm kuwadhibiti wasifanye shughuli zao maiti anawezakufanya kitu gani?
 
'Movement' kama hizi za kina G55 ndani ya Chadema, Mbowe alikuwa hodari mno wa kuzidhibiti bila kuvuruga chama, ila kwa Lissu sijui itakuaje..

JokaKuu zitto junior
Lissu hana budi kujifunza kuwa “Transparency does not mean nakedness”
.Kama kiongozi sio kila kitu ni for public consumption! Kuna mambo mengine ni kwa wachache wanao stahiri.
Hata huko kwenye vikao vyemu vya juu inabidi mfanye tathmini ya kina kwa wajumbe wenu and handle them accordingly!!
 
Lema hajawahi kuwa na akili nzuri.Lissu kupitia ushauri wa mjinga Lema atakwenda kuizika CDM soon.

Lema asipokuwa na akili nzuri, wewe ambaye hujawahi kuleta hoja yoyote ya maana hata hapa JF, si utaitwa mwendawazimu kabisa?

Mrema ametamka kuwa nyuma tao wao, wapo waliokuwa viongozi, lakini hakuwataja majina, Lema akiwataja majina, kuna tatizo gani?
 
Back
Top Bottom