Kuna watu wawili nawaona wamekwazana baada ya mmoja kumkumbushia mwenzake kwamba we masikini upo! Eti kwa sababu tu alikuta mjadala kama huo wakuitana masikini.
Kumbe sababu ilikuwa kama hii..
hapakua na haja ya ugomvi kuhusu tu umaskaini bana..
binadamu tuna umaskini wa hali na namna mbalimbali, na kwahivyo naweza sema umaskini ni sehemu ya maisha ya mwanadamu.....
kuna umaskini wa roho, hali, fedha na mali, umaskini wa fikara, makazi, mavazi malazi, njaa, kiu n.k
hujawahi kuskia kwamba kuna matajiri wa mali na fedha, lakini ni maskini wa kutupwa wa kukosa amani, hawapati usingizi na hawapendi wala kupendeka kwa jamii, hawawezi kuishi na mke au mume kwenye nyumba moja tena ya ghorofa na maru maru kwa upendo na amani...
lakini maskini wa fedha na mali hadi kwenye dalaladala ana uchapa usngizi mwanana kwa amani na utulivu, anapendwa na anaipenda jamii inayomzunguka, ame oa au kuolewa na wanaishi kwa amani na upendo kwenye nyumba yao ya udongo na matope.....
umaskini si kitu kizuri,
ila kwa utashi, akili, nguvu na maarifa tuliojaaliwa na Mungu, tunaweza kujikwamua katika hali, hiyo tukiamua kujizatiti moja moja, na kisha baadae kwa umoja
