Lema, kwenye press yako tunategemea utakuja na majibu ya tuhuma hizi

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
Unatuhumiwa kuikutanisha familia ya Lissu na viongozi wa serikali kwenye hoteli ya Sea Cliff ili familia imuombee msamaha Lissu kwa Samia, je tuhuma hizi ni za kweli?

Kwanini unalazimisha Maridhiano, ina maana unapinga maamuzi ya Baraza Kuu na Kamati kuu?

Hukuhudhuria kwenye msiba wa dereva wa Heche wala hukutoa pole, je tuhuma hizi ni za kweli?

Ulitoa tuhuma kuwa Heche huwa anafanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, DGIS. Je ni Kweli?

Kwanini kila hukumu ya Mkiti Lissu inapokaribia kusomwa huwa anaita press za utata. Lengo lako hasa huwa ni nini.

Ulisema Katiba mpya haisaidii kitu, kwanini unapingana na maamuzi ya chama chako na msimamo wa Mkiti wako?

Kwenye kikao cha Kamati Kuu Kigoma ulitaka Heche apishe kikao ili wajadili pesa za Tone Tone. Je ni kweli na ulikuwa na sababu gani.

Uliandika mtandaoni kuwa endapo maazimio ya Kamati Kuu yataenda kinyume (nafikiri kuhusu tone tone) utalazimika kujitetea mwenyewe. Huiamini Kamati Kuu? Na kwanini utumie press badala ya vikao halali vya chama.

Unatuhumiwa kumshawishi John Pambalu arudi nchini mambo yote umeyaweka sawa, je ni kweli?

Na mwisho, kuna tuhuma kuwa unataka Heche apishe kiti ili Mbowe arudi akiingize chama kwenye maridhiano, je tuhuma hizi ni za kweli?

Tunategemea kwenye press yako ya leo utakuja na majibu ya kuridhisha au uache ziendelee kuwa tuhuma ili Umma uje na majibu yake.
 
Mbona tuhuma zote zina dhamira nzuri tatizo nini hapo
 
CCM mnaangaika sana. Mlizoea kufanya uhuni wa kuwanunua wanachama wa CHADEMA wenye njaa. Sasa mtawanunua waliobaki wenye njaa lakini hamtafanikiwa dhamira yenu ovu
Kuna mwingine anaitwa Odero Odero kila siku anafanya press ya maridhiano.
 
Ushauri kwa CCM mbowe alishapoteza mvuto kwa kutoshikamana na mwenzie mahakamani asitumiwe hana impact
 
Kuna mwingine anaitwa Odero Odero kila siku anafanya press ya maridhiano.
Yap. Hilo jamaa unaona kabisa limeongwa. CHADEMA isione aibu kuwachukulia hatua kali sana. waTanzania lazima waelewe tuko kwenye vita ya kumuondoa mkoloni. CCM ni typical mkoloni. Sielewi kabisa eti mtu anataka maridhiano na mkoloni!!! Huo ni usaliti mkubwa sana
 
Tuhuma ya kuwauza wenzake wa Nairobi?
 
Niliishawahi kuwashauri Chadema; FUKUZA kila mtu ndani ya Chadema chama kibaki peke yake bila mtu. Hii ndio dawa ya kutokuwa na mamluki ndani ya Chadema!!
 
Umemaliza kazi. Asante.
 
Niliishawahi kuwashauri Chadema; FUKUZA kila mtu ndani ya Chadema chama kibaki peke yake bila mtu. Hii ndio dawa ya kutokuwa na mamluki ndani ya Chadema!!
Muda ukifika atajiondoa mwenyewe kama alivyojiondoa Zitto, lkn hatapotezwa kama Polepole na Nchimbi .
 
"Usiweke maagano na masikini maana masikini anabadilika" - Maboya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…