Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Lema fanya yako..Jimboni hakuna maji ya uhakika wala umeme!Miundo mbinu ya shida na vijana wengi hawana ajira!Ila kila siku una deal unarukia yasiyokuhusu..Fanya yako na shughulikia kero za wananchi wako!Period

weee hebu koma, Arusha sio Koromije, Arusha tuna kila kitu cha maana kasoro rais tu.
 
Mh Rais wakati wa Msiba wa Christina Lissu dada yake na Mh Tundu Lissu nilikuona katika msiba ule wewe na Mama yetu Mke wako , je Mh Rais na wewe ulikuwa unasaliti Chama chako ?

😀😀😀😀
I wish kuld be a Jaji but before that i kuld see physician answers regarding the question above!!!

Nipo South najifunza jinsi ya kukitangaza Kijiji cha Bashite kwa kimombi ie Call Me J or Korem-jee as in Karimjee!!
 
Hata kama wakikumata, watakamata mwili na sio mawazo na fikra zako, fikra na ukweli vitabaki daima hata pale utakaporejea kwa muumba wako
Hawawezi Kumkamata kwa sababu hajaropoka
 
Duh,

Ni lini Mheshimiwa umeanza kufahamu kuwa vyama vya siasa sio uadui?

Hongera kama umefahamu kimatendo maana ya upendo.

Kumbuka pia kumpenda mtu sio one way traffic!

Yaani kutaka wewe tu upendwe lakini wewe kuwapenda wengine iwe ni option.

Hata kumuombea mtu mabaya sio upendo achilia mbali kutaka watu wasisalimiane au kususa futari yao. Unapomwambia Mkuu wa Mkoa ni shoga huo sio upendo bali ni kueneza chuki.

Mbona hatukuona huo upendo au ushauri kwenye hii habari iliyobeba matendo yako na UKAWA?

LINK==> CCM wazungumzia uamuzi wa wabunge wa UKAWA kutowasalimia

LINK==> Saed Kubenea ataka wabunge wa UKAWA wenye wapenzi wao CCM wawasuse

LINK==> Wabunge wa UKAWA wasusa futari ya Waziri Mkuu

Ama kweli mkuki kwa Nguruwe ni mtamu...

Don't worry, this is karma at its best!

It's very easy to act as victim wakati wewe ndiye aggressor.

Inanikumbusha kwenye football ambapo mchezaji anamtemea mate mchezaji mwingine ambapo yule aliyetemewa mate anapatwa na hasira na kurusha kofi au ngumi. Referee ataona mwenye makosa ni yule aliyerusha kofi au ngumi na hapohapo atampatia kadi nyekundu.
 
Huwezi ukamtukana, kumvunjia Heshima, Au kumdharau Rais,Mwenyekiti wa chama cha hao wabunge, Halafu
hao wabunge waje kukupongeza au kukusalimia kwa mbwembwe!!
Hii inaonyesha na wao wapo kundi moja la kumdharau Rais na Mwenyekiti wao wa chama.

Yote na yote Pongezi kwa kujua huyu ni Mh Rais
safi sana
naona sasa umeanza kujitambua.
Lema Magufuli ndiye Rais wa Tanzania kwa sasa
umpende usimpende ndiye Rais wako,
Jaribu kuwa Na Heshima kwa Mamlaka
 
So sad...inauma inauma ...inauma sana kuona wenyewe tunaifukuza amani tuliyonayo kwa manufaa ya kibinafsi...Viongozi wa dini wapo wapi Ama mnataka amani ipotee ndo muanzishe mifungo makanisani..Mungu atatuuliza siku moja tusipopaza sauti kukataa uonevu wa waziwazi ambao unaweza kuwa Chanzo kikubwa cha kupoteza Amani yetu..
 
Sidhani kama ana Muda wa ziada kufanya mambo ya Kijinga kama hayo Urais ni kazi ngumu sana.
Ila ana muda wa kuangalia clouds TV daily na kupiga simu mara kwa mara na bila kusahau wale wasela wa kipindi cha shilawadu?! Halafu anatuomba tupige magoti tumwombee wakati wao wanahubiri chuki na uzandiki?!
 
Kauli za huyu Rais wetu awamu hii,ni za hatari mno,sio za kufumbia vinywa hata kidogo.

Ama kweli "mchuma janga hula na wa kwao"...
Naanza kuamini wale waliosema huko nyuma huyu mkulu hayuko njema upstairs.

Lawama zote zimwendee Kikwete
 
Tulipofika chadema atamzikia ccm. Na ccm atamzikia chadema. Je?hii ndo,nchi tuliyopewa na mungu tuitawale kwa chuki? Nawaomba viongozi wetu, ongozeni taifa kwa kutanguliza utu, siyo itikadi.sisi, ni jamii moja, wa taifa moja.na babayetu ni tanzania.kama kifo kisivyobagua,tusibaguane kwa chuki ya kidunia. Muogopeni mungu.
 
Huku Mhe. Rais anapotupeleka tulishatoka huko enzi za ukoloni za divide and rule.


Hata wabunge wa CCM wana uhuru wa kuamua kumtembelea mgonjwa, au aliyeko mahabusu ambaye sio wa chama chao, kama hawavunji katiba ya nchi wala chama chao. Isifike wakati mkashindwa hata kuzikana kisa tofauti za kiitikadi.
Waliotangulia hawakutufundisha hivyo.

Mungu yuko nawe Mhe. Godbless J Lema .
 
Na upinzani munawajibu wa kuhubiri haya uliyoyasema kwa wanachama wa wapenzi wenu, Chadema mna wanachama na wapenzi wenye chuki kwa serikali na dola kwaujumla. Kila mmoja anamuhitaji wenzake kwa njia moja au nyingine.
Hujajiuliza chuki inatoka wapi? Inatoka kwenye miongozo kama hii.

Kule Pemba hali baada ya uchaguzi ilifanana hivi kwa mujibu wa ripoti, zikapigwa kelele kuwa ule sio ubinadamu. Ikafika hatua kuna bwana mkubwa mmoja aligoma kupokea mkono wa salamu wa bwana mkubwa mwingine, hapo napo kukawa na kelele. Leo bwana mkubwa anawafundisha mabwana wakubwa wasijuliane hali wala kupeana pole, ilhali bwana mkubwa kwenye kesi ya mabwana mkubwa wa visiwani alisema ule sio uungwana...sisi tudogo tudogo tunafundishwa nini hapa?
 
Ujumbe Muhimu sana. Ni na uhakika watu wake wameuso na kumfikishikia. Binafsi niliogopa sana niliposikia hii kauli kutoka kwa Mh. Rais wa Jamhuri.

Kwetu sisi Roman Catholic,kuwatembelea wafungwa/mahabusu kunaongeza rehema na baraka zaidi. Hapo naona Rais anataka kuwafundisha watu matendo gani ya huruma wafaanye. Mbinguni kila mtu ataenda peke yake. Asitake kuwafanya watu watende dhambi ya chuki kwa maslahi yake binafsi.
Halafu hichi ni kipindi cha kwaresma na jamaa anajiita mroman. Jaman mapdri acheni unafiki mwambieni ukwel
 
Back
Top Bottom