Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Unaruhusiwa kumkosoa Rais kwa hoja na ustaarabu sio kwa kejeli na matusi
 
Unaruhusiwa kumkosoa Rais kwa hoja na ustaarabu sio kwa kejeli na matusi
Sasa Halima Mdee kamtukana Rais?

Kwani kusema matamko ya Rais yamegeuzwa sheria ni matusi?

Kwani hatujaona Rais kapiga marufuku vyama vya upinzani visifanye shughuli za kisiasa hadi mwaka 2020, na tumeona naDC,maRC na maRPC wakitekeleza agizo hilo kwa uaminifu mkubwa?
 
Mhaini kesi yake ni kifo au kifungo cha maisha Kuna mpinzani kapata adhabu kama hiyo?

Tufuate sheria,kanuni na taratibu tu hakuna shida
Rais wako kawaambia trafiki wakikuta mtu anaendesha gari kwenye lane ya mwendokasi wachukue gari, waipeleke polisi, watie matairi, wauze, kisha wakatae kwamba wameuza matairi.

Labda ungeanza naye kumwambia atoe masuluhisho yalito ndabi ya sheria

Yeye ni mkuu wa nchi na anachisema kina uzito sana.
 
Kama Kuna vyama vimekubalina na kauli hiyo basi hakuna vyama imara vya siasa
Kauli za Magufuli zinatakiwa kupingwa mahakamani.

Tatizo hatuna wanasheria wanaoweza kudiriki kufanya hili Tanzania.
 
Si kama.....wapinzani wengi wana tabia za kiaini kama sio wahaini.....
 
Kwa hiyo kwako wewe Mbunge mwenye heshima ya kuitwa Mheshimiwa ni Mbunge wako wa CCM 'chamatusi' Kibajaj?

Hivi wewe hujui hata lile sakata la kutimuliwa akina Halima Mdee na Esther Bulaya lilitokana na upendeleo wa wazi wa Spika Ndugai?

Kwani wewe hujui kuwa Mbunge Shonza aliwasha mic na kumuita Mnyika mwizi?

Sasa ni kwanini Mnyika alipoomba mwongozo ambapo ni kwa mujibu wa kanuni za Bunge kwa kumwomba Spika kuwa aliyewasha mic na kumuita yeye mwizi, aidha afute kauli yake au authibitishe wizi wake.

Sasa ni kwanini Spika Ndugai alifanya upendeleo wa wazi kwa mbunge mwenzake wa CCM aliyemwita Mnyika mwizi na badala yake akawaamuru Polisi wa Bunge wamtoe Mnyika kama kibaka?

Ni wazi CCM imelewa madaraka na inaamini kuwa itaitawala hii nchi milele.....

Hata hivyo lazima wajikumbushe, wako wapi KANU ya Kenya?

Wako wapi UNIP ya Zambia?

Wako wapi Malawi Congress?

Kitu ambacho CCM wanapaswa waelewe ni kuwa hakuna kitu chochote hapa dunia ni kilichokuwa na mwanzo ambacho hakitakuwa na mwisho....
 
Kwa akili zilizo fair kidogo utasema ni wapinzani tu wanaokosa nidhamu bungeniqf ukawaacha akina Shonza, Kibajaji, Msukuma etc ?!
 
Kwenye DS nilipokuwa UDSm niliulizwa: Opposition Parties in Tanzania are dying: Discuss.
 
Katika hii posti yangu uliyo quote nioneshe mahali nilipo andika maneno CCM au CHADEMA, tafadhali.


Na washawasha!


 
Kwa akili zilizo fair kidogo utasema ni wapinzani tu wanaokosa nidhamu bungeniqf ukawaacha akina Shonza, Kibajaji, Msukuma etc ?!
Tena hiyo list uliyoitaja, kama kweli Spika angekuwa fair, hao ndiyo wangefukuzwa bungeni, lakini badala yake akina Shonza na Kibajaj ambao ndiyo waliosababisha lile tukio la Mnyika kutolewa kama kibaka.......

Badala yake tukamshangaa Spika Ndugai anamsifu Kibajaj, eti wewe ni kiboko umesababisha hadi wabunge wote wa upinzani watoke bungeni?

Halafu Spika huyo huyo eti anawalaumu wabunge wa upinzani, eti ni kwanini walisusia futari ya Waziri Mkuu!

Hivi yeye Spika Ndugai haoni namna anavyofanya jambo la hatari la kuweka mgawanyiko kwenye Bunge letu la vyama vingi?

Mbona maspika wenzake akina Mama Ana Makinda na marehemu Samuel Sitta hawakuongoza Bunge kwa style hiyo?
 
Na ndiyo maana Halima Mdee amesema kuwa kauli ya Rais inageuzwa kuwa sheria na watendaji walio chini yake.

Cha kushangaza DC Ally Hapi akaamrisha Jeshi la Polisi limkamate, eti kamtukana Rais!
 
Only in Tanzania......

Eti Rais anawahimiza Polisi wake wajichiukuliie sheria mkononi!
 
Hivi unaweza kusema eti Halima na Esther walifungiwa kwa kutoa hoja nzito Bungeni,hebu tuletee hapa hizo hoja nzito walizotoa hadi kupelekea kufukuzwa Bungeni ni zipi kama siyo mizuka ya kusukumwa na bangi hatimaye kufanya matendo yasiyostahili. DC au RC atamuweka ndani yeyote yule atakayehatarisha amani ndani ya eneo lake bila kujali anatoka mrengo upi,na woote wanaohatarisha amani ni hao vichaa wanaojiita makamanda wasio na mafunzo ya kijeshi..!!!
 
Sasa sijui hivyo viwanda vitajengwa wakati gani, wakati kila siku serikali ya awamu hii priority no 1 kwao ni kudeal na wapinzani!
Kwani uliambiwa serikali inajenga viwanda au inaweka mazingira bora ya ujenzi wa viwanda?
 
We
Wewe usiye muoga chukua hatua,mbona unaishia humu JF na kelele nyiingii
 
Hebu tuwe wakweli hivi ni nani kati ya Halima Mdee na Esther Bulaya wa Chadema na Kibajaj na Msukuma wa CCM wanaoonekana hawa ndiyo wanaopata lile jani?
 
Hebu tuwe wakweli hivi ni nani kati ya Halima Mdee na Esther Bulaya wa Chadema na Kibajaj na Msukuma wa CCM wanaoonekana hawa ndiyo wanaopata lile jani?
Nimeomba hizo hoja nzito za Halima na Bulaya ziwekwe hapa tuzione
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…