Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Na ndiyo maana Halima Mdee amesema kuwa kauli ya Rais inageuzwa kuwa sheria na watendaji walio chini yake.

Cha kushangaza DC Ally Hapi akaamrisha Jeshi la Polisi limkamate, eti kamtukana Rais!
Rais anatakiwa kushukuru watu wanaomtukana wazi, kama kweli kamtukana.

Hilo katika somo la uongozi ni sehemu ya feedback kujua wasichokipenda unaowaongoza ni kipi.

Tanzania hatuwezi kuendelea mpaka tukubali kukosoana kwa lugha kali.

Siku moja kulikuwa na mgogoro mkubwa katika habari kuhusu masuala ya mazingira, mgogoro huu ulihusu kampuni yangu kwani ilihusika katika kutoa fedha zilizofanikisha mradi huu.

CEO wetu akaitisha an online forum kujibu majibu ya wafanyakazi.

Kuna wafanyakazi vijana walikuwa wanapaka mpaka nikaona noma mimi. Yaani kupaka anapaka mtu mwingine, lakini noma naona mimi kwa jinsi walivyokuwa wanapaka kisawasawa. Wengine wakawa kama Twitter activists mpaka na hashtags.

Sasa mimi nikafikiri watakaripiwa au kufukuzwa kazi. Kumbe naona wanaheshimiwa sana kwa kuleta mawazo tofauti katika kampuni!

Nikasema hii ni moja ya sababu wenzetu wanaendelea na sisi hatuendelei.

Mfano mwingine, miaka mingi iliyopita nilivyokuwa nasomea undergraduate, mwalimu wangu wa falsafa nilikuwa namchachafya sana darasani. Nilikuwa namuuliza maswali na kumpinga sana mapaka ikawa kama na dominate darasa. Nilikuwa nimesoma mambo mengi mwenyewe kabla ya darasa na darasani nilikuwa namchallenge sana mpaka wanafunzi wengine wakaniuliza "hivi wewe upinzani wako darasani huwa unaamini unayosema kweli au uzushi tu (mainly atheism). Nikawaambia ni kweli nasimamia hivyo.

Mwisho wa term profesa akanitumia e-mail, akasema nisije kwenye mtihani.

Nikaona hapa nishaharibu Profesa ananifelisha kwa technicality.

Nikamuuliza, kwa vipi nisije kwenye mtihani?

Akasema umeshafaulu kwa kazi yako ya darasani.

Nikauliza nimefaulu vipi? Akasema umepata A+. Yale mahojiano yako ya darasani ni mahojiano ya darasa la masters, si undergraduate. Huna haja ya kuja kwenye mtihani.

Huyu Profesa alikuwa ni conservative, jaji, mtunzi wa vitabu na mwalimu wa chuo kukuu. Mimi ni immigrant mbishi nambishia kila kitu darasani katika namna ambayo Profesa wa kibongo angeona namkosea heshima.

Lakini yeye alithamini sana uwezo wangu wa kujenga hoja. Mpaka akawa ananialika niende kwenye events zao kuongea na ku network na rafiki zake.

Hapo niligundua kwamba wenzetu wanaendelea kwa kuthamini mawazo tofauti.

Na sisi, bila kuthamini mawazo tofauti hatuwezi kuendelea.
 
Mkuu wa Kaya amekazana sana kupandikiza hisia za kwamba kuwa mpinzani Tanzania ni kuwa mhaini. Yaani kwake mtu akiwa Chadema/UKAWA anaonekana si mtanzania kabisa na si mzalendo kwa nchi yako.

Nawashangaa hata wanaoendelea kufanya utafiti kuhusu siasa. Unafanyaje utafiti wa kisiasa wakati shughuli za siasa zimepigwa marufuku?
 

Aya ya kwanza tu inaonyesha hujui historia ya nchi yetu.Chama kimoja hakikuanza 1961,uliza ujue ndipo uandike.Humu jukwaani kuna watu kila wanachosoma wanaamini kuwa ndicho.Tuandike tunachokijua.
 
You are very right.....

Kiongozi bora ni yule hachukii kukosolewa ili ajirekebishe pale alipokosea, kwa kuwa yeye as Human being hawezi kuwa 100%
 
You are very right.....

Kiongozi bora ni yule hachukii kukosolewa ili ajirekebishe pale alipokosea, kwa kuwa yeye as Human being hawezi kuwa 100%
Huyu wetu anasema hapangiwi na hakuchukua fomu na mtu.
 
Aya ya kwanza tu inaonyesha hujui historia ya nchi yetu.Chama kimoja hakikuanza 1961,uliza ujue ndipo uandike.Humu jukwaani kuna watu kila wanachosoma wanaamini kuwa ndicho.Tuandike tunachokijua.
Nimekwambia tulirejea kwenye mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Nafahamu pia kuwa nchi yetu ilikuwa kwenye mfumo wa vyama vingi kwa kipindi kifupi baada ya nchi yetu kupata Uhuru wake mwaka 1961.

Baadaye nchi ikaingia kwenye mfumo wa chama kimoja.

Na baadaye ndiyo tukarejea tena kwenye mfumo wa vyama vingi nwaka 1992.
 

Je ungependa kuwa na binti wa aina ya Halima Mdee kwa tabia.mwenendo na lugha? ana uwezo mkubwa wa akili na kujenga hoja.Ana tatizo kubwa la kuudhibiti ulimi wake.Waingereza wana msemo muhimu sana kwa Halima Mdee na watu wa aina yake,unasema"What matters is not what you say but how you say it".

Ukiwa timamu kimalezi unajua namna ya kusema na waliokuzidi umri na unapaswa kujua unasema wapi.Siyo kila mahali ni bungeni.
 
Hivi wakoloni wangemminya Nyerere kama wanavyominywa wenye mtazamo tofauti na watawala wa sasa tungepata uhuru? Tungekuwa na kumbukumbu zipi za Nyerere? nakumbuka Nyerer alikuwa na maneno makali kuliko ya Mdee au Lissu. Akiwahutubia wananchi aliwataja wakoloni kuwa ni makupe, mabeberu, mapepari, wanyonyaji wakubwa. Akasema mmetupuuza na kutunyonya vya kutosha sasa tunataka tuwe huru. Pamoja na kwamba wakoloni walikuwa na dola lakini walimpa Nyerere uhuru wa kuhutubia na kufanya siasa na matunda yake tulipata hotuba zake nyingi na vitabu vyake vingi kabisa. Leo watu wanaogopa hata kuandika vitabu vya riwaya, mashairi, n.k.

Nakumbuka enzi za Nyerere kulikuwa na riwaya, mashairi na vitabu vya kiuanaharakati vingi tu hadi kwenye utawala wa Mkapa. Lakini leo kila mtu yuko kimyaaaaaaaaa! Anakufa na maarifa yake kichwani kwa hofu ya utawala uliopo. Ngoja tuone mwisho wake.
 

Waambie baada ya uhuru vyama vingi viliondolewa lini? vimerejeshwa 1992 sawa baada ya kuwa chini ya Chama kimoja kwa muda gani?
 
Hiyu wetu anasema hapangiwi na hakuchukua fomu na mtu.
Kwanza yale maneno ya kusema kuwa hakuna mtu aliyenituma kwenda kuchukua fomu ya Urais kwa hiyo hakuna mtanzania yeyote anayepaswa kunielekeza la kufanya, ni maneno ya dharau kubwa kwa wapiga kura wake, kwa kuwa anajua siyo yeye mwenyewe aliyejipeleka Ikulu, Bali kwa kura za watanzania.

Sasa tusubiri 2020 kwa hizo tambo zake tuone kama kura yake moja na ya mama Jesca kama ndizo zitakazomrejesha Ikulu!
 
Tumemsikia DCwa Kinondoni akisema kuwa aliamuru Polisi wamkamate Halima Mdee kwa kuwa amemtukana Rais.

Sasa nikuulize wewe Halima Mdee kusema Rais anaichukulia kauli yake kuwa sheria, hapo tusi liko wapi?
 
Yule kwajinsi anavyompeleka Mama Jesca puta nina shaka hata kama kura ya Mama Jesca aliipata.

Wewe huoni hata kwenye kampeni tu Mama Jesca aligoma mpaka wazee wakamshawishi sana kwamba haileti picha nzuri Baba azunguke kwenye kampeni bila mama?

Na hivi kura ilivyo siri Mama wa watu anaweza kuwa kampigia Lowassa au hata Rungwe au kuharibu tu kura ilinafsi isimsute kwa kumpigia kura gubegube huyu anayemjua vizuri sana kwa vituko vyake vya mpaka ndani ya nyumba.
 
Aya ya kwanza tu inaonyesha hujui historia ya nchi yetu.Chama kimoja hakikuanza 1961,uliza ujue ndipo uandike.Humu jukwaani kuna watu kila wanachosoma wanaamini kuwa ndicho.Tuandike tunachokijua.

anaweza kuwa kakosea hapo vipi hayo mengine?
 

Msitafute matusi ya bure ili mseme unaona wanapendelea wa kumshtaki.Kuna mama niliyedhani anastahili heshima kubwa,wakati wa kampeni alikamatwa sehemu zinazostahili kuguswa na baba mwenye nyumba tu,tena chumbani.Sijasikia chochote kulaani kitendo hiki.JPM akisemwa hovyo mnaona sawa na mnamtaka avumilie kuna mtu akiguswa tu mnatamani maandamano yaruhusiwe.Poleni.
 
Unaposema "msitafute" unakikusudia kikundi gani?

Mimi sifungamani na namba yoyote, ni "singularity" kama kugawanya kwa ziro.

Huyo Mama nisiyemjua wala hata kumtaja unamhusishaje na mimi mpaka ukaniwekee habari zake kwenye nukuu ya bandiko langu?

Watu tunamsema ovyo Mungu, nini JPM huyo gubegube ambaye hata Kiswahili hajui?

Uhuru wa wananchi kuwasema vibaya viongozi ni sehemu muhimu ya jamii kuendelea.

Hakuna namna ya kulikwepa hili.
 
Reactions: PNC
usisome juu tu huu mjadala huru sio shule
.

Mjadala ni zaidi ya shule ya darasani.Ni mahali sahihi pa kujifunzia maisha halisi ya mtaani.Huku hakuna "copy and paste".Ukianzisha uzi hakiki kwa uhakika unachoandika,ukikosea sarufi si kosa kubwa japo utawapotosha wanaojifunza lugha lakini ukipotosha mada unawapoteza kabisa watoto wa kizazi cha "copy and paste".

Nilisoma makala nzima mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…