Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

I wish Magufuli angekua active member wa jf......

Mh. Rais ni active invisible member wa JF ingawaje hachangii maoni. Kumbuka siku aliwaapisha wakurugenzi tarehe 12 July 2016 alisema kwenye mitandao watu walisema huyo 'Luhende' alimchagua kuwa mkurugenzi hana cheti cha master. (Hii tuhuma ilitolewa hapa Jf hivyo JPM aliisoma) Sikiliza hapa:



Lakini toka swala la Daudi Bashite kughushi vyeti kujulikana. Mh Rais sasa anadai eti hasomi habari za mitandao🙂 Alitoa kauli hii hapa chini kwenye hotuba yake ya Mtwara 5th March 2017

"Hata ndugu yako anaweza asikupende, saa zingine hata baba yako au hata mdogo wako anaweza asikupende, huwezi ukapendwa na kila mmoja, hata mitume hawakupendwa na wote na wengine walisulubiwa pamoja na kwamba walifanya mazuri. Kwa hiyo Prof. Muhongo wewe fanyakazi tena usihangaike hata kusoma ile mitandao, mimi sisomagi hiyo mitandao achana nayo watandae huko huko wenyewe wewe chapa kazi" alisisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Sababu Mh. Rais anajua akisema anasoma mitandao basi tutajua kama anajua vizuri swala la RC Daudi Bashite ambalo amelifumbia macho mpaka leo.
 
Mheshimiwa Lema napata wakati mgumu kukuelewa kwa haya uliyoyaandika, una uhakika gani kuwa mheshimiwa rais amewatumbua hao uliowataja kwasababu walikuja kukutembelea gerezani?

Nilidhani ungekuja na hoja za mashiko ambazo zingeweza saidia CHADEMA na wanachama wake kwa ujumla. Mh. rais kawatumbua hao uliowataja kwasababu zingine tofauti kabisa na ambazo zimewekwa wazi.
Mh.Lema nakushauri ujitafakari upya acha kutafuta kiki kwa kivuli cha rais wetu.
 
Jumapili njema jamani.
Ni muda mrefu sana kumekuwa na kilio cha raia kuminywa katika kutoa mawazo,kuamua na hata kutenda mambo mbali mbali ya kijamii na kibinafsi.
Mfano ni marufuku ya kufanya maandamano ya kitaifa kwa vyama vya siasa, utekwaji nyara wa baadhi ya wasanii, kupotea kwa watu kama Ben 8 o'clock nk,nk.
Hoja yangu ni hii,hivi uhuru unaweza kupatikana kweli wakati ukiwa huna kitu mifukoni?Kwa maoni yangu tujitahidi kuuona ukweli na umuhimu wa kuanza kujikomboa kibinafsi kwanza kabla ya kutafuta huo uhuru wa makundi kama vyama vya siasa,wanafunzi,wafanyakazi nk.Tafuta uhuru wako kwanza kabla hujajifungamanisha na watu wengine.
 
Jibu unalo kumbe...

watanzania tuna uoga sio amani mnadanganywa (By Roma Mkatoliki)
 
Siku si nyingi Gambo ataanza kutoa vibali vya kusali misikitini na makanisani
 
nikumbusheni ile kauli ya Abdallah Zombe kuhusiana na huyu ndugu.
 
Wananchi msijali uzuri miaka inakimbia fasta,angalia mheshimiwa amekamata mwaka wa pili.
 
Nianze kwa kuonesha masikitiko yangu makubwa sana kwa mwendelezo wa vitendo vya kinyama vinavyofanywa na Serikali ya Ccm na Bunge la JMT. Kitendo cha kunyanyasa Wabunge wsa upinzani ni cha kulaani sana katika nchi ambayo inataka kulazimisha wananchi kuhubiri juu ya Uzalendo. Uzalendo si dhana bali halisia ya matendo yenye fanaka na imani ya matunda yaliyojengwa kwa makubaliano ya makusudi katika kuhuisha amani ya Taifa.

Serikali ya ccm imekuwa mstari wa mbele kutaka kuivunja amani ya Taifa kwa kuonesha matendo yenye kuleta mpasuko katika Taifa. Wapinzani ndiyo njia mbadala ya kupata mawazo yatakayoweza kuisaidia nchi kusonga mbele. Mawazo yanayokinzana ndiyo hujenga, kuamini katika fikra zako pekee ni umasikini wa fikra mfu. Badala ya kutumia nguvu nyingi kuwadhalilisha mngekaa nao na kuchota yaliyo mazuri na kuyatumia ili kujenga Taifa moja.

Spika wa Bunge nae amekuwa kibaraka, ameamua kutumia mabavu, ubabe na mamlaka ili kupunguza nguvu ya wapinzani. Ni Spika huyu huyu aliyempiga kwa fimbo mgombea mwenzake wa ubunge mpaka kulazwa ndiye leo anayeongoza kufanya mambo ya hovyo. Bunge lingetumika kufanya kazi yake kusudiwa lingeheshimika kuliko vioja vinavoendelea vya kupuuza na kudhalilisha wapinzani.

Mnaposema uzalendo mnapaswa kujiangalia mara mbili juu ya Uzalendo mnaotaka kuaminisha Watanzania, muache unafiki kwanza, Serikali ya Ccm ndiyo ilisaini mikataba hii mibovu, Wabunge wa Ccm ndiyo waliopitisha sheria mbovu za uwekezaji na madini, halafu leo mnasema tumuunge Rais kwa kusambaza UZALENDO.

UZALENDO wa kuzuia mchanga
Yaani Uzalendo wa kuzuia ngozi kusafirishwa wakati nyama wameshachukua na kuisafirisha, huu ni uzuzu wa hali ya juu sana. Tuache unafiki, Rais ajue kuwa nchi hii ni mali ya wote na si ccm.
PhotoGrid_1496431935744.jpg
 
Mabango ya CCM haya. Uzalendo na hali ngumu ya maisha wapi na wapi?
 
Nguvu inayotumika kudhibiti vyama vya upinzani, tungetumia nguvu hiyo hiyo kwenye kilimo,tungekuwa tunagawa misaada kwenye nchi nyingine lazima tufike mahali tufanye kazi kwa ubunifu,kuliko kufanya kazi kwa kutumia misuli,wapinzani ni watanzani,ogopa kijiandaa kupigana na wananchi wako mwenyewe kwa kutumia majeshi ya ndani,hii ni kati ya vita ngumu sana duniani
 
Back
Top Bottom