Huyo Mama Hillary Clinton mbona sijamsikia akiendelea na Kampeni na matusi km Halima Mdee?
Kwanini CHADEMA wasitulie km Democrate party wamwache Rais aliyeshinda
huko USA Democrat walishinda zaidi ya kura milioni 2 lkn Trump aliongoza kwa majimbo mbona kuko kimya
msitake kuleta visiasa uchwara kuwa maisha yote ni siasa na kukaa vijiweni kusbiri kukosoa tu
Umemtaja Hilary Clinton wa huko 'kwenu' Marekani.
Lakini kumbuka Halima Mdee ni mbunge wa jimbo la Kawe na kujishughulisha na mambo ta kisiasa ndiyo wajibu wake mkuu kwa wapiga kura wake.
Lakini ngoja nikuulize swali dogo, through media tumekuwa tukishuhudia maandamano na ubebaji mabango kwa wananchi wa huko Marekani wakimpinga waziwazi Rais Trump, mbona hatujashuhudia Rais Trump akiyaamuru majeshi ya nchini humo yazime maandamano hayo?
Sasa ni kwa nini Rais wetu aogope mno wapinzani kufanya mikutano ya kisiasa kama kweli yeye anajiamini kuwa wananchi wengi wanamuunga mkono kwa mambo makubwa anayowafanyia wananchi wa nchi hii?
Ni vyema akatumia ile methali inayosema kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza.....
Kama kweli wapinzani hawana tena sera na support ya wananvhi, Magufuli na chama chake cha CCM hawapaswi kuwa na hofu, kwa kuwa hata wakiitisha mikutano yao haitapata watu watakaohudhuriia.
Kitendo cha Magufuli na chama chake cha CCM kuogopa kupita kiasi kuruhusu vyama vya upinzani kufanya mikutano, kunazua maswali mengi yanayokosa majibu.
Au pengine ndiyo kile kitu kinachoitwa guilty consciousness?
Refer matamshi ya EL ya hivi karibuni kuwa kura kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015, zilikuwa hazikuhesabiwa vizuri..........