Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Kupotea kwa watu si Ben tu wapo wengi wanaopotea kila siku nchini na duniani kwa ujumla
Hata yule mwenyejina linalofanana na Mashudu aliyekuwa mpinzani wa Nigeria aliposhinda uchaguzi alipelekwa gerezani akiwa hai baadae akarudishwa akiwa ndani ya sanduku,vyama tawala ni hatari tupu.
 
Huo ni ushamba na ukosefu wa hekima tu. Ni uchanga waacheni watakuwa tu na kuyaacha hayo wayafanyayo
 
Kwenu unaweza kumuuita tu
Hivi Mkuu kama hili la kuendesha shughuli za kisiasa hapa nchini, Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 3(1) inasema wazi kuwa nchi yetu itafuata mfumo wa vyama vingi na vyama hivyo vinapaswa viendeshe shughuli zao vikiwa huru, sasa inapotokea Rais aliyeko madarakani anasimama jukwaani na kusema kuwa anapiga marufuku shughuli zozote za kisiasa hadi mwaka 2020, ambapo anajua wazi kuwa kauli yake hiyo ni uvunjaji wa wazi wa Katiba yetu ya nchi ambayo aliapa kuilinda na kuitii.

Na inapotokea kuwa maDC, maRC na maRPC wanatekeleza kwa vitendo agizo hilo la Rais kwa kuzuia shughuli za kisiasa za vyama vya upinzani na wakati huo huo kuendelea kukiruhusu chama tawala cha CCM kuendelea na shughuli zake za kisiasa bila kubughuziwa.

Sasa inapotokea Mbunge kama Halima Mdee akatoa maoni yake, ambapo anatumia haki yake ya kikatiba iliyopo kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 18 ambayo inatoa Uhuru wa kila mwananchi kuwa huru kutoa maoni yake na kusema nchi yetu imeyageuza matamshi ya Rais kuwa sheria na kutokana na kauli hiyo ya Halima Mdee, anaibuka DC wake na kusema kuwa Halima Mdee ametumia lugha ya matusi dhidi ya Rais wetu na anawaamuru Polisi kuwa wamkamate na wamuweke ndani kwa masaa yake 48.

Hivi katika mazingira hayo anapotokea mtu kusema maamuzi hayo ni ya hovyo, hivi kweli atachukuliwa huyo mtu katukana?

Sasa anapotokea Mbunge kama Halima Mdee anatamka kuwa tatizo la Rais wetu ni kujiona tamko lake lolote ni sheria, ndiyo aonekane amemtusi Rais na kuonekana kama mhaini na kuswekwa ndani bila kesi yake kufikishwa mahakamani?

Nadhani kwa mfumo huu wa serikali hii ya awamu ya 5 unavyoenda nadhani ni vyema wakaamua kujenga magereza mengine mengi tu kwa kuwa nina hakika ni wengi tutaswekwa huko!
 
Nchi hii haijawahi kuwa na demokrasia.safari hii tumeolewa ndoa ya kisukuma,mume ndo mwenye kauli ya mwisho acha tuendelee kuisoma binary
 
Hivi kama mzazi wako anafanya mambo ya hovyohovyo kama vile kunywa pombe kwa kupitiliza na kufanya ufuska mtaani, ina maana kwa maoni yako watoto wa mzazi wa design hiyo hawapaswi kumwita mzazi wao kuwa ni wa HOVYO?

Tena siyo hivyo tu nitamwambia Dingi aacha mambo ya kipumbavu period.
 
Kagame stayle
Na ndiyo maana huyo Bwana mkubwa ziara yake ya kwanza kabisa kwenda nje ya nchi baada ya kuapishwa, akaenda kwa huyo rafiki yake lli ampe mbinu za namna gani anaweza kufanikisha kuua upinzani hapa kwetu.
 
Hata shetani anapambana sana ulimwenguni kuzuia wanadamu kumjua na kumtii Mungu, haya ni mambo ya nyakati tu kama ilivyokuwa kwa wengine duniani.Mwisho wa ubaya AIBU
 
Haya hufanywa na viongozi wa Kiafrika ili waogopwe na wananchi wao. Kwa yanayoendelea sasa tunaweza kusema hawakukosea kuliita Afrika "bara la giza".
 
It is true.

Lengo kubwa la CCM na hususani hii serikali ya awamu ya 5 ni kutaka kuua upinzani kwa mbinu zozote hata zile za haramu ili nchi hii irejee kwenye mfumo wa chama kimoja
Huyo Mama Hillary Clinton mbona sijamsikia akiendelea na Kampeni na matusi km Halima Mdee?
Kwanini CHADEMA wasitulie km Democrate party wamwache Rais aliyeshinda
huko USA Democrat walishinda zaidi ya kura milioni 2 lkn Trump aliongoza kwa majimbo mbona kuko kimya
msitake kuleta visiasa uchwara kuwa maisha yote ni siasa na kukaa vijiweni kusbiri kukosoa tu
 
Huyo Mama Hillary Clinton mbona sijamsikia akiendelea na Kampeni na matusi km Halima Mdee?
Kwanini CHADEMA wasitulie km Democrate party wamwache Rais aliyeshinda
huko USA Democrat walishinda zaidi ya kura milioni 2 lkn Trump aliongoza kwa majimbo mbona kuko kimya
msitake kuleta visiasa uchwara kuwa maisha yote ni siasa na kukaa vijiweni kusbir/QUOTE]
Ngoja nikuulize swali, hivi huko 'kwenu' Marekani wananchi wa huko hawamkosoi Rais wao Trump kwa madudu mengi anayoyafanya?

Mbona mara nyingi kupitia media mbalimbali tumekuwa tukishuhudia maandamano ya wamerekani tena wakibeba mabango wakimpinga waziwazi Trump. Mbona hatujashuhudia Polisi wa huko wayazime maandamano hayo kwa viringu na magari ya washawasha?

Sasa ni kwa nini hapa TZ, ikiwa Magu na CCM yake wanaamini kuwa Rais Magufuli anafanya kazi mzuri sana, ni kwanini asiwaache wapinzani wakajieleze kwa wapiga kura wao na wananchi ndiyo wawakatae?

Hizi dalili za serikali ya Magufuli kuwafhibiti wapinzani kwa kiwango hiki, kunaleta maswali mengi yanayokosa majibu, au pengine ni kweli kura zilikuwa hazikuhesabika vizuri kama alivyobainisha EL?

Guilty people are always afraid.......
 
Me nachokiona Viongozi wetu wanadhani ukiwa mpinza mbasi wewe sio mtanzania umetoka somalia kuja kua mpinzani kwenye nchi ambayo sio yako lakini wangekaa wakatafakari kidogo wakajua ni watanzania wenzao hata awa ma DC na Ma RC wasingekua wanatoa matamko ya ovyo kwa akina Mdee lakini kwa sababu wana huwezo mdogo wa kufikiri wanafikiri wamezaliwa wao watawale tu hakuna chama kingine kinaweza kutawala Alafu kua Rais wa Tanzania haimaanishi kwamba wewe una akiri kuwazadi watu wote milioni 50 unaowaongoza
 
Tatizo watanzania wengi hawajielewi, pamoja na matatizo yote haya yanayosababishwa na serikali ya ccm bado huendelea kuichagua! Siku bunge letu likiwa na idadi kubwa ya wabunge wa upinzani ndio itakuwa mwisho wa maringo na majivuno ya watawala wa ccm! Hawa wachache kina Esta na Halima wanawapanikisha kina Job kiasi hiki, wangekuwa wengi hakika tungeheshimiana! Wameshatuona wa tz mazoba!

Eti wanasema mataifa mengine ikiwemo na Kenya wanamuomba Baba J akawe rais wao! Huyo hapo Kenya hawezi kuongoza hata kwa wiki 2, wakenya wanajiamini, sio waoga, sio wanafiki na wengi wao wameelimika vya kutosha! yeye hapendi kuongoza watu wa aina hiyo.

Wiki mbili nyingi hata siku nne hawezi kufikisha
 
Huyo Mama Hillary Clinton mbona sijamsikia akiendelea na Kampeni na matusi km Halima Mdee?
Kwanini CHADEMA wasitulie km Democrate party wamwache Rais aliyeshinda
huko USA Democrat walishinda zaidi ya kura milioni 2 lkn Trump aliongoza kwa majimbo mbona kuko kimya
msitake kuleta visiasa uchwara kuwa maisha yote ni siasa na kukaa vijiweni kusbiri kukosoa tu
Umemtaja Hilary Clinton wa huko 'kwenu' Marekani.

Lakini kumbuka Halima Mdee ni mbunge wa jimbo la Kawe na kujishughulisha na mambo ta kisiasa ndiyo wajibu wake mkuu kwa wapiga kura wake.

Lakini ngoja nikuulize swali dogo, through media tumekuwa tukishuhudia maandamano na ubebaji mabango kwa wananchi wa huko Marekani wakimpinga waziwazi Rais Trump, mbona hatujashuhudia Rais Trump akiyaamuru majeshi ya nchini humo yazime maandamano hayo?

Sasa ni kwa nini Rais wetu aogope mno wapinzani kufanya mikutano ya kisiasa kama kweli yeye anajiamini kuwa wananchi wengi wanamuunga mkono kwa mambo makubwa anayowafanyia wananchi wa nchi hii?

Ni vyema akatumia ile methali inayosema kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza.....

Kama kweli wapinzani hawana tena sera na support ya wananvhi, Magufuli na chama chake cha CCM hawapaswi kuwa na hofu, kwa kuwa hata wakiitisha mikutano yao haitapata watu watakaohudhuriia.

Kitendo cha Magufuli na chama chake cha CCM kuogopa kupita kiasi kuruhusu vyama vya upinzani kufanya mikutano, kunazua maswali mengi yanayokosa majibu.

Au pengine ndiyo kile kitu kinachoitwa guilty consciousness?

Refer matamshi ya EL ya hivi karibuni kuwa kura kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015, zilikuwa hazikuhesabiwa vizuri..........
 
No Longer at Ease!uoga wa watanzania ndiyo unaouweka ccm mtaani.Ki uhalisia hakuna mtanzania anayeitaka ccm na siasa za chuki
 
Mhaini kesi yake ni kifo au kifungo cha maisha Kuna mpinzani kapata adhabu kama hiyo?

Tufuate sheria,kanuni na taratibu tu hakuna shida
Yeye ndio hafuati sheria mshaurini afute vyama vya upinzani ili aishi bila stress,upinzani kazi yke ni kukosoa ili ujisahishe pia siasa sio uhasama,chuki,visasi,ubabe anaofanya yeye.kila cku povu linamtoka na kuropoka tu
 
Tatizo ni kuwa unamkosoa kwa jinsi gani? Kumkosoa kwa kuhamasisha watu watumie lugha itakayosikika na kuelewaka na serikali huku ukijua viongozi wa serikali na walinda amani wanauliwa na watu wasiojulikana, ukishukiwa kwamba unapigia chapuo uhaini utamlaumu anaye kushuku? Ukiitwa mhaini utamlaumu nani zaidi ya ulimi wako uliokuponza?

Unazungumza vipi lugha ya kihaini kama wewe na wanaokuzunguka hamzungumzii hiyo lugha? Acha hata kufikiria kutenda matendo ya kihaini. Kumbuka yale maneno "kimtokacho mtu ndicho kilicho ujaza moyo wake".



Na washawasha!
 
Na ndicho kinachowatokea Bulaya na Mdee nje ya bunge sasa hivi


Jiengezeni kidogo basi, kama umekosa nidhamu ndani ya bunge, unakuwa nayo vipi nje ya bunge? Kuna wakati huwa na pata taabu ni kijiuliza kwa nini baadhi ya hawa jamaa wanastahili kuitwa title ya waheshimiwa. Hivi unakuwaje mheshimiwa kama huwezi hata kujiheshimu?


Na washawasha!
 
Yeye ndio hafuati sheria mshaurini afute vyama vya upinzani ili aishi bila stress,upinzani kazi yke ni kukosoa ili ujisahishe pia siasa sio uhasama,chuki,visasi,ubabe anaofanya yeye.kila cku povu linamtoka na kuropoka tu
Yaani tatizo linaloendelea nchini kwetu halitofautiani sana na ile hadithi ya yule Mfalme aliyekuwa mkali sana ambaye wananchi wake walikuwa wakiogopa kumwambia lolote.

Siku moja alikuwa akitembea uchi mitaani lakini wananchi wake hawakuthubutu kumwambia ukweli kuwa anatembea uchi badala yake wakawa wanamsifu kwa nyimbo na mapambio kuwa Mfalme leo umependeza sana na vazi lako!

Hata hivyo mtoto mmoja akamwambia mama yake kwa sauti kuwa mbona Mfalme leo anatembea uchi?

Mama yake akamuonya mwanae kuwa asirudie kusema hivyo kwa kuwa akisikika na Mfalme, maisha yake na ya mamamtu yatakuwa hatarini...

Ndicho kinachotokea hapa TZ hivi sasa.Watu wengi wananung'unika kimoyomoyo namna wasivyoridhishwa na ubabe anaoutembeza Mkuu wetu wa nchi na wengine wamo hata ndani ya CCM yenyewe, lakini wanakosa ujasiri wa kuyasema hayo hadharani.

Kama kweli Taifa letu litataka kuepuka hali ya machafuko huko siku za mbele, ni lazima kila mtu apaze sauti kuwa nchi yetu inapaswa kuongizwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi na si kwa utashi wa mtu na nchi yetu isigeuzwe ya ONE MAN SHOW
 
Back
Top Bottom