Lema: Msitetee mtu sababu ya Ushungi na Kanzu, teteeni mtu sababu ya Haki

Lema: Msitetee mtu sababu ya Ushungi na Kanzu, teteeni mtu sababu ya Haki

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Lema amewaambia waislamu wasitetee mtu sababu ya Ushungi na Kanzu, teteeni mtu sababu ya Haki.

Huku akiwaambia Wakristo wasitetee mtu sababu ya uchungaji bali wamtetee sababu ya haki.

Akisema kuwa wengi wanaleta mambo ya udini sababu hawamjui Mungu, Maandiko wala haki, na kwamba wangekuwa wanajua haki wasingekuwa wanachonganisha watu kwa sababu ya udini.

Lema ameyasema hayo katika mkutano wa kupinga mkataba wa bandari unaofanyika Temeke leo tarehe 23/7/2023.
 
Hili taifa lazima liwe la watu waliopevuka kifikra, tusiendelee kuishi kama watumwa wa fikra za wengine, huku wao wanajipigia 10% wengine wanabaki kuwatetea kwasababu ya mwenzao katika imani, huu ni utumwa mbaya sana.
 
Baba wa taifa aliwahi kusema kuwa mwanasiasa aliyefilisika kisiasa hukimbilia dini na kabila kama njia ya kujihalalisha. Sio siri tena kuwa aliyekuwa anaimbwa kuwa anaupiga mwingi pumzi imekata, sasa anakimbilia kwenye Udini na Uzanzibari
 
ChAdeMa waondoe KWANZA udini,ukanda na ukabila kwenye chama Chao ndio tutawaona wakweli. Haiwezekani wabunge wa viti maalumu karibu wote ni wachaga! Tena Wakristo!
 
ChAdeMa waondoe KWANZA udini,ukanda na ukabila kwenye chama Chao ndio tutawaona wakweli.
Mkataba wa hovyo wa bandari umewahi kuuona? nina wasiwasi utakuwa debe tupu.

Nenda kausome ule mkataba wa kinyonyaji wa bandari, kisha ujiulize kama Chadema wanachosema uongo.
 
Mkataba wa hovyo wa bandari umewahi kuuona? nina wasiwasi utakuwa debe tupu.

Nenda kausome ule mkataba wa kinyonyaji wa bandari, kisha ujiulize kama Chadema wanasema uongo.
Nimeuona Mangi. Unahitaji maboresho.

Anyway sio Kila mnayetofautiana mtazamo ni 'debe tupu'
 
Lema amewaambia waislamu wasitetee mtu sababu ya Ushungi na Kanzu, teteeni mtu sababu ya Haki.

Huku akiwaambia Wakristo wasitetee mtu sababu ya uchungaji bali wamtetee sababu ya haki.

Akisema kuwa wengi wanaleta mambo ya udini sababu hawamjui Mungu, Maandiko wala haki, na kwamba wangekuwa wanajua haki wasingekuwa wanachonganisha watu kwa sababu ya udini.

Lema ameyasema hayo katika mkutano wa kupinga mkataba wa bandari unaofanyika Temeke leo tarehe 23/7/2023.
yupo sawa, kabisa
 
waTanzania tunayo changamoto ya kutofautisha mapenzi ya kisiasa na maslahi mapana ya uchumi.
 
Back
Top Bottom