Kwa mawazo hayo, utakuwa sahihi zaidi ukihoji uwepo mzima wa CHADEMA (raison d'être) na wanachokipigania ambacho, kama ulivyofafanua, hakiwezekani. Yaani unaona wanafanya uzururaji tu usiokuwa na tija inayopimika.
Yaani watu wamhangaikie Lissu atoke jela ili arudi kujiunga na muendelezo wa "uzururaji" wa CHADEMA usio na tija? Kwa nini, kwanza, CHADEMA yenyewe isikubali kuachana na huo upuuzi inaofanya kisha Lissu aombewe huo msamaha ili arudi uraiani kufanya mambo ya maana?
Tunajua serikali ina mpango gani kwa Lissu na CHADEMA kwa ujumla (it's open). Tunajua kuwa CHADEMA wanapambania mambo ambayo ni magumu sana kufanikiwa kiasi cha kuonekana hayawezekani. LAKINI, Lissu na viongozi wa CHADEMA wameamua kuwa hawatakata tamaa na hawatatafuta shortcut katika mapambano yao.
Lissu mwenyewe amesema wazi kabisa kuwa hataki huruma wala msamaha wa Rais katika kesi hii na yuko tayari kwa hukumu ya kunyongwa akikutwa na hatia. Kama ni maumivu, Lissu ameshaumizwa sana na serikali ya JMT miaka mingi tangu akiwa kijana mdogo. Kwa hiyo, kwa suala la maumivu ya Lissu, ni yeye pekee ndiye mwamuzi. Haiwezi kuwa initiative ya Lema, kiongozi yeyote wa CDM wala mtu mwingine yeyote yule.
Unaweza kuwaona na kuwaita wajinga, wapuuzi, wazururaji, wasiojali, n.k. LAKINI ieleweke kuwa maamuzi ya kufa au kupona yanabakia kuwa yao pekee (Lissu, viongozi na wanachama wa CDM).