Lema: Nilitegemea mpaka sasa baada ya statement ya Rais Samia kuhusu mauaji ya Ally Kibao basi Waziri Masauni, IGP wawe wamejiuzulu

Lema: Nilitegemea mpaka sasa baada ya statement ya Rais Samia kuhusu mauaji ya Ally Kibao basi Waziri Masauni, IGP wawe wamejiuzulu

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Godbless Lema ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Kaskazini akieleza kushangazwa kwake mpaka sasa kwanini Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni na IGP kutujiuzulu kufuatia tukio la kutekwa na kuuawa kwa Ally Mohammed Kibao.

Niliposikia Ali amekamatwa ameshushwa kwenye basi sikuhisi kwamba ni tukio ambalo lingeweza kumpotezea maisha, niliamini kwamba pengine amekamatwa na vyombo vya ulinzi na usalama pengine kwa kesi zingine za kisiasa na baada ya siku chache pengine tungemuona.

Lakini taarifa ya jana, Mh. Waziri(Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni) upo hapa baada ya kupata taarifa kwamba Ali ameokotwa Ununio, Maisha yangu yamekuwa magumu sana, Lakini Mh. Waziri nikuombe sana usiende tena kwenye msiba wa mtu mwingine ambaye ametekwa nenda kwenye msiba wa mtu ambaye ameteka”

"Nyie ambao mko serikalini mjue kuwa haya mambo (ya utekaji na mauaji ya raia) yakiendelea kuna kisasi kinaweza kikazaliwa kwa sababu damu huwa inanena"

Pia soma
 
Badala ashangae kwann mbowe aambatane na masauni msibani anahoji kujiuzuru
Ameambatana nae vipi?
Kwani walipanda gari Moja?
Au ulitarajia Mbowe angemzuiya Masauni?
Kama nikumkataa Masauni ingepaswa kuwa jukumu la familia na ndicho kilichofanyika
 
Hawawezi kujiuzulu kwa sababu nchii hii uwaziri ni fursa ya ulaji.Hata IGP hawezi kujiuzulu pia.Hao wote wanajua kinachoendelea
 
Hii iataleta tafrani endapo Polisi hawakua na taarifa ya kwenda kumteka,ila vyombo vingine ndo vikamteka Meddy,maana lawama zote ni kwa polisi,TISS wao wana kinda ya kutoshtakiwa na polisi ndo hao wanatupiwa lawama.Polisi kutoshughulika na hilo suala,watazidi kuchukiwa,unless otherwise ni wao ndo watekaji.
 
Godbless Lema ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Kaskazini akieleza kushangazwa kwake mpaka sasa kwanini Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni na IGP kutujiuzulu kufuatia tukio la kutekwa na kuuawa kwa Ally Mohammed Kibao.

Niliposikia Ali amekamatwa ameshushwa kwenye basi sikuhisi kwamba ni tukio ambalo lingeweza kumpotezea maisha, niliamini kwamba pengine amekamatwa na vyombo vya ulinzi na usalama pengine kwa kesi zingine za kisiasa na baada ya siku chache pengine tungemuona.

Lakini taarifa ya jana, Mh. Waziri(Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni) upo hapa baada ya kupata taarifa kwamba Ali ameokotwa Ununio, Maisha yangu yamekuwa magumu sana, Lakini Mh. Waziri nikuombe sana usiende tena kwenye msiba wa mtu mwingine ambaye ametekwa nenda kwenye msiba wa mtu ambaye ameteka”

"Nyie ambao mko serikalini mjue kuwa haya mambo (ya utekaji na mauaji ya raia) yakiendelea kuna kisasi kinaweza kikazaliwa kwa sababu damu huwa inanena"
Ni lini utekaji na uuaji vilikoma kuwa sehemu ya maisha ya kijamii?. Kila kinachofanyika Tanzania ya sasa ni siasa tu, yaani siasa zenye kuambatana na maongezi meengi ambayo hayana tija yoyote.

Huyo Marehemu alikuwa binadamu aliyeishi katikati ya wanadamu, kwa hiyo kufanyiwa unyama aliofanyiwa mpaka akapoteza uhai wake pengine chanzo ni muingiliano wa kawaida wa maisha ya kibinadamu.

Watu walikuwa wanatekwa na kuuliwa tangu awamu ya kwanza ya Nyerere. Mauaji mengi tu yamekuwa yakifanyika katika awamu zote sita, haya ni masuala yenye kuhitaji busara katika kuweza kuyatatua.

Tatizo siasa za vyama vingi zinakuja na uhasama pamoja na kila aina ya uadui.
 
Back
Top Bottom