Lema, umelikoroga, rudi Canada kwanza ujifikirie

Lema, umelikoroga, rudi Canada kwanza ujifikirie

Hiyo hotuba aliandaliwa? Kama ni ndio basi hawampendi. Kama ni yeye basi arudi Canada akajipange namna ya kuongea.
 
We una uwezo wa kua argue na Mimi kweli
Akili ndogo huwa naipa nafasi ijiangamize yenyewe.
Na hujajibu hoja kwa nini mwanaiasa asiye na akili, amerudi tu anaanza kutukana masikini.
Halafu anategemea masikini hao wamwelewe au wampe kura 2025!
Huo ndo tunaita umburula!
 
Akili ndogo huwa naipa nafasi ijiangamize yenyewe.
Na hujajibu hoja kwa nini mwanaiasa asiye na akili, amerudi tu anaanza kutukana masikini.
Halafu anategemea masikini hao wamwelewe au wampe kura 2025!
Huo ndo tunaita umburula!
Lema akiri kubwa sana we popoma huwezi mwelewa kamwe
 
Lema amekuwa nje ya nchi kwa muda mrefu. Karudi ana mawazo ya ajabu ajabu na bado anafikiri yupo kipindi cha Magufuli, kile cha ugomvi ugomvi na mivutano. Anachoongea sasa ni kama samaki aliyetolewa majini. Hajui siasa za Tanzania zimesonga.

Ameanza kwa kuwananga madereva wa bodoboda, ati kazi ile ni laana. Sasa hata kabla hajaomba radhi, tunasikia bado kakalia kuti lile lile la kuwalaani bodaboda, kwav ile ati watoto wa wakubwa akiwemo Majaliwa Waziri Nkuu hawaendeshi bodaboda!

Huyu bwana ana kichaa.

Anashambulia nyasi zitakazo mwunguza.
Ni kama mtoto anayejamba halafu anashangaa harufu inatoka wapi!

A powerful mass, umma wa kikundi chochote nchini ndiyo oxygen ya mwanasiasa, na kata hiyo oxygen unakufa.

Mama Samia alitumia akili kubwa kuwaondoa machinga barabarani, hakuwananga, hakuwatukana, wala hakutumia polisi kuwatoa, aliwabembeleza na wakamwelewa.

Sasa Lema kaingia kichwa kichwa kuwatukana boda boda. Najiuliza, huko Canada hakutumia muda wake kusoma vitabu vya siasa za Class Struggle?

Nashauri arudi Canada na akajiandae vizuri zaidi.
1. Kama ni kichaa, kinachokusumbua wewe kujibizana na kichaa ni kitu gani?

2. Lakini kikubwa kabisa ni hiki, hata wewe ni kichwa maji tu maana hukumwelewa na hutaweza kumwelewa Godbless Lema.

Alisema kazi ya bodaboda ni moja ya ishara (indicator) ya umasikini. Na umasikini ndugu yangu ni LAANA. Umasikini wa Tanzania ni WA kutengenezwa na CCM na serikali yao..

Hii ndiyo point ya Godbless Lema na Kwa hakika ameeleweka vyema kabisa

3. Sasa basi, Kwa kuhitimisha I can seriously say, kuwa, katika situation kama hii ambayo bodaboda wenyewe Kwa asilimia kubwa wamemwelewa GL, lakini wewe na kusoma kwako hadi form four division four unajifanya mjinga, huelewi, basi actually wewe Jidu La Mabambasi Kwa jina lako kabisa ndiye kichaa na chizi halisi!!
 
Hii ndio tulikuwa tunataka, tunataka watu wenye mawazo tofauti na yenu, tunataka watu wanaofikiri tofauti na nyie haiwezekani wooote tudumishe fikra za mwenyekiti.

Boda boda ni laana hata mimi naona Lema yuko sawa, watu gani hawapati pesa mpaka wakaliwe nyuma bhana. Zipo fursa nyingi za kutengeneza ajira na zina madhara machache kuliko boda boda. Haki sema laana haina maana wapo wachache wamenufaika nayo ila wengi wameumia.

Serikali na wanasiasa walaghai mnatumia shida za bodaboda kutimiza yenu hii ndio laana kubwa waliyonayo boda boda ltr 5 za petrol tu wananfanya unachowaambia wafanye.
yupo sawa kabisa majitu kugonga raia mwenzake hayaogopi hata kwenye zebra, ndio majizi ya tatu mzuka, ndio wanaoharibu wake za watu na watoto wa shule. Ndio watumia na wasbazaji madawa ya kulevya wakuu.

NB: Ni kero zangu ninazoziona kwao sijui kwa mlengwa atakaye quote hapa...
 
Lema kalewa raha za Kanada, hivyo anataka watanzania tuishi maidha kama aliyo yaona huko Kanada!!!

Mzee Lema nakushauri waombe radhi waendesha bodaboda, hakika umewakosea sana kuwaita masikini.
Watu wa kaskazini walahidi(materialists),wanaabudu Mali/hadhi,akifika hatua flan anayoamini ni ya juu kimaisha Basi wa chini mtakoma
 
Kaja na matusi mapya ;
1.Washamba
2:Laaana
3:Mke wangu nitamkana akijiunga vicoba
3:Mimi ni mchagga
5:Arusha wanajielewa wanajua hata cafelate ni nini
Anayafyatua tu maneno hii inaitwa mtajuana wenyewe.
 
Kaja na matusi mapya ;
1.Washamba
2:Laaana
3:Mke wangu nitamkana akijiunga vicoba
3:Mimi ni mchagga
5:Arusha wanajielewa wanajua hata cafelate ni nini
Kwenu hayo ni matusi kumbe..!?
 
Kama unamjua mbunge wa Arusha 2025, tuambie na Ajaye ni nani!!
Mama for presidency till death. We huoni nchi ilivyo shwari? Furaha imeongezeka mara dufu. Bei ya vitu kushuka ni swala la mda mda tu. Subili vita ya Ukraine iishe vitashuka sequentially
 
Mama for presidency till death. We huoni nchi ilivyo shwari? Furaha imeongezeka mara dufu. Bei ya vitu kushuka ni swala la mda mda tu. Subili vita ya Ukraine iishe vitashuka sequentially
Presidency till death unamaanisha nn?
 
Back
Top Bottom