Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,922
- 3,252
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amesema yupo katika hali ya kukata tamaa kutokana na mwenendo wa baadhi ya vijana wanaotanguliza burudani badala ya masuala muhimu ya kisiasa na kijamii.
Akizungumza Oktoba 13, 2026 jijini Arusha katika hafla ya uzinduzi wa ofisi ya CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Lema amesema baadhi ya vijana wamekuwa wakijikita katika matamasha ya burudani, ikiwemo tamasha la kuadhimisha miaka 30 ya muziki wa Bongo Fleva na matamasha ya Nyama Choma, akidai kuwa hali hiyo inawafanya kusahau masuala ya msingi yanayohusu haki na mustakabali wa taifa.
Amesema inaumiza kuona baadhi ya wananchi hawatoi uzito unaostahili kwa mapambano ya kudai haki, akitolea mfano wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ambaye anashikiliwa mahabusu ya magereza akikabiliwa na kesi ya uhaini.
Aidha, Lema amewataka vijana kuelekeza nguvu zao katika masuala muhimu ya kisiasa na kufuatilia mwenendo wa kesi ya Tundu Lissu, huku akieleza kuwa licha ya juhudi zake za muda mrefu katika kupigania haki za wananchi, mwenendo wa baadhi ya vijana umemvunja moyo na kumfanya ajikute katika hali ya kukata tamaa, akimuomba Mungu amsaidie.