Lema: Waziri Kalemani alimpigia simu mkewe akimtaka kuwapa Polisi ushirikiano wa kuondoa kamera

Lema: Waziri Kalemani alimpigia simu mkewe akimtaka kuwapa Polisi ushirikiano wa kuondoa kamera

Tarehe 7/9/2017 ilikuwa Ni siku ambayo MUNGU huenda hakulala Kama huwa analala kwani mja wake asiye na hatia LISSU wenye mamlaka walitaka kuhitimusha maisha yake.
Rais wa nchi alikuwepo.
Makamu wa RAIS alikuwepo.
Waziri Mkuu alikuwepo.
IGP pia alikuwepo.
Mkuu wa TISS alikuwepo.
Mkuu wa JWTZ alikuwepo.
DCI naye alikuwepo.
Mkuu wa zima Moto alikuwepo.
Mkuu wa JKT alikuwepo.
Mkuu wa skauti alikuwepo.
Mkuu wa PCCB alikuwepo.
RPC walikuwepo.
OCD walikuwepo.
Mawaziri walikuwepo.
Jaji Mkuu alikuwepo
SPIKA wa bunge alikuwepo.
Wote hao Hawakufahamu Nani aliyerusha risasi 38 kwa LISSU.Ila Mungu pekee ndiyo hakulala mchana ila wote Hapo juu walikuwa wamesinzia.
Waziri Medard kalemani ndiye aliyeshiriki kutoa CCTV camera kwenye nyumba yake hivyo alipaswa kuhojiwa ipasavyo.
Mfugale, Chamriho, Kilangi, Bashiru, Polepole, kijazi et al there must be something. Nyie hamuoni??
 
Hizo ni chokochoko kama mnadai aliyepanda mpango amekufa basi na kesi imekufa msitusumbue na mambo yaliyokufa.

Kuhusu CCTV kwani anayetakiwa kuzitoa ni Nani? Kwani kinachofanyiwa uchunguzi ni Yale makamera au server?

Ukitafakari vizuri utabaini kwamba endapo washika dau wangepanga Mauaji mambo mengi yasingefanyika wangeweza kumtafuta kwa njia nyingi rahisi kwani hawana woga wa kumshambulia mtu kwa kificho wangemsubiri nyumbani au kwenye ulevi pia CCTV zingerekenishwa mapema.

KILICHOTOKEA Kuna wahusika wasio na utaalamu walifanya tukio kwa maslahi Yao lakini pia serikali kutokana na usumbufu wake wakatekeleza ule usemi wa adui muombee njaa. Ni sawa na wewe ukisikia mchawi wako amepata ajali utakachoweza kufanya ni zaidi ya ajali.
Hao "wahusika wasio na utaalamu" kwa nini hawajawahi kutafutwa??
 
Hebu isome Tena hiyo thread kuna mahali unajichanganya na ama hujarudia kusoma na umekimbilia kujibu! Mleta Uzi kaandika kuwa, kalemani alimpigia simu make wake akimuelekeza kuwapa ushirikiano wote wanaoutaka! Upo?
Tatizo liko kwenye kuelewa... Inaonekana huyu jamaa ni mzito kuelewa akisoma kitu..... Eti mke wa mbunge!? Pole ndugu barafuyamoto soma vizuri uelewe.
 
Na baada ya happ aliteuliwa Uwaziri
Alikua tayari ni waziri, ndiyo maana aliishi hizo nyumba za viongozi (nyumba za serikali) hapo area D. Nyumba yake ilikua karibu na nyumba ya Lissu na Naibu speaker Tulia Akson.
 
Alikua tayari ni waziri, ndiyo maana aliishi hizo nyumba za viongozi (nyumba za serikali) hapo area D. Nyumba yake ilikua karibu na nyumba ya Lissu na Naibu speaker Tulia Akson.
Kalemani tayari bado Tulia. Kitu kizito kinamnyemelea.
 
Kwa hiyo kila kifo ni adhabu.?
Jibu ni ndiyo. Kifo kama kifo ni adhabu iliyoletwa baada ya dhambi.

Hata huyo Lissu atakufa siku yake ikifika maana hata yeye pia ana dhambi zake. Mimi na wewe pia ipo siku tutalipia dhambi zetu.

Lakini mimi binafsi naweza kuishi mpaka siku atakaporudi tena Messiah sababu nimemwamini na kumtwisha zigo langu la dhambi.

Ukimwamini Messiah na kuzishika Amri zake, na kufanya yote kama alivyoagiza huwezi kufa na hata ukifa utaishi tena.
 
Uchunguzi uanze wauji tuwajue na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria
 
Lema! Nakuamuru kwa jina la aliye juu, toka mafichoni, njoo nyumbani. Unajificha una kosa gani? Njoo ujieleze kieleweke.
 
Kama ni hivyo huyo Lema yeye amejuaje kama siyo uongo mkubwa,yani Kalemani ampigie simu mke wake halafu Lema ndiyo atoe hiyo taarifa na iaminike kweli?
CCTV ilikuwepo au haikuwepo kwa Kalemani?

RPC alisema au hakusema kuwa wameipata CCTV camera?

CCTV iliondolewa au haikuondolewa nyumbani kwa Kalemani?

CCTV inapoondolewa, inaweza kuondolewa bila ya mwenye nyumba kuwapa ushirikiano?
 
Mtu anampigia simu mke wake maongezi yao yeye ameyajuaje.
Mke wa Kalemani ndiye aliyewaambia majirani. Mke wa Kalemani alielewa kuwa camera yao imeondolewa kwa nia njema, ili wataalam wakawabaini washambuliaji. Ndiyo maana hakuona shida kuwaambia majirani.
 
Lema kupitia space anasema

"Waziri Kalemani, alimpigia mke wake simu kwamba polisi wanakuja hapo kuondoa kamera wape ushirikiano, hii ni baada ya Tundu Lissu kupigwa risasi.." —; Godbless Lema

Natamani kusikia hii Taarifa siyo kweli, natamani kusikia kutoka kwa Mhe. Kalemani. Kama mke aliambiwa atoe ushirikiano means waliomba ushirikiano kwa Kalemani wanafahamika na yeye anawafahamu.

Tunafanya haya kwa sababu yakutafuta Nini hapa Duniani? Vyeo tu au Kuna mengine. Inaumiza Sana pale mapadre, maaskofu na wachungaji wanapojua kwamba waumini wetu wanatembea na dhambi vifuani mwao. Pls natamani niskie full story ya huu ushahidi wa Lema.
uwongo mtupu, tupa kule!
 
naendelea kunywa supu, kabla ya mawio ukwelio utajulikana tu.
 
Mke wa Kalemani ndiye aliyewaambia majirani. Mke wa Kalemani alielewa kuwa camera yao imeondolewa kwa nia njema, ili wataalam wakawabaini washambuliaji. Ndiyo maana hakuona shida kuwaambia majirani.
Mke wa Kalemani atakuwa shaidi nambari moja kwa kesi ya Lissu upande wa mashtaka, ipo siku tu yote yaliyo sirini yataanikwa.
 
Back
Top Bottom