Kulwa Jilala
JF-Expert Member
- Sep 6, 2022
- 3,891
- 8,448
Wote mmeshindwa kuwafunga, wanadunda mitaaniSiyo wote walikuwa waovu, waovu ni wale Sukuma gang kama Saambaya, Bashite na the likes
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wote mmeshindwa kuwafunga, wanadunda mitaaniSiyo wote walikuwa waovu, waovu ni wale Sukuma gang kama Saambaya, Bashite na the likes
Waliyaondoa mashtka wao walioyaleta Sasa yéyé c alkuw tayr kwa utetezi?Mbowe alipokutwa na kesi ya kujibu alipangua mashitaka?
Hayakuondolewa yalisogezwa mbele baada ya gaidi kuomba alambe asaliWaliyaondoa mashtka wao walioyaleta Sasa yéyé c alkuw tayr kwa utetezi?
Vip kuhusu Ile kesi ya akwilina walihukumiwa jela kabisa baadae mahakama kuu ikafutilia mbali hukumu hyo
Hakuna ugaidi WA kukata miti Sawa Lumumba?
Serikali wajanja walimzungusha kwwnye kesi Hadi vihela vyote vya wizi vikaisha ndo wakamwachiaWameshindwa kumfunga miaka 30
Hakutetewa na mabeberu wala viongozi wa dini
Adhabu yenyewe ya kukiri ni milioni 5 , lakini tuliambiwa ujambazi alioufanya ni wa mabilioni ya fedha!
Unaweza kumwibia mtu milioni 500 alafu akubari ukiri umpe milioni 5 yaishe?
#usaniii
Sheria haijaongelea habari za kifungo cha jela, bali imesema "Katika kipindi cha miaka 5 kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu amepata kuhukumiwa na kupewa adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na utovu wa uaminifu au kwa kuvunja Sheria ya maadili ya viongozi wa Umma."1. Kosa la uchochezi ni kosa la jinai, hivyo kesi ya uchochezi ni kesi ya Jinai.
2. Ili kupoteza sifa za kugombea ubunge ni lazima ukutwe na hatia na kuhumiwa kifungo cha jela kinachozidi miezi 6 jela.
3. Mtuhumiwa anayekiri kosa kwa plea bargain au kifungo cha nje kiahesabiwa sio kifungo cha jela hivyo anaruhusiwa kugombea ubunge.
Mfano mzuri ni Mbunge wa Njombe, Mhe. Deo Mwanyika alikuwa na kesi ya uhujumu uchumi, akakaa mahabusu miaka 4, akakiri kosa, akalipa faini na kuachiwa huru sasa ni Mhe. Mbunge.
P
Tuoneshe hukumu ya gaidi tuione hapa! Mwambie makonda asiye gaidi na mbowe gaidi wakaombe visa ya USA Tuone nani mpumbavuUnashangaa nini na upo na gaidi aliachiwa na kulambishwa asali ikulu siku hiyohiyo
USSR
Bora sabaya kashinda kesi,kuliko yule gaidi na muuaji aliye achiliwa kwa utata,Halafu mvuta joint na mwizi wa kuku wanaozea jela
Jambazi Mkuu wa Wilaya anasamehewa ili aje kupumzika na mastupid huku uraiani.
Ile kesi ilikuwa ya kubumba kesi feki.Bora sabaya kashinda kesi,kuliko yule gaidi na muuaji aliye achiliwa kwa utata,
Hukumu ya gaidi ilisogezwa mbele siku akiingia rais asiyetoa asali gaidi anarudi mahakamani.Tuoneshe hukumu ya gaidi tuione hapa! Mwambie makonda asiye gaidi na mbowe gaidi wakaombe visa ya USA Tuone nani mpumbavu
Misukule ya mwendazake mna akili finyu mnoHukumu ya gaidi ilisogezwa mbele siku akiingia rais asiyetoa asali gaidi anarudi mahakamani.
Jambz sabaya sashv Kabaki na kichwa tuHayakuondolewa yalisogezwa mbele baada ya gaidi kuomba alambe asali
Muda utaongeaMisukule ya mwendazake mna akili finyu mno
Kivipi ?Atafute nchi ya kwenda bongo hapamfai
Lakini Samia siyo Sukuma gangHata Samia aliteuliwa na Jiwe tena mchana kweupe
Mbowe anapewa visa sababu ni mtetezi wa Upinde.Tuoneshe hukumu ya gaidi tuione hapa! Mwambie makonda asiye gaidi na mbowe gaidi wakaombe visa ya USA Tuone nani mpumbavu
Huyu ni wa pili. Kuna zittokabwe mwaka uli alihukumiwa kwa uchochezi akidai Polisi wameua Wanyantuzu na baadaye akasema CAG Professor Assad katekw kumbe yuko madrassa. Akahukumiwa hivi hivi tena siku hiyo alikuwa tayari kanyoa upara.Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, ambaye amekuwa akikabiliwa mashtaka saba ikiwemo uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na kuongoza genge la uhalifu leo Aprili 05, 2023 ameachiliwa huru.
Taarifa zaidi zitakujia hapa hapa baadae.
Chanzo: Jambo TV
===
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, leo April 5, 2023 ameachiliwa huru na mahakama baada ya kufutiwa mashtaka saba yaliyokuwa yakimkabili, ikiwemo uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na kuongoza genge la uhalifu.
Mahakama imetoa uamuzi wa Lengai Ole Sabaya kulipa kiasi cha shilingi milioni 5 kama fidia kwa mwathirika na hapaswi kufanya kosa lolote la jinai kwa muda wa mwaka mmoja.
Sabaya ambaye mapema asubuhi ya leo alifika kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Moshi, kabla uamuzi wa kuachiwa haujatangazwa, kupitia Kifungu cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai namba 91 kifungu cha 1A, kesi yake ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2022 ilifanyiwa marejeo kama upande wa mshtakiwa ulivyoomba.
Mawakili upande wa Jamhuri waliiomba mahakama kubadilisha mashtaka ya Lengai Ole Sabaya kutoka kuwa ya kesi ya Uhujumu Uchumi na kufungua kesi yenye Mashtaka ya Makosa ya Jinai baada ya Lengai Ole Sabaya kuomba kufanya mazungumzo nje ya mahakama na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Ombi hilo la Sabaya lilikubaliwa na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Salome Mshasha baada ya Mawakili wa Lengai Ole Sabaya kuridhia na kufutwa kwa kesi yake namba 2 ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2022.
Baada ya kuridhia hilo, kesi mpya aliyofunguliwa Sabaya ni kesi kesi ya Jinai Namba 31/2023 ambayo ndani yake kulikuwa na mashtaka mawili mapya dhidi yake, kosa la kwanza likiwa ni kuchukua madaraka ambayo siyo yake.
Imeelezwa kuwa Lengai Ole Sabaya na wenzake, Januari 19, 2021 katika eneo la Masama Mbosho wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, bila kibali walivamia duka la Alex Evarest SwaI na kuchukua mali na kuzizuia na kujipatia kaisi cha fedha shilingi milioni 50.
Kosa la pili ni kuzuia upatikanaji wa haki ambapo Januari 19, 2021 katika maeneo tofautitofauti katika Wilaya ya Hai na Tulia jijini Arusha na maeneo tofauti ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, walikula njama za kumfanya Alex Swai kuwa ametenda kosa la kukwepa kodi.
Baada ya kusomewa mashtaka, Sabaya alikiri kufanya makosa yote hayo mawili mbele ya hakimu Salome Mshasha.