Lengai Ole Sabaya aachiwa Huru kwa sharti la kutofanya kosa la Jinai kwa kipindi cha mwaka mmoja
Sijasikia kwa muda muendelezo wa kesi ya huyu mwamba. Je alishamalizana na Mahakama au bado.
Ushauri wangu kwake kama atakuwa ameshamalizana na Mhimili huo wa haki na endapo akiwa ameachiwa basi jambo la kwanza atenge muda wa kupiga goti na kurarua mavazi yake kujutia dhambi alizotendea watu kwa kuwaonea sababu ya kiburi cha madaraka na nguvu ya dola.
Binafsi sina uhakika kama alidhulumu au alinyanyasa watu lakini kwa yanayosemwa na kulalamikiwa juu yake YANAFIKIRISHA SANA. Kuna dhambi itaendelea kumtafuna sana hasa wale ambao waneshaondoka na yeye hakupata nafasi ya kuwaomba msamaha.

Japo najua Wamasai wengi huwa hawana majuto hata kama kamdhulumu mtu au kaua. Yeye majuto yake ni kuhusu ng'ombe wake tu
 
Aliachiwa yupo huru, ila sijui ndio anajificha ndani..
Amshukuru Mungu kwa hatua hiyo, pia nashauri Serikali isije kumpa kazi yoyote ile(hafai), na Chama/ccm isimfikirie kwa lolote lile yaani hata kazi ya kupiga mihuri au ukarani haimfai kabisa. Kuna mengi aliyoyafanya ambayo hayakuelezwa. Kifupi tu HUYU KIJANA NI LAANA.

Kama ni cheo cha Kiburi na ukatili basi huyu Kijana cheo chake ni AFISA MWANDAMIZI
 
Back
Top Bottom