Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Huko hakuna hayo yalioko nikuwa wakubwa wa kiccm hawataki kusikia madai ya katiba mpya na ndicho alichokamatiwa yeye hayo mengine nikunogeshana tu hapo lumumba ili kuaminishwa hayo.



Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app

Kumbuka utetezi wa Sabaya kwenye kesi yake...ikitokea madai ya Sabaya akiwa kiongozi wa umma hapo tutawalaumu Lumumba....?
 
Huu mchezo umekaa kimkakati sana.

Bado naamini jamaa atatoka.

Kuna watu wanabeba credit for now. ! Tukisahau atarudi mtaani soon.
 
Take a note from this post/thread, hukumu hii kuna kitu inataka kuhalalisha. Watamfunga Mbowe!
Then baadaye Sabaya will be pardoned!
Sidhani. Hakuna kesi ya maana dhidi yake. Ungeniambia nibashiri probability ya Mbowe kufungwa, ningesema ni chini ya 5%. Mimi naamini wanataka kum manage tu ili wenye nchi watawale bila "kelele" za wapinzani. Makesi tu hayo yatachukua muda.

Well, hii nchi haiishi vituko. Ngoja tusubiri.
 
Kubalansi wote Kuachiwa imeshindikana hivyo balansi inayofanyika sasa ni Wote kwenda Jela ili Jumuiya ya Kimataifa ione kuna Haki na hakuna anayeonewa Tanzania.
Hakuna kitu kama hicho, mmepigwa za uso na lijambazi lenu.
 
Shenzi kabisa haki ipo wapi hapo, mtu alikuwa anapokea maelezo kutoka juu una muhukumu vipi? Kwa hiyo JPM angekuwa hai angehukumiwa?
Anapokea maelekezo kutoka juu kwa Mungu? Hakuna aliye juu ya sheria.wewe unaambiwa ukachukuwe fedha za watu kwanguvu unaenda kama mbumbumbu .haya si alisema makamu wa Rais na Mama samia walikua wanajua wako wapi sasa mbona wasimsaidie? Huyo bwanamdogo ni ulimbukeni wake na tamaa ya mali za harakaharaka vimemponza.
 
Utaambiwa hata kwa Sabaya busara ilitamalaki ndio maana akapigwa 30yrs baadala ya 90yrs au kunyongwa mpaka kufa.... utaambiwa mwenye uwezo wa kusema una hatia au huna ni mahakama si vinginevyo, ukitaka kuipinga mahakama kata rufaa...

Uliona pale kwenye "uamuzi ni wao?"

Uamuzi si lazima uwe wa haki au siyo?

Sisi tunasubiri kama wao wanavyosubiri kila mmoja akiwa entitled to one's opinion au vipi?

Kuna taabu hapo?
 
Makengeza is next!
 
Mbaya Zaidi Sabaya anakwenda kuwa shahidi..
 
Wote mnaofurahia msiombe siku moja ukaenda mahakamani na ujua kabisa ukweli huna kosa ila ukaenda na maji ...

Duniani hakuna mahakama ni upumbavu mtupu hakuna cha mahakama wala nini ni ujinga + ujinga ...

Sibirini ya Mbowe ndio mtajua hamjui
Kama hutendi uovu, na haupendi uovu Hilo halita kukuta labda ubambikiwe kama aliyebambikiwa ugaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…