Tulia wewe, dogo kaiambia mahakama kwamba alikuwa anatumwa na Jambazi Mkuu kutenda hayo!! Kweli mambo sasa ni hadharani.Kwani gaidi nae wamemlainisha?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tulia wewe, dogo kaiambia mahakama kwamba alikuwa anatumwa na Jambazi Mkuu kutenda hayo!! Kweli mambo sasa ni hadharani.Kwani gaidi nae wamemlainisha?
Hata Ikisomwa wiki nzima bora apate kifungo cha miaka 30 jela
Lengai alipaswa aje Dkt Magufuli amtetee lakini hayupo, kesi imepindishwa ili afungwe, hilo litatokea pia kwa Mbowe. Tena Mbowe atafungwa maisha.Mle hqmna kesi...PGO yenyewe tu imewaumbua..
Unapataje legal right wakati hukufuata utaratibu wa ukamataji na haki ya uliyemkamata.
Sheria naanzia pale police anapokwambia upo chini ya ulinzi kwa kutumia PGO na si anavyoona yeye inafaa
Kwa ushahidi upi? PGO ipi? Ushahidi wa kuwafunga pingu kuwatesa kuwapiga watu ?Bado mbowe nae mvua 30
Kwa ushahidi ule wa Kingai mzee wa PGO hakuna kesi pale .poleni sanaNa mbowe akilimwa miaka muunge mkono hivihivi, msipige kelele
Kwahiyo magufuli alikuwa anatetea majambazi?Lengai alipaswa aje Dkt Magufuli amtetee lakini hayupo, kesi imepindishwa ili afungwe, hilo litatokea pia kwa Mbowe. Tena Mbowe atafungwa maisha.
Mahakama imejiridhisha pasi na shaka kwamba hata huyo jiwe hakuwa na mamlaka ya kuagiza watu wateswe...waporwe mali .Lengai alipaswa aje Dkt Magufuli amtetee lakini hayupo, kesi imepindishwa ili afungwe, hilo litatokea pia kwa Mbowe. Tena Mbowe atafungwa maisha.
Wanajukwaa poleni kwa kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa Taifa letu,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Bila shaka baada ya Hukumu ya Lengai Ole Sabaya kuhairishwa tarehe 1/10/2021 ilipangwa kwamba itatolewa leo. Hivyo tuelekeze masikio yetu katika viunga vya mahakama.
=======
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili leo Ijumaa Oktoba 15, 2021 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusikiliza hukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Amalia Mushi aliahirisha hukumu hiyo Oktoba Mosi, 2021 baada ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, kutokamilisha kuandika hukumu hiyo.
Agosti 24 mwaka huu, Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura walikamilisha kujitetea mahakamani hapo baada ya Jamhuri kukamilisha mashahidi 11 na vielelezo vinane.
Sabaya alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 4, mwaka huu baada ya kukamatwa Mei 27 wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Chanzo: Mwananchi
UPDATE: MAHAKAMA YAMKUTA NA HATIA OLE SABAYA
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imemkuta na hatia Lengai Ole Sabaya na wenzake katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha.
Mahakama ilimpatia nafasi Ole Sabaya ajitetee(Shufaa) kwanini asipewe adhabu kali naye aliiomba Mahakama imuonee huruma kwani si yeye bali alikuwa anatekeleza amri ya mamlaka ya uteuzi, pia ameomba mahakama imuonee huruma kwani ana mchumba anayetegemea kufunga naye ndoa na mahari ameshalipa.
UPDATE: SABAYA NA WENZAKE MIAKA 30 JELA
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wamehukumia na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.
WASIFU WA OLE SABAYA
Lengai Ole Sabaya amezaliwa 26/12/1986 mkoani Arusha. Amesoma Shahada ya Sayansi katika Elimu Chuo Kikuu cha Mtakatifu John Dodoma (St. John University).
Ole Sabaya aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) Mkoa wa Arusha na pia aliwahi kushika wadhifa wa Udiwani katika kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha Mjini mwaka 2015.
Ole Sabaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro tarehe 28 Julai 2018 ya aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano, Hayati John Pombe Magufuli.
Sabaya alitenguliwa nafasi hiyo ya ukuu wa Wilaya ya Hai tarehe 13 Mei 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan ili kupisha uchunguzi wa makosa yaliyokuwa yakimkabili ikiwemo unyang’anyi wa kutumia silaha. Tarehe 15 Oktoba 2021 Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha imemhukumu Sabaya na wenzake kifungo cha miaka 30 jela.
Kesi ya mbowe haifanani na ya Sabaya ambayo ilikuwa na ushahidi wa kweli na wazi, kesi ya mbowe ni kesi ya kubambikiwa hata walinzi wa mbowe wametendewa ukatili mkubwa na Polisiccm akina mahita kingai, mbowe hawezi kufungwa hakuna ushahidi wa kuweza kumfungaLengai alipaswa aje Dkt Magufuli amtetee lakini hayupo, kesi imepindishwa ili afungwe, hilo litatokea pia kwa Mbowe. Tena Mbowe atafungwa maisha.
LELA VIHI - LET IT BE.Take a note from this post/thread, hukumu hii kuna kitu inataka kuhalalisha. Watamfunga Mbowe!
Then baadaye Sabaya will be pardoned!
Acha TuLaiti angesikiliza maneno ya lema,ambapo MUNGU alimuonya sabaya kupitia kwa lema angelipona
Haiwezekani kwa ushahidi upi?Mbowe soon tuu
Kafungwa miaka 7 au 30?Laana ya mama Anna Mghwira inamuandama huyu dogo. Miaka 7 jela + 34 aliyonayo atatoka akili zimekaa sawa.