Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Hakuna kesi pale.

Sabaya alipaswa kushtakiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka na wenzake wangekuwa ndio mashahidi.

Ataachiwa huru mchana kweupe!

Mtabiri uchwara....haya wikiend hii kampelekee sabuni na mswaki huyo fala mwenzako gerezani huko!!!
 
Dah nimemuonea huruma nita mtembelea nita msaidia kumpa mchumba wake matumizi
 
Mungu yupo kazini kwakuwa yamekukuta? Wakati mnapowaonea wengine shetani anakuwa zamu sio?
 
Namtakia kila la heri katika maisha yake mapya aliyo jichagulia. Natambua fika usiku wa leo kwake utakuwa kama ndoto vile, lakini ndiyo hivyo tena.

Ndani ya wiki hii ataanza kushindia zile nguo za rangi ya machungwa! Na siyo suti tena za Mheshimiwa DC wa Hai.
 
Yesu pekee ndiye Rafiki wa kweli!

..CCM inajivunia kuwa na rasilimali watu.

..sasa imeshindwa vipi kumtafutia ahueni kada wake?

..Sabaya sio mtu wa kupewa hukumu mbaya-mbaya utadhani ni mpinzani nchi hii.

..CCM imetumia Sabaya na kumtupa kama kondom.
 
Kwan amekamatwa kwa ushahidi upi
Kukamatwa kienyeji na Polisiccm ni tofauti na ushahidi mahakamani kule mahakamani Polisiccm wameumbuka sana hawajui PGO walitumia Mbinu katili kuwatesa watuhumiwa kinyume cha Sheria
 
Usilitaje jina la Mungu wako hovyo! Mungu hajawahi kuwa kazini na kamwe haitatokea awe kazini! Mungu ni mkamilifu na ni mwema!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…