Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

wanasheria tunaomba ufafanuzi hapa kuna wengine wanasema hukumu ni jumla ya miaka 30 hivyo inagawanywa kwa watu 4 kila mmoja mika 7, wengne wanasema kila mmoja miaka 30 kwasababu miaka haigawanyiki

hivyo ukweli ni upi
nenda wenye penal code . Hakuna kitu kinaitwa kugawana miaka..........

Azam TV

September 13, 2019 ·

JELA MIAKA 30 KWA UNYANG'ANYI WA KUTUMIA SILAHA: Mahakama ya Hakimu mkazi Tabora imewahukumu kwenda jela miaka 30 kila mmoja washtakiwa watano baada ya kupatikana na hatia ya unyang'anyi wa kutumia silaha wanalodaiwa kulifanya huko wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mahakama ya Hakimu mkazi Tabora, Saraphin Nsana alisema mahakama imepitia maelezo ya pande zote mbili na kujiridhisha pasi na shaka kuwa washtakiwa Hamisi Yusuph na wenzake wanne walitenda tukio la unyang'anyi wa kutumia silaha ambapo walivamia nyumbani kwa Ally Hamad Ludabaza huko Tutuo Madukani wakiwa na bunduki aina ya Shotgun walipora kiasi cha shilingi milioni 28, Oktoba 10 majira ya usiku.



episode two

ELA MIAKA 30 KWA UNYANG'ANYI WA KUTUMIA SILAHA​

VENANCE BLOG December 27, 2013 Kitaifa,



Wakazi wawili wa vijiji vya Nyabisaga Kata ya Pemba wilayani Tarime mkoani Mara, Mhoni Chacha Ng’wena (25) na Isack Magawi Meng’anyi (30), wamehukumiwa kwenda jela miaka 30 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya unyang’anyi wa kutumia silaha. Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama ya Wilaya ya Tarime.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Tarime, Adrian Kilimi alisema ameridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka, ukiongozwa na Inspekta Usu, George Lutonja kwamba washitakiwa walitenda kosa la unyang’anyi wa silaha.Alisema Mahakama imeridhika na ushahidi, ulioambatana na vielelezo vya mlalamikaji, vilivyokamatwa kwa watuhumiwa hao, vikiwemo baiskeli, simu ya mkononi, viatu na tochi.
Awali, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Usu Lutonja alidai kuwa washitakiwa hao pamoja Januari 3, mwaka huu saa 12 alfajiri, wakiwa na silaha za jadi za mapanga na marungu walivamia na kuingia ndani ya nyumba ya Selestin Omahe, mkazi wa Sirari na kumshambulia na familia yake na kupora vitu vya ndani, vikiwemo baiskeli aina ya Phoenix, simu ya mkononi, viatu na tochi, vyote vyenye thamani ya Sh 284,000.Alidai baada ya tukio hilo, mlalamikaji Omahe alipiga yowe, kuomba msaada na majirani, ambao walitokea pamoja na polisi, waliokuwa doria eneo hilo. Hata hivyo, hawakufanikiwa kukamata washitakiwa hao wakiwa na mali za mlalamikaji.
Baada ya kukamatwa, washitakiwa walifikishwa kwenye vyombo vya sheria, ambapo upande wa mashitaka ulileta mashahidi wanne na vielelezo, vilivyokamatwa kwa washitakiwa wakati wa tukio hilo. Washitakiwa hao waliomba wasamehewe. Mwendesha Mashitaka aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa washitakiwa. Hakimu Kilimi alisema anawahukumu kwenda jela miaka 30 kila mmoja ili iwe fundisho kwa watu wenye tamaa ya kupora mali za watu.
 
Kuna mkanganyiko gani hapo?

Zero mlizopata shule zinawaandama mpka mtaani!
zero zinauhisiano gan na swali mkuu wewe uliopata one unahela umemfikia hata mo biriani lete fact usilete mipash**o
 
Aliyekuwa Dc wa Hai Ole Sabaya baada ya kuhukumiwa amewatoa wasiwasi wafuasi wake kwa kuwapa kauli ya kiroho , Amesema hivi , Nanukuu , MSIJALI MAANA MUNGU YUKO KAZINI , Mwisho wa kunukuu .

Chanzo : Mwananchi

Nachukua nafasi hii mimi binafsi kuipa pole sana familia ya Ole Sabaya kwa shida iliyotokea kutokana na hukumu aliyopewa kijana wao .

Mtu mpaka kazimia.huo ujasiri wa kusema hivyo kautoa wapi ?.
 
wanasheria tunaomba ufafanuzi hapa kuna wengine wanasema hukumu ni jumla ya miaka 30 hivyo inagawanywa kwa watu 4 kila mmoja mika 7, wengne wanasema kila mmoja miaka 30 kwasababu miaka haigawanyiki

hivyo ukweli ni upi
Kwani Hakimu alisemaje?

Maana seems ulipokuwa darasani ulikuwa unamsikiliza mwalimu mwanzo mwisho na akiuliza mmelewa unaongoza kwaya ya kusema ndiyooo..
Akitoa assignment unaanza kuulizia kwa watoro wenzako kuwa mwalimu alifundisha topic gani leo?
 
Aliyekuwa Dc wa Hai Ole Sabaya baada ya kuhukumiwa amewatoa wasiwasi wafuasi wake kwa kuwapa kauli ya kiroho , Amesema hivi , Nanukuu , MSIJALI MAANA MUNGU YUKO KAZINI , Mwisho wa kunukuu .

Chanzo : Mwananchi

Nachukua nafasi hii mimi binafsi kuipa pole sana familia ya Ole Sabaya kwa shida iliyotokea kutokana na hukumu aliyopewa kijana wao .
Familia ilidha wahi kuwaomba radhi walio umizwa na jambazi Sabaya?
Malipo ni hapa hapa duniani..
 
Wakati anatekeleza nmaagizo kutoka mamlaka zilizomteua hakua anajua kua MUNGU YUOPO KAZINI?
 
Aliyekuwa Dc wa Hai Ole Sabaya baada ya kuhukumiwa amewatoa wasiwasi wafuasi wake kwa kuwapa kauli ya kiroho , Amesema hivi , Nanukuu , MSIJALI MAANA MUNGU YUKO KAZINI , Mwisho wa kunukuu .

Chanzo : Mwananchi

Nachukua nafasi hii mimi binafsi kuipa pole sana familia ya Ole Sabaya kwa shida iliyotokea kutokana na hukumu aliyopewa kijana wao .
Daima tunavuna tunachokipanda
 
Sabaya bado kuna wale aliowaumiza lakini hawakwenda mahakamani. Nashauri watu hao waonane na kwenda kukazia hukumu ya leo kwenye Mahakama ya kimila.
 
mungu wetu amtangulie Sabaya ameonewa Sana najua watu wabaya wameamua kumsingizingizia hiyo kesi,
Baba yetu kipenzi umetuacha yatima Leo tunanyanyasika😥😥😥
mungu Bora urudi tu mashetani yameshika mpini makali kwetu ila yote yatapita tu!😥😥😥

(Alisikika Msukule wa Sir Buyer Toka LUMUMBA)

mungu = mweshimiwa mungu
(in Prof majalala voices)
yaani mungumtu aliyelala chattle Mabatini kwasasa pamekua hekaluni MATAGA na S. Gang tutaendaga kuhiji Kila tukimkumbuka Mwendakuzimu!
 
Hukumu ya kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya inasomwa muda huu katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Akisoma maelezo ya awali Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Odira Amworo amesema kati ya mashahidi 11 wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi wao, ambapo ushahidi wa watu 9 umeonekana una mashiko na ushahidi wa watu wawili umetupwa.

Hakimu Amworo amesema kuwa mahakama imejiridhisha kuwa siku ya tukio February 9 mwaka 2021 washtakiwa wote watatu walikua dukani kwa Saad na wote walishiriki kufanya unyang'anyi wa kutumia silaha, kabla ya kumpiga Saad na kumsabanishia majeraha, wakitaka wapewe TZS 100M au mfanyabiashara huyo apewe kesi ya uhujumu uchumi.

Hakimu anasema kwa mujibu wa kifungu cha 201 cha sheria ya makosa ya adhabu, mtu yeyote anayepatikana na hatia ya kutumia silaha kunyang'anya mali ya mtu mwingine, adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela pamoja na viboko 12 au miaka 30 bila viboko.

Baada ya kusema hayo Sabaya alianguka na kudaiwa kuzimia, hali iliyofanya Hakimu kuahirisha kusoma hukumu hiyo kwa dakika 5. Baadae Sabaya alizinduka na hukumu ikaendelea kusomwa.

Kabla hajataja adhabu, Hakimu amewapa washtakiwa nafasi kujitetea kwa mara ya mwisho, ambapo Sabaya ameomba apunguziwe adhabu kwa sababu anaye mchumba ambaye ameshamtolea mahari na hivyo akihukumiwa miaka mingi atashindwa kumuoa.

Hukumu inaendelea kusomwa. Letz keep waiting.!View attachment 1975366

IMG-20211015-WA0093.jpg


IMG-20211015-WA0073.jpg
 
Back
Top Bottom