Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Ana wakati mgumu sana hili tukio limemkuta ghafla hakutegemea, alijua atalindwa na mamlaka mpaka mwisho wa safari kumbe hakuwa akilindwa na mamlaka bali alikuwa akilindwa na mtu mmoja ambae kwa sasa ni marehemu, amejikuta yuko peke yake mahakamani asijue la kujitetea ndio maana ameongea vitu vinavyoonekana vya ajabu.
Angeliyajua mapema angetoroka nchi maana alikua na madolali ya kutosha.
 
Aliyekuwa Dc wa Hai Ole Sabaya baada ya kuhukumiwa amewatoa wasiwasi wafuasi wake kwa kuwapa kauli ya kiroho , Amesema hivi , Nanukuu , MSIJALI MAANA MUNGU YUKO KAZINI , Mwisho wa kunukuu .

Chanzo : Mwananchi

Nachukua nafasi hii mimi binafsi kuipa pole sana familia ya Ole Sabaya kwa shida iliyotokea kutokana na hukumu aliyopewa kijana wao .
Leo kwa mara ya kwanza umetoa pole kwa ccm
 
15 October 2051
IMG-20211015-WA0014.jpg
 
Wanajukwaa poleni kwa kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa Taifa letu,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Bila shaka baada ya Hukumu ya Lengai Ole Sabaya kuhairishwa tarehe 1/10/2021 ilipangwa kwamba itatolewa leo. Hivyo tuelekeze masikio yetu katika viunga vya mahakama.

=======

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili leo Ijumaa Oktoba 15, 2021 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusikiliza hukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Amalia Mushi aliahirisha hukumu hiyo Oktoba Mosi, 2021 baada ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, kutokamilisha kuandika hukumu hiyo.

Agosti 24 mwaka huu, Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura walikamilisha kujitetea mahakamani hapo baada ya Jamhuri kukamilisha mashahidi 11 na vielelezo vinane.

Sabaya alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 4, mwaka huu baada ya kukamatwa Mei 27 wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Chanzo: Mwananchi

UPDATE: MAHAKAMA YAMKUTA NA HATIA OLE SABAYA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imemkuta na hatia Lengai Ole Sabaya na wenzake katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha.

Mahakama ilimpatia nafasi Ole Sabaya ajitetee(Shufaa) kwanini asipewe adhabu kali naye aliiomba Mahakama imuonee huruma kwani si yeye bali alikuwa anatekeleza amri ya mamlaka ya uteuzi, pia ameomba mahakama imuonee huruma kwani ana mchumba anayetegemea kufunga naye ndoa na mahari ameshalipa.

UPDATE: SABAYA NA WENZAKE MIAKA 30 JELA

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wamehukumia na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.

WASIFU WA OLE SABAYA

Lengai Ole Sabaya amezaliwa 26/12/1986 mkoani Arusha. Amesoma Shahada ya Sayansi katika Elimu Chuo Kikuu cha Mtakatifu John Dodoma (St. John University).

Ole Sabaya aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) Mkoa wa Arusha na pia aliwahi kushika wadhifa wa Udiwani katika kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha Mjini mwaka 2015.

Ole Sabaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro tarehe 28 Julai 2018 ya aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano, Hayati John Pombe Magufuli.

Sabaya alitenguliwa nafasi hiyo ya ukuu wa Wilaya ya Hai tarehe 13 Mei 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan ili kupisha uchunguzi wa makosa yaliyokuwa yakimkabili ikiwemo unyang’anyi wa kutumia silaha. Tarehe 15 Oktoba 2021 Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha imemhukumu Sabaya na wenzake kifungo cha miaka 30 jela.

Mnashangalia hukumu ya Sabaya Leo; lakini atakata rufaa na tusubiri matokeo !

FB_IMG_1634320832095.jpg


FB_IMG_1634321240558.jpg
 
Tupia snap ya demu yake Sabaya itanoga
mbona picha ya dem wake tiyar ishatupiwa humu, angalia kwenye thread ya 30 hadi 35 zimetupiwa nyingi tu, demu lina shep nzr, sura nzr, na dimpoz afu dem amepanda ameenda hewani yaonesha ni mnyarwanda maana ana figa ya kinyarwanda.

Huyu demu tiyari wajuba washamweka kune mahesabu yao. Huyu halazi siku anachukuliwa. Hata jamaa yake alivojitetea vile, tiyari alishajua hana chake pale.
 
Mi nasubiri hukumu ya mbowe [emoji28][emoji28], kulia kupokezana [emoji28][emoji28]...
 
Kwenye rufaa pia ni ngumu kuchomoka labda wale wenzake wawili
 
Makonda alinyanganya nani ela?kama sio Chuki binafsi kwa Makonda;

..kuna watu wanadai Bashite alikuwa na genge la kulawiti watu waliokuwa wakitekwa.

..kwa hiyo wale victims wake akiwaachia wanatunza siri hawaripoti popote.

..Sabaya naye angekuwa na genge kama la Bashite huenda mashahidi wasingekuwa tayari kueleza kilichowatokea.

..Na kosa lingine la Sabaya lilikuwa kutumia magari yenye namba za UMOJA WA MATAIFA / UN wakati akifanya uhuni.

..Sasa hali hiyo inalitoa suala lake toka ndani ya nchi na kulipeleka ktk viunga vya UN. Alikuwa akiichafua serikali kwa washirika wake wa nje. Hivyo ni vigumu kumlinda mtu wa namna hiyo.
 
Nitafungua kesi mpya dhidi ya sabaya kwa aliyofanya kwenye bustani yetu Sanya.
 
Mnashangalia hukumu ya Sabaya Leo; lakini atakata rufaa na tusubiri matokeo !

View attachment 1975626

View attachment 1975628
misekule hamkosekani huyo ndio basi Tena warangi tunasema Yasilile
Na sisi wahehe tunasema vile vile
Yasilile
Wabena tunasema vile vile
Yasilile

Yaaani yasilile Mwana agwilie mu liganga pufuuuuuu!

Gakusemwa ago mnyalukolo!

Wahaya tunasema Acholile mwana Acholile
Hiiiiiiii bha goshaaaaa!
😁😁😁😁
 
Back
Top Bottom