Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Hukumu ya kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya inasomwa muda huu katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Akisoma maelezo ya awali Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Odira Amworo amesema kati ya mashahidi 11 wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi wao, ambapo ushahidi wa watu 9 umeonekana una mashiko na ushahidi wa watu wawili umetupwa.

Hakimu Amworo amesema kuwa mahakama imejiridhisha kuwa siku ya tukio February 9 mwaka 2021 washtakiwa wote watatu walikua dukani kwa Saad na wote walishiriki kufanya unyang'anyi wa kutumia silaha, kabla ya kumpiga Saad na kumsabanishia majeraha, wakitaka wapewe TZS 100M au mfanyabiashara huyo apewe kesi ya uhujumu uchumi.

Hakimu anasema kwa mujibu wa kifungu cha 201 cha sheria ya makosa ya adhabu, mtu yeyote anayepatikana na hatia ya kutumia silaha kunyang'anya mali ya mtu mwingine, adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela pamoja na viboko 12 au miaka 30 bila viboko.

Baada ya kusema hayo Sabaya alianguka na kudaiwa kuzimia, hali iliyofanya Hakimu kuahirisha kusoma hukumu hiyo kwa dakika 5. Baadae Sabaya alizinduka na hukumu ikaendelea kusomwa.

Kabla hajataja adhabu, Hakimu amewapa washtakiwa nafasi kujitetea kwa mara ya mwisho, ambapo Sabaya ameomba apunguziwe adhabu kwa sababu anaye mchumba ambaye ameshamtolea mahari na hivyo akihukumiwa miaka mingi atashindwa kumuoa.

Hukumu inaendelea kusomwa. Letz keep waiting.!View attachment 1975366
Daah! From DC to Prisoner,
Hapa ndipo dreams zinapopoteana!

Tutende haki jamani, uongozi Ni dhamana
 
Mahita rafiki yake mkubwa waliokuwa wakishirikiana kuwatesa chadema huko Kilimanjaro ameshikwa na simanzi kubwa na sasa yupo mbioni kusuka Mipango Sabaya atolewe jela akajifiche msumbiji
Mbinu zozote ovu, zifichuliwe Kwa maslahi mapana ya Taifa pendwa Tanzania, Kwa taifa hili ni la Wantanzania wote.
 
Mahita rafiki yake mkubwa waliokuwa wakishirikiana kuwatesa chadema huko Kilimanjaro ameshikwa na simanzi kubwa na sasa yupo mbioni kusuka Mipango Sabaya atolewe jela akajifiche msumbiji
Mahakama imetenda haki ee?
 
Aliyekuwa mkuu wa hai ole lengai sabaya na wenzake wamehukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Minne inatosha
 
Kesi inakoelemea si kunaonekana mkuu.

Kesi ya Mbowe inafuatiliwa. Kwamba Jaji kapandishwa cheo akielekea kutoa hukumu ya pingamizi 19/10, nani asiyejua?

Kwamba mawaidha ya Jaji mkuu kwa majaji ni kutoa hukumu zenye kuzingatia mwelekeo wa serikali, nani hakusikia?

Nani alisema nini mahakamani nini kisichojulikana?

Patiently yetu ni subira. 19/10 kwani ni mbali?

Kwani kimya kingi kiliacha kuwa na mshindo mkuu?
Kuna kitu kibaya kinakuja............... CJ ana maelekezo kamili...
 
Mungu amjalie mh hakimu kwa kutenda haki. Sabaya hata Lumumba mumteeje alikwa na roho ya shetani hata kama alikuwa anatumwa alitakiwa achanganye na za kwake.
Sasa tusisikie mahakama haitendi haki kwa gaidi
 
Take a note from this post/thread, hukumu hii kuna kitu inataka kuhalalisha. Watamfunga Mbowe!
Then baadaye Sabaya will be pardoned!

Mkuu usikonde. Mungu ni mwema. Nini hakionekani? Mahakamani ni mahali pa wazi:

"Kesi inakoelemea si kunaonekana mkuu?

Kesi ya Mbowe inafuatiliwa. Kwamba Jaji kapandishwa cheo akielekea kutoa hukumu ya pingamizi 19/10, nani asiyejua?

Kwamba mawaidha ya Jaji mkuu kwa majaji ni kutoa hukumu zenye kuzingatia mwelekeo wa serikali, nani hakusikia?

Nani alisema nini mahakamani, nini kisichojulikana?

Painstakingly, yetu ni subira. 19/10 kwani ni mbali?

Kwani kimya kingi kiliacha kuwa na mshindo mkuu?"
 
Tupatieni jina na number ya mchumba wake tutamtunzia ili akitoka tumkabidhi.

Pole yake, 30 si mchezo ..ukisikia kuulia ujana wote jela ndiko huku.
 
Kiturilo asubiri kesi anayoshadadia aone inavyogeukia Kwa wale wa PGO. Na mwisho nao wale mvua za kuwatosha.
Mbowe hafungwi hakuna ugaidi wowote kafanya
Kwa hiyo kwa sabaya mahakama inatenda haki ila kwa mbowe anaonewa?
 
Hukumu ya kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya inasomwa muda huu katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Akisoma maelezo ya awali Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Odira Amworo amesema kati ya mashahidi 11 wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi wao, ambapo ushahidi wa watu 9 umeonekana una mashiko na ushahidi wa watu wawili umetupwa.

Hakimu Amworo amesema kuwa mahakama imejiridhisha kuwa siku ya tukio February 9 mwaka 2021 washtakiwa wote watatu walikua dukani kwa Saad na wote walishiriki kufanya unyang'anyi wa kutumia silaha, kabla ya kumpiga Saad na kumsabanishia majeraha, wakitaka wapewe TZS 100M au mfanyabiashara huyo apewe kesi ya uhujumu uchumi.

Hakimu anasema kwa mujibu wa kifungu cha 201 cha sheria ya makosa ya adhabu, mtu yeyote anayepatikana na hatia ya kutumia silaha kunyang'anya mali ya mtu mwingine, adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela pamoja na viboko 12 au miaka 30 bila viboko.

Baada ya kusema hayo Sabaya alianguka na kudaiwa kuzimia, hali iliyofanya Hakimu kuahirisha kusoma hukumu hiyo kwa dakika 5. Baadae Sabaya alizinduka na hukumu ikaendelea kusomwa.

Kabla hajataja adhabu, Hakimu amewapa washtakiwa nafasi kujitetea kwa mara ya mwisho, ambapo Sabaya ameomba apunguziwe adhabu kwa sababu anaye mchumba ambaye ameshamtolea mahari na hivyo akihukumiwa miaka mingi atashindwa kumuoa.

Hukumu inaendelea kusomwa. Letz keep waiting.!View attachment 1975366
Huyo boya heri yeye anamchumba,aliowaibia kinguvu wana wake,watoto...yeye mchumba tu analialia
 
Back
Top Bottom