Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata hivyo kesi ya msingi SI Bado? Wewe unasemea maamuzi ya kesi ndogo. Ngoma yenyewe Bado!Mkuu usikonde. Mungu ni mwema. Nini hakionekani? Mahakamani ni mahali pa wazi:
"Kesi inakoelemea si kunaonekana mkuu?
Kesi ya Mbowe inafuatiliwa. Kwamba Jaji kapandishwa cheo akielekea kutoa hukumu ya pingamizi 19/10, nani asiyejua?
Kwamba mawaidha ya Jaji mkuu kwa majaji ni kutoa hukumu zenye kuzingatia mwelekeo wa serikali, nani hakusikia?
Nani alisema nini mahakamani, nini kisichojulikana?
Painstakingly, yetu ni subira. 19/10 kwani ni mbali?
Kwani kimya kingi kiliacha kuwa na mshindo mkuu?"
Wanajukwaa poleni kwa kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa Taifa letu,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Bila shaka baada ya Hukumu ya Lengai Ole Sabaya kuhairishwa tarehe 1/10/2021 ilipangwa kwamba itatolewa leo. Hivyo tuelekeze masikio yetu katika viunga vya mahakama.
=======
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili leo Ijumaa Oktoba 15, 2021 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusikiliza hukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Amalia Mushi aliahirisha hukumu hiyo Oktoba Mosi, 2021 baada ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, kutokamilisha kuandika hukumu hiyo.
Agosti 24 mwaka huu, Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura walikamilisha kujitetea mahakamani hapo baada ya Jamhuri kukamilisha mashahidi 11 na vielelezo vinane.
Sabaya alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 4, mwaka huu baada ya kukamatwa Mei 27 wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Chanzo: Mwananchi
UPDATE: MAHAKAMA YAMKUTA NA HATIA OLE SABAYA
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imemkuta na hatia Lengai Ole Sabaya na wenzake katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha.
Mahakama ilimpatia nafasi Ole Sabaya ajitetee(Shufaa) kwanini asipewe adhabu kali naye aliiomba Mahakama imuonee huruma kwani si yeye bali alikuwa anatekeleza amri ya mamlaka ya uteuzi, pia ameomba mahakama imuonee huruma kwani ana mchumba anayetegemea kufunga naye ndoa na mahari ameshalipa.
UPDATE: SABAYA NA WENZAKE MIAKA 30 JELA
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wamehukumia na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.
WASIFU WA OLE SABAYA
Lengai Ole Sabaya amezaliwa 26/12/1986 mkoani Arusha. Amesoma Shahada ya Sayansi katika Elimu Chuo Kikuu cha Mtakatifu John Dodoma (St. John University).
Ole Sabaya aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) Mkoa wa Arusha na pia aliwahi kushika wadhifa wa Udiwani katika kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha Mjini mwaka 2015.
Ole Sabaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro tarehe 28 Julai 2018 ya aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano, Hayati John Pombe Magufuli.
Sabaya alitenguliwa nafasi hiyo ya ukuu wa Wilaya ya Hai tarehe 13 Mei 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan ili kupisha uchunguzi wa makosa yaliyokuwa yakimkabili ikiwemo unyang’anyi wa kutumia silaha. Tarehe 15 Oktoba 2021 Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha imemhukumu Sabaya na wenzake kifungo cha miaka 30 jela.
Ndo hivyo ashakuwa mali ya serikaliNaomba kuuliza, kuanzia leo ndo atavaa zile nguo za wafungwa? Na atapangiwa jela kama wafungwa wengine?
Mwenye picha ya mchumba wa sabaya alete basi, na namba kama ipo tumpe pole.
Hauna namba yakeView attachment 1975428
Huyo hapo
Kwa sheria gani bwashee?!
Walinzi wa mbowe walikuwa wageni hawajui chochote wakaenda kuwakamata kienyeji bila RB wala PGO haikufuatwa na kibaya zaidi wakawafunga pingu saa 24 kila siku huku wakiwatesa kuwapiga kuwalazimisha wakubali ugaidi hewa ugaidi feki ugaidi ambao haukuwepo na haujawahi kuwepo, uonevu mkubwa sana ikiwemo kuwaua Moses lejenje na LT Urio ambao hawakuwa magaidi na hawajui chochote juu ya ugaidi, hakuna kitu kibaya alikifanya magufuli kama hiki hapa Duniani, watesaji wa mbowe na walinzi wake wana pressure kubwa endapo mbowe ataachiwa huru kwani wanahofia laana za ndugu jamaa marafiki na Alibadiri za wapenda haki kote TanzaniaMle hqmna kesi...PGO yenyewe tu imewaumbua..
Unapataje legal right wakati hukufuata utaratibu wa ukamataji na haki ya uliyemkamata.
Sheria naanzia pale police anapokwambia upo chini ya ulinzi kwa kutumia PGO na si anavyoona yeye inafaa