Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Aliyekuwa Dc wa Hai Ole Sabaya baada ya kuhukumiwa amewatoa wasiwasi wafuasi wake kwa kuwapa kauli ya kiroho , Amesema hivi , Nanukuu , MSIJALI MAANA MUNGU YUKO KAZINI , Mwisho wa kunukuu .

Chanzo : Mwananchi

Nachukua nafasi hii mimi binafsi kuipa pole sana familia ya Ole Sabaya kwa shida iliyotokea kutokana na hukumu aliyopewa kijana wao .
Wakati anakaba watu na kupora pesa Nani alikuwa kazini?
 
Makonda ni mzinga wa nyuki, ukiguswa nchi haitakalika.
Mbele ya SSH Makonda ni kijana wa shamba ambaye hana lolote analoweza fanya. Makonda ana nini mpaka aogopwe? Hata ten most influential people in Tanzania hayupo wala hana maamuzi au washirika wa maana.

Kwa Tanzania hii rais ana nguvu sana ambazo hawakuwahi kuzitumia. Nyerere alikuwa alibadilisha Mkuu wa Majeshi kuwa mkuu wa Mkoa. JPM kamtoa DG wa TISS kuwa Balozi. SSH kamtoa Brig. Gen. Mbuge na kuwa Mkuu wa Mkoa, Katibu Mkuu kuwa mbunge, Waziri wa Ulinzi wa kike. Kipi anacho Bashite?
 
"nina mchumba ninatarajia kumuoa hivi karibuni na mahari nimeshalipa naomba mahakama iniachie huru..." [emoji23]
Ila jamaa limeacha demu mzr, huyu demu hawezi salimika analiwa mapema kabla hata ya mumewe kuwekwa nyuma ya nondo.
 
Kubalansi wote Kuachiwa imeshindikana hivyo balansi inayofanyika sasa ni Wote kwenda Jela ili Jumuiya ya Kimataifa ione kuna Haki na hakuna anayeonewa Tanzania.

Sioni uhusiano katika kesi ya Sabaya na Mbowe.
 
Mimi kama mwana ccm, Sabaya tulishamuonya sana hapa JF,

Siasa sio uadui, Mimi ni ccm lakini mtu wangu wa karibu hana chama kabisa

Yeye anapenda mpira sana na ni shabiki wa Timu ambayo Mimi Siipendi kabisa hapa Tanzania

Siku wakishinda Yeye na watoto wanashangilia na kunizomea week nzima mpaka pale watoto watakapo sahau ndio pona yangu

Hata ccm tukishinda wananicheka sana, Wanaona nina mawazo ya kizamani kisa kuwa ccm

Sabaya aligeuza siasa vita na ubaguzi

Sasa kama nina ndugu wengi Chadema, Act na CUF na CCM na tunaishi kwa Amani na kushirikiana

Sabaya Yeye nani?
Yaani umeiweka vizuri mno mkuu@GUSSIE. Ndugu zetu wengine wa damu kabisa wako upinzani. Marafiki na majirani ndiyo usiseme. Sasa hawa binadamu wenzetu utawachukia na kutoshiriki nao hata mambo ya kijamii? Tujue kuwa Siasa za ustaarabu Hazina uhasama. Tunajisahau Sana tunapoona wapinzani ni maadui.
 
You are very right, perfectly right, lakini kwa nchi gani? Tanzania? ya Samia? Huyu mama hana aibu..... Umesikia matamshi ya CJ juzi? Kuwa lazima mahakama ziangalie mwelekeo wa serikali! I need your comment on this!
Nakuelewa lakini ukumbuke international commumity inataka kuona haki inatendeka. They may need to impress them!
 
Wanajukwaa poleni kwa kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa Taifa letu,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Bila shaka baada ya Hukumu ya Lengai Ole Sabaya kuhairishwa tarehe 1/10/2021 ilipangwa kwamba itatolewa leo. Hivyo tuelekeze masikio yetu katika viunga vya mahakama.

=======

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili leo Ijumaa Oktoba 15, 2021 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusikiliza hukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Amalia Mushi aliahirisha hukumu hiyo Oktoba Mosi, 2021 baada ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, kutokamilisha kuandika hukumu hiyo.

Agosti 24 mwaka huu, Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura walikamilisha kujitetea mahakamani hapo baada ya Jamhuri kukamilisha mashahidi 11 na vielelezo vinane.

Sabaya alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 4, mwaka huu baada ya kukamatwa Mei 27 wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Chanzo: Mwananchi

UPDATE: MAHAKAMA YAMKUTA NA HATIA OLE SABAYA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imemkuta na hatia Lengai Ole Sabaya na wenzake katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha.

Mahakama ilimpatia nafasi Ole Sabaya ajitetee(Shufaa) kwanini asipewe adhabu kali naye aliiomba Mahakama imuonee huruma kwani si yeye bali alikuwa anatekeleza amri ya mamlaka ya uteuzi, pia ameomba mahakama imuonee huruma kwani ana mchumba anayetegemea kufunga naye ndoa na mahari ameshalipa.

UPDATE: SABAYA NA WENZAKE MIAKA 30 JELA

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wamehukumia na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.

WASIFU WA OLE SABAYA

Lengai Ole Sabaya amezaliwa 26/12/1986 mkoani Arusha. Amesoma Shahada ya Sayansi katika Elimu Chuo Kikuu cha Mtakatifu John Dodoma (St. John University).

Ole Sabaya aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) Mkoa wa Arusha na pia aliwahi kushika wadhifa wa Udiwani katika kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha Mjini mwaka 2015.

Ole Sabaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro tarehe 28 Julai 2018 ya aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano, Hayati John Pombe Magufuli.

Sabaya alitenguliwa nafasi hiyo ya ukuu wa Wilaya ya Hai tarehe 13 Mei 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan ili kupisha uchunguzi wa makosa yaliyokuwa yakimkabili ikiwemo unyang’anyi wa kutumia silaha. Tarehe 15 Oktoba 2021 Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha imemhukumu Sabaya na wenzake kifungo cha miaka 30 jela.
Nilicho funzwa na Mama mzazi ni kutokujikweza.......

Katika Umri mdogo nime wai pewa position kubwa ya maamuzi katika sehemu nayo fanyia kazi.....Nacho amin viongozi wazuri wanazaliwa na talented.....

Sio siri nimeishi Sana maisha ya Mwalimu Nyerere....

Ila sijawai kua kama Ole sabaya....Hii dunia na ardhi tuikanyage kwa heshima.....kuna muda Sabaya alijisahau na kujiona Mungu Mtu.....

Vijana tukiaminiwa katika uongozi Tujitahidi kuacha alama chanya.....
 
Hivi ile crip ya Lema wakiongea kwa simu huku Lengai akiwa amelewa mayo?iwekeni.Dogo alilewa sn
 
Back
Top Bottom