Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

TABASAMU LA OLE SEBAYA LINA SIRI NZITO.

Anaandika, Robert Heriel

Ni kweli Ole Sebaya ni miongoni mwa Viongozi waliokuwa wakifanya kazi Kwa namna ya kipumbavu Sana, Hakuwa pekeake, walikuwa wa Aina yake kadha wa kadha, hao walijifanya miungu watu. Maneno yaliyowatoka midomoni yalikuwa kama wendawazimu. Sitaki kuwataja Ila wanajifahamu wenyewe na wengi walipata nafasi ya kusoma baadhi ya maandiko yangu. Wapo waliojirekebisha lakini wapo waliokaidi. Hata hivyo ndivyo maisha yatakavyo hivyo, wengine waangamie na wengine waokoke.

Mbali na udhaifu wa Ole Sebaya katika misukosuko yake tangu imkute lakini Jambo moja ninaweza kumsifu; nalo ni TABASAMU.

Ole Sebaya pamoja na uhuni wako ambao wengine tuliutambua Kwa ishara za lugha uongeapo kipindi ukiwa Mkuu wa wilaya, siwezi kuwa Mnafiki nikanyamaza kukunyima sifa hii, TABASAMU hata kwenye nyakati ngumu.


TABASAMU la OLE Sebaya linanifundisha mambo kadhaa, na linanifanya nimsifu Kwa ushujaa huo. Unajua kutabasamu wakati WA taabu sio mchezo.

Kila nilipomuona Ole Sebaya akishuka kwenye karandinga la mahabusu alishuka akiwa anatabasamu.
Jambo hili niliwahi fundishwa zamani Sana nikiwa mtoto mdogo kuwa;

Mbinu moja wapo ya kukabiliana na nyakati ngumu ni KUTABASAMU.
Mbinu hii nimeishuhudia mara mbili, na Ole Sebaya anakuwa mtu wa tatu kumuona akiwa anatabasamu hata akiwa katika Mazingira magumu.

Sina Shaka kuwa Ole Sebaya ni Mhalifu, katika hilo sina Shaka kwani alishajuonyesha tangu alipopewa Cheo cha ukuu wa wilaya. Ingawaje wapo wengine ambao bila Shaka muda huu wanaomba miungu yao kuwa upepo wa Sebaya usiwageukia na wao.

TABASAMU la Sebaya linaweza kuwa na maana Kati ya zifuatazo;
1. Matumaini.
Ole Sebaya anatabasamu huenda anamaana kuwa anayopitia ni majaribu tuu, yote yatapita

2. Majuto
Ole Sebaya anatabasamu Kama mtu anayejuta, anayejidharau kuwa alikuwa mjinga na Mpumbavu, n.k

3. HAKUWA PEKEAKE.
Ole Sebaya huenda anatabasamu Kwa sababu anashangaa kageuka Mbuzi WA kafara, waliofanya Kama yeye huenda walikuwa wengi lakini anaona yeye ndiye kaangukiwa na kitu kizito.

4. MAPENZI YA MCHUMBA WAKE YAMEMPONZA.
TABASAMU la OLE linasema mambo mengi.
Yale ya ngoswe kipenzi cha uzembe yanaweza kuwa yamemkuta Bwana Sebaya.
Huenda zile hela za unyang'anyi alikuwa anazipeleka Kwa mchumba wake huyo ambaye ndiye aliiomba mahakama imfikirie kwani anamchumba amemtolea mahari.

Sebaya huenda anatabasamu Kwa kujicheka kuona mchumba wake kasababisha kajiingiza katika matatizo.
Huenda anatabasamu kila akikumbuka akiombwa pesa ndefu na mchumba wake, huku Mshahara wa ukuu wa wilaya akiona ni mdogo. Hayo yote ni assumption tuu.

Ila Siri za TABASAMU la OLE Sebaya anazijua yeye mwenyewe.

Ole Sebaya mbali na kuwa sikupendezwa na tabia zako mbofu na nilitarajia matokeo haya kwako lakini nisiwe muongo kuwa nilikuona jasiri kila nilipoona unatabasamu.

Nitaenda kumtembelea Ole Sebaya kisha nitamuuliza TABASAMU lake lilikuwa na maana gani?

Ipendeze Ukate Rufaa alafu ujipange kwenye kujitetea bhana. Masuala ya kitoto ya kuleta Uchumba kwenye ishu nzito zinazokukabili uachane nazo.

Mimi nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam

Ujinga tu
 
Naomba mwenyewe namba yake wakuu,😋😋 kuda kufaanaa

2965149_JamiiForums40625557.jpg


2965148_JamiiForums-1241357733.jpg
 
"TABASAMU", imekuwa "TABASAMU", robo tatu ya andiko zima, 'what the heck is that'!

Hapa kuna mtu aliyekuwa tayari kutoa roho za watu, leo hii tunahadithiwa juu ya tabasamu lake? Hakuna habari ya kumzungumzia huyu mtu na wengine wa aina yake ambao tunapaswa kuwaepuka kila iwezekanavyo kuweka watu wa aina hiyo kwenye uongozi wa nchi?

Hakuna mafunzo yoyote tunayoweza kuyafafanua tukitumia mifano ya hawa watu ili jamii ielewe hatari zinazoambatana na kutokuwa waangalifu kwenye kutafuta viongozi wa nchi yetu?


Funzo tulilolipata ni kutabasamu hata katika nyakati ngumu.

Uzi huu inahusu zaidi TABASAMU la OLE Sebaya, hayo mengine sio muda wake
 
Ajiongeze akamuoneshee tabasamu vizuri nyapara wa jela inaweza kusaidia kuepukana na shulba za mle mjengoni

Akinyea makasha miaka miwili tutahitaji kuona hilo tabasamu limefikia level ipi
 
Ajiongeze akamuoneshee tabasamu vizuri nyapara wa jela inaweza kusaidia kuepukana na shulba za mle mjengoni

Akinyea makasha miaka miwili tutahitaji kuona hilo tabasamu limefikia level ipi


😄😄😄

Unazingua ujue.

Hatochoka kutabasamu, ashakuambia Mungu yupo kazini,
 
kwani mbowe ni nani mbele ya sheria za nchi hii?!
kama Haki imetendeka kwa Sabaya bilashaka itayendeka pia kwa Mbowe.
yaani wafuasi wa mtuhumiwa wa Ugaidi wanataka kutuaminisha kuwa Haki kwa mbowe ni kuachiwa tu sio kufungwa jela!!!
Haki ni Haki tu.
Sabaya Kala 30 huko!!..Mbowe bado kesi iko mahakamani!!..Msaidieni General Sabaya aliyekiri Makosa na kuomba apunguziwe Adhabu kisa ametoa mahali Kwa mtoto wa Mjini (slay queen)
 
wanasheria tunaomba ufafanuzi hapa kuna wengine wanasema hukumu ni jumla ya miaka 30 hivyo inagawanywa kwa watu 4 kila mmoja mika 7, wengne wanasema kila mmoja miaka 30 kwasababu miaka haigawanyiki

hivyo ukweli ni upi
Kila mshtakiwa atakwenda jela miaka 30.

Kwa hesabu za Magereza watakaa miaka 20 hivyo watatoka 2041 ma kumkuta Rais wa awamu ya 8!
 
Namwonea huruma sana huyu bwamdogo wanampoteza kihuni tu wakati wao ndio walikua wanamtumia.
Zamani sana hata pia Ben saa8 tangu anajiunga hapa,akawa lopolopo sana kila kitu anakijua yeye.
Niliwai kumshtua tu kama mdogo wangu "e bana taratibu"siasa za Bongo nenda nazo mdogo mdogo.
Ndo kwaanza akawa bichwa hilo.
Alikopotelea hamna anayejua mpk leo.
 
Namwonea huruma sana huyu bwamdogo wanampoteza kihuni tu wakati wao ndio walikua wanamtumia.
Zamani sana hata pia Ben saa8 tangu anajiunga hapa,akawa lopolopo sana kila kitu anakijua yeye.
Niliwai kumshtua tu kama mdogo wangu "e bana taratibu"siasa za Bongo nenda nazo mdogo mdogo.
Ndo kwaanza akawa bichwa hilo.
Alikopotelea hamna anayejua mpk leo.


😄😄😄😄

Mungu ndiye Hakimu
 
Anajaribu kuonyesha watu kwamba yuko sawa ila amevurugwa sana ndani yake

Sabaya ni mtu flani smart nikisema smart simaanishi ni mwema hapana
Ila anauwezo wa kufanya maasi na kuaminisha watu kwamba yeye ni mwema kama hauko makini unaweza ukamuamini

Tofauti na makonda mzee wa kufeli alikuwa anafosi tu Ufox

Kwa mambo aliyokuwa anafanya sabaya
Siyo mtu wa kuja na kusema alitumwa na Rais na Mpango anajua hiyo, kwa kauli hii ni kwamba hayo mambo yanamchanganya sana kwa ndani

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Anajaribu kuonyesha watu kwamba yuko sawa ila amevurugwa sana ndani yake

Sabaya ni mtu flani smart nikisema smart simaanishi ni mwema hapana
Ila anauwezo wa kufanya maasi na kuaminisha watu kwamba yeye ni mwema kama hauko makini unaweza ukamuamini

Tofauti na makonda mzee wa kufeli alikuwa anafosi tu Ufox

Kwa mambo aliyokuwa anafanya sabaya
Siyo mtu wa kuja na kusema alitumwa na Rais na Mpango anajua hiyo, kwa kauli hii ni kwamba hayo mambo yanamchanganya sana kwa ndani

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app


Umesema kweli.

Mshikaji hapo sijui ilikuwaje
 
Back
Top Bottom