Naomba niongelee suala hili kwa ufupi, kwa mtazamo wa dini ninayofuata mimi.
mimi nimezaliwa kwenye uislamu, na ninaishi kiislamu mpaka sasa...lakini kuzliwa muislamu, hakukunifanya nisichunguze na kujifunza vitu muhimu vya dini zingine, na kuuchunguza uislamu na kuulinganisha na dini zingine ili niweze kuwa na sababu zaidi ya kuniridhisha kuendelea au kutoendelea na dini hii!! so, mimi ni muislamu wa makusudi kabisa, na sipo katika uislamu by chance, najua niko wapi na kwa ajili gani, na naelewa nilipo kadiri ya elimu niliyojaaliwa.
DINI ni nini: Dini ni mfumo mzima wa maisha ya mwanadamu (kulingana na Islam)
- Maana hiyo, imetokana na kwamba, Waislamu wana mwongozo mzima wa jinsi ya kuishi hapa duniani, wana mwongozo jinsi ya kutembea, kula, kulala, kuamka, kusalimia, kuishi na wasio wasilamu, kuongea, kusoma na kila kitu kihusucho maisha yake, ndio maana Kiislamu, dini ni mfumo mzima wa maisha (Uliotoka kwa Mungu)
Lengo la kuumbwa na kuwekwa duniani:
-Tumeumbwa ili tumuabudu, viumbe wanaotakiwa kumuabudu Mungu (Kwa hiari yao) ni Watu na Majini! kwa sababu, Mungu kaumba kaumba viumbe wengi, majini, watu, malaika, mimea na vingine... lakini, ktk viumbe hawa, ningependa kuwaelezea kwa uchache watu, malaika na majini..
1 - Watu
. wameumbwa kwa udongo, wana nguvu za mwili ziwawezeshazo kufanya kazi zao.
. wamepewa akili, utashi.
. wamepewa na matamanio na uchaguzi huru (yani unaweza ukatamani siku nzima wewe uogelee kwa mfano au chochote, na ukaamua either ufanye kitu fulani au usifanye may be uwe muislamu au uwe mkristo)
2 - Majini
. Wameumbwa kwa ulimi wa moto (smokeless flame)
. Nguvu za miili(physical abilities and capacity) yao ni nyingi kuliko za watu eg wana kasi kubwa, na uwezo wa kuiga umbo la viumbe wengine i.e wanyama au watu au hata kuwa-possess watu na hawaonekani kwa watu mpaka watakapoamua wao kuwa visible)
. wana matamanio kama walivyo watu na wana uchaguzi huru kama watu
3 - Malaika
. Wameumbwa kwa nuru (light) na wana akili na utashi
. Wana nguvu zaidi ya jini na mtu, speed na wao pia ni ninvisible mpaka iamuliwe kuonekana na pia wanaweza kubadili umbo na kuonekana kivingine, ila wao mara zote huonekana kwa umbo la binaadamu wa kiume aliye safi, tofauti na jini anaweza tokea kama nyoka, au mtu pia
. Hawana matamanio, na hawana uchaguzi huru, wao ni watiifu, na waliumbwa wengi, tofauti tofauti kwa malengo tofauti, hawasahau wala kukiuka majukumu yao.
3 - Wanyama
. hawana utashi
. wana matamanio
. wao waliumbwa kwa amri tu ya neno la mungu, kwamba "kuwa kitu fulani" basi wakawa.
kwa uchache ya maelezo hayo, jini na binaadamu ndio wana fuzu kuwa na jukumu la ibada!
ibada ni nini:
ibada ni utii au kufanya mambo kama yalivyoamriwa na Mungu kwa mfano, sali kama alivosema, ishi na watu kama alivosema, kula kama alivoagiza, sema na watu kama alivoagiza fanya kila kitu kama alivoagiza, hiyo ndio ibada au kuabudu!
kwa nini sasa dini, na kuabudu:
Tumeumbwa kwa lengo mahsusi kabisa la kumuabudu, na katuweka hapa duniani, MAHSUSI KABISA KWA KUTUPA MITIHANI NA MAJARIBU!!!
hapa dunia ndio maana tunaumwa, vita, misunderstanding, wizi, kuuwana, na kila aina ya machukizo tunayaona hapa, na YOTE MAZURI YANAYOTUFURAHISHA mfano mali, mke au mume, watoto na mengine, YOTE NI MITIHANI NA MAJARIBU na huyo shetani pia akawepo (ingawa baada ya shetani kuwepo, katuletea mitume na vitabu mbali mbali ambavyo vinatufundisha kuhusu shetani, lengo lake na mwisho wake kama ukimfwata na mbinu kede kede za kujikinga naye...Waislamu tuna mpaka dua ya kuomba kikingwa na shetani!!!
kwa ufupi, dunia ni kama chumba cha mtihani, kila kitu utakiona hapa, ILA ATAKAYEFAULU, NDIYE ATAKAYEENDA PEPONI.
Kuhusu huruma na Upendo wa Mungu:
Licha ya kutupa haya mabalaa yote, LAKINI KUMBUKA AMETUPA AKILI, NA UWEZO WA KUCHAGUA KUFANYA JAMBO AMA LA!!! lakini, licha y ya yote hayo, HATA UFANYE DHAMBI MARA NGAPI, kwa miaka mingapi, ukikaa ukamwomba msamaha ndani ya sekunde chache tu, hata usikae dakika, ATAKUSAMEHE!!!! na makosa aliyokusamehe, hayatohusika tena mbeleni, labda ufanye mengine, nayo ukiomba toba kwa dhati, atasamehe pia!
pia, haya mabalaa yanayotupata, kwa vile tupo duniani maalumu kwa ajili ya majaribio, kuna malipo yake, huteseki hivi hivi (ila kwa wenye imani sahihi juu ya Mungu)
Kuhusiana na Mungu Kuhitaji:
umesema anahitaji kuheshimiwa na mengine.
naomba nikurekebishe, hahitaji, ANATAKA!!!!! ambapo, kumuheshimu, ni kwa ajili ya nafsi yako, maana yake, ukimuabudu na kumuheshimu, humwongezi kitu yeye na ukiacha, humpunguzii kitu! yote hayo unafanya kwa kuiokoa nafsi yako!
MWISHo kabisa:
Katika Islam, tunaambiwa-
Tumeiumbwa kisha tukapewa njia 2, ima USHUKURU (kwa kuwa mtiifu au kuamini na kufanya mema) ima UKUFURU (Kwa kufanya yoyote nafsi yako inayokutuma ambayo ni kinyume na amri).
lakini, mwisho wa siku, you will be hel accountable kwa kila ulichokifanya!..maana umeshapewa akili, matamanio, na energy, ukaambiwa shetani ni nani na anafanya nini na kwa nini, na ukaambiwa uko hapa kwa sababu gani na ukapewa vitabu, mitume na mwongozo wa jinsi ya kuishi!
hapo kwenye kuabudu na kutii kila alichoamrisha Mungu, na kuacha aliyokataza, ambayo kwa lugha nyingine ni ibada, ndo LINAKUJA NENO ISLAM, yani SUBMISSION au KUJISALIMISHA au UNYENYEKEVU mbele za Mungu!
*****kama kuna makosa yoyote, mimi ni binaadamu, turekebishe, tutoe maono yetu, tuelimike na tudumishe amani*****
deni FaizaFoxy