Lengo la dini ni nini?

Lengo la dini ni nini?

Hivi kwanini NASA hawakutengeneza chombo cha kugundua Mungu yuko wapi ??!!!.. kazi kuchunguza masayari .. si watengeneze chombo watutafutie huyu Mkuu kakaa kipande IPI...
Ndugu yangu mmungu huwa hazihakiwii jaribu kuwa na busara kidog na pia jaribu kuwa na fikra kabla huja andika kitu japo una uhuru wa mawazo unacho kifikir.

Note
NASA kwanza watengeneza kitu kitakacho tambua ile ndege ya malaysia air line MH80 imepotelea wapi hata mwili hauja patikana hadi leo na bahar ni hizi hizi .
Munyezi mungu anasema kweny vitabu vyake amempa BINAADAM akili kidogo sn kwa maan (ELIMU) ili apate kushukuru.
 
Mbulaaa......unautak auwendawizumu muda sio mrefu! AAcha kabisa kufikiri juu ya uwepo wa Mungu,..

Wewe kama unaamini hayupo kaa kimya..

Kama unaamini yupo, endelea kumwabudu na kumsifu milele!

Siamini kama mungu wako anaweza kufundisha haya ulio andika
 
Naomba niongelee suala hili kwa ufupi, kwa mtazamo wa dini ninayofuata mimi.

mimi nimezaliwa kwenye uislamu, na ninaishi kiislamu mpaka sasa...lakini kuzliwa muislamu, hakukunifanya nisichunguze na kujifunza vitu muhimu vya dini zingine, na kuuchunguza uislamu na kuulinganisha na dini zingine ili niweze kuwa na sababu zaidi ya kuniridhisha kuendelea au kutoendelea na dini hii!! so, mimi ni muislamu wa makusudi kabisa, na sipo katika uislamu by chance, najua niko wapi na kwa ajili gani, na naelewa nilipo kadiri ya elimu niliyojaaliwa.

DINI ni nini: Dini ni mfumo mzima wa maisha ya mwanadamu (kulingana na Islam)
- Maana hiyo, imetokana na kwamba, Waislamu wana mwongozo mzima wa jinsi ya kuishi hapa duniani, wana mwongozo jinsi ya kutembea, kula, kulala, kuamka, kusalimia, kuishi na wasio wasilamu, kuongea, kusoma na kila kitu kihusucho maisha yake, ndio maana Kiislamu, dini ni mfumo mzima wa maisha (Uliotoka kwa Mungu)

Lengo la kuumbwa na kuwekwa duniani:
-Tumeumbwa ili tumuabudu, viumbe wanaotakiwa kumuabudu Mungu (Kwa hiari yao) ni Watu na Majini! kwa sababu, Mungu kaumba kaumba viumbe wengi, majini, watu, malaika, mimea na vingine... lakini, ktk viumbe hawa, ningependa kuwaelezea kwa uchache watu, malaika na majini..

1 - Watu
. wameumbwa kwa udongo, wana nguvu za mwili ziwawezeshazo kufanya kazi zao.
. wamepewa akili, utashi.
. wamepewa na matamanio na uchaguzi huru (yani unaweza ukatamani siku nzima wewe uogelee kwa mfano au chochote, na ukaamua either ufanye kitu fulani au usifanye may be uwe muislamu au uwe mkristo)

2 - Majini
. Wameumbwa kwa ulimi wa moto (smokeless flame)
. Nguvu za miili(physical abilities and capacity) yao ni nyingi kuliko za watu eg wana kasi kubwa, na uwezo wa kuiga umbo la viumbe wengine i.e wanyama au watu au hata kuwa-possess watu na hawaonekani kwa watu mpaka watakapoamua wao kuwa visible)
. wana matamanio kama walivyo watu na wana uchaguzi huru kama watu

3 - Malaika
. Wameumbwa kwa nuru (light) na wana akili na utashi
. Wana nguvu zaidi ya jini na mtu, speed na wao pia ni ninvisible mpaka iamuliwe kuonekana na pia wanaweza kubadili umbo na kuonekana kivingine, ila wao mara zote huonekana kwa umbo la binaadamu wa kiume aliye safi, tofauti na jini anaweza tokea kama nyoka, au mtu pia
. Hawana matamanio, na hawana uchaguzi huru, wao ni watiifu, na waliumbwa wengi, tofauti tofauti kwa malengo tofauti, hawasahau wala kukiuka majukumu yao.

3 - Wanyama
. hawana utashi
. wana matamanio
. wao waliumbwa kwa amri tu ya neno la mungu, kwamba "kuwa kitu fulani" basi wakawa.

kwa uchache ya maelezo hayo, jini na binaadamu ndio wana fuzu kuwa na jukumu la ibada!

ibada ni nini:
ibada ni utii au kufanya mambo kama yalivyoamriwa na Mungu kwa mfano, sali kama alivosema, ishi na watu kama alivosema, kula kama alivoagiza, sema na watu kama alivoagiza fanya kila kitu kama alivoagiza, hiyo ndio ibada au kuabudu!

kwa nini sasa dini, na kuabudu:
Tumeumbwa kwa lengo mahsusi kabisa la kumuabudu, na katuweka hapa duniani, MAHSUSI KABISA KWA KUTUPA MITIHANI NA MAJARIBU!!!
hapa dunia ndio maana tunaumwa, vita, misunderstanding, wizi, kuuwana, na kila aina ya machukizo tunayaona hapa, na YOTE MAZURI YANAYOTUFURAHISHA mfano mali, mke au mume, watoto na mengine, YOTE NI MITIHANI NA MAJARIBU na huyo shetani pia akawepo (ingawa baada ya shetani kuwepo, katuletea mitume na vitabu mbali mbali ambavyo vinatufundisha kuhusu shetani, lengo lake na mwisho wake kama ukimfwata na mbinu kede kede za kujikinga naye...Waislamu tuna mpaka dua ya kuomba kikingwa na shetani!!!
kwa ufupi, dunia ni kama chumba cha mtihani, kila kitu utakiona hapa, ILA ATAKAYEFAULU, NDIYE ATAKAYEENDA PEPONI.

Kuhusu huruma na Upendo wa Mungu:
Licha ya kutupa haya mabalaa yote, LAKINI KUMBUKA AMETUPA AKILI, NA UWEZO WA KUCHAGUA KUFANYA JAMBO AMA LA!!! lakini, licha y ya yote hayo, HATA UFANYE DHAMBI MARA NGAPI, kwa miaka mingapi, ukikaa ukamwomba msamaha ndani ya sekunde chache tu, hata usikae dakika, ATAKUSAMEHE!!!! na makosa aliyokusamehe, hayatohusika tena mbeleni, labda ufanye mengine, nayo ukiomba toba kwa dhati, atasamehe pia!
pia, haya mabalaa yanayotupata, kwa vile tupo duniani maalumu kwa ajili ya majaribio, kuna malipo yake, huteseki hivi hivi (ila kwa wenye imani sahihi juu ya Mungu)

Kuhusiana na Mungu Kuhitaji:
umesema anahitaji kuheshimiwa na mengine.
naomba nikurekebishe, hahitaji, ANATAKA!!!!! ambapo, kumuheshimu, ni kwa ajili ya nafsi yako, maana yake, ukimuabudu na kumuheshimu, humwongezi kitu yeye na ukiacha, humpunguzii kitu! yote hayo unafanya kwa kuiokoa nafsi yako!

MWISHo kabisa:

Katika Islam, tunaambiwa-
Tumeiumbwa kisha tukapewa njia 2, ima USHUKURU (kwa kuwa mtiifu au kuamini na kufanya mema) ima UKUFURU (Kwa kufanya yoyote nafsi yako inayokutuma ambayo ni kinyume na amri).

lakini, mwisho wa siku, you will be hel accountable kwa kila ulichokifanya!..maana umeshapewa akili, matamanio, na energy, ukaambiwa shetani ni nani na anafanya nini na kwa nini, na ukaambiwa uko hapa kwa sababu gani na ukapewa vitabu, mitume na mwongozo wa jinsi ya kuishi!

hapo kwenye kuabudu na kutii kila alichoamrisha Mungu, na kuacha aliyokataza, ambayo kwa lugha nyingine ni ibada, ndo LINAKUJA NENO ISLAM, yani SUBMISSION au KUJISALIMISHA au UNYENYEKEVU mbele za Mungu!

*****kama kuna makosa yoyote, mimi ni binaadamu, turekebishe, tutoe maono yetu, tuelimike na tudumishe amani*****

deni FaizaFoxy
 
Fikra za uwepo wa mungu ni pana sana na zinahitaji utulivu wa akili na uelewa wa namna ya juu sana
Mungu ni upendo, mungu ni kufanya mema, mungu ni kama nguvu flani katika akili yako, Mungu ni kama nguvu ya akili yako uwapo ndotoni, Mungu ni mtu yeyote unaemwona mbele yako.
Ila dini ni mahali flani ambapo watu ukusanyikia kuelimishana kuhusu nguvu na umuhimu wa upendo na kuishi katika misingi flani ili tu tusiwe chukizo, kukwaza mtu ambae ndiyo mungu hivyo huo upendo ni mungu
Mungu ni nguvu safi ya akili inayokufanya kufanya mambo meme hapo ndiyi tunakuwa na usawa wa akili na baada ya kuwa na usawa wa akili ndiyo mafanikio upatikana na shetani ni nguvu mbaya ya akili ambay umfanya mtu kufanya mambo bila utaratibu mzuri, ubaya, chuki, jirasi hivyo basi mtu wa aina hii mara chache sana ufanikiwa kwa sababu anakuwa hana ana mpangilio mzuri wa mambo ambayo yatamfanya kufanikiwa
 
Hongera nadhani mmeanza kuelewa
....Free ideas....
 
Dini is for, mass mind control of people. Hapo huchomoki dini na uongozi are two things for one purpose
 
Daktari (surgeon) anayeokoa maisha ya wengine anafanya hivyo kupitia elimu na anayetengeneza bomu la kuteketeza kijiji kizima anatumia elimu hiyo hiyo. Au tafsiri nyingine ni kuwa huenda aliyebuni kisu nia yake ilikuwa ni kukatia nyanya na anayekitumia kuua binadamu mwenzie anakiona kimemsaidia kutimiza malengo yake pia.

Kwa dini ni kama dawa kwa matatizo ya dunia kama ulivyoyaainisha na naona uko sawa kabisa kwa maana kama dawa iliyokusudiwa inamuongezea matatizo mgonjwa basi ni bora isiwepo. Hivyo hivyo kama binadamu tumeshindwa kuielewa dini na kuitumia kutusaidia badala yake tukaishia kuuana kwa sababu ya dini basi ni bora isiwepo!
 
Nilizaliwa nikiwa sielewi chochote kuhusu huu ulimwengu na maisha kwa ujumla, kadri nilivyozidi kukua nilifundishwa mambo mengi. Dini ni miongoni mwa yale ambayo nilifundishwa wakati nakua, lakini leo nimefikia mahali nimeaza kuona kwamba Dini ni swala amabalo nilikua nafundishwa kwa msistizo mkubwa , lakini ki uhalisia sioni umuhimu wake.

Katika mjadala huu ni jaribu kuziwasilisha fikra zangu kwa kutumia dini ya kikristo kama reference, kwa kua hiyo ndo nilibahatika kuwa na uzoefu nayo; nimekua na uzoefu nayo kwa kuwa ni random chance tu imetokea nikazaliwa kwenye familia ya kikristu.

Wazazi wangu na viongozi wa dini walinifundisha, kupitia dini, kwamba kuna Mungu aliyeumba kila kitu kilichopo na huyo Mungu anasifa zifuatazo:

  • Anaweza yote na anajua yote.
  • Ana upendo kuliko wote, yeye ni mwema kuliko wote.
  • Anachukia uovu, na atawachoma na kuwatesa milele wale walio mkosea.(kwa akili yangu hili kama linakinzana na sifa ya kuwa na upendo).
  • Yeye ana kila kitu hana uhitaji (lakini hili linakinzana na pale nilipofundishwa kwamba Mungu anahitaji sifa na kuheshimiwa, tena kuna wakati Mungu anaonekana ana wivu)
  • Aliumba kila kitu
  • Alimuumba shetani ambaye mabaya yote yanaunganishwa na yeye, alafu badae akamuumba Yesu atuokoe (This is one of tricky things that God is described to do on us) yaani Mungu anatuchezesha kama midoli.

Nilifundishwa sifa nyingi za Mungu, ambazo nyingi zinakinzana, nyingine nimeshindwa kuzikumbuka kwa sasa wakati naandika.

Katika dini yangu nilifundishwa(indirectly), kutokuwasikiliza watu wa dini nyingine kuhusu imani zao. Dini yangu ilinifanya niwatazame watu wa dini nyingine kwa mtizamo wa mashaka na kiasi flani cha chuki, na wakati mwingi niliamini wao wapo upande mbaya. Cha ajabu ni kwamba watu wadini nyingine nao walinitazama kwa mtazamo huo huo.

Dini zinajaribu kuniaminisha kwamba natakiwa kuishi maisha ya kujiandaa ili nipate maisha mazuri ya mbinguni baada ya kufa, kwa sababu bila kufanya ivyo nitaishi maisha ya taaabu milele.

Najua dini nyingine zina baadhi ya mitizamo inayofanana na hii, kwa sababu kabla sijaamua kuzipuuzia dini nimekua nikijaribu kuzifuatilia, ila nyingi zinaonekana zina mitizamo mingi ya kukinzana na mingi isiyoeleweka kiakili.

Nimefikia mahali nimeamua kufikiria bila kuongozwa na dini ambazo nimezaliwa na kuzikuta tu. Nimebadili mitazamo na kuwa na mitazamo ifuatayo.

  • · Ukweli ni kwamba sifahamu asili ya huu ulimwengu ni nini, kunawezekana kukawa kuna jibu la asili ya ulimwengu lakini mpaka sasa sijapata hata moja ambalo halina utata.
  • Kitu nnacho kinachopatana na akili yangu kuhusu baada ya kufa, ni kwamba baada ya kufa kutakua ni sawa na kabla ya kuzaliwa kwangu. Hainiingii akilini kuhusu swala la kuteswa milele au kupewa raha milele.
  • · Sioni umuhimu wa dini.
  • · Kama Mungu (creator) yupo, basi inaonekana hana interest ya kuwasilia na sisi na kutuweka clear. Watu wengi wa dini wameshindwa kulielewa hili, ndio maana tunaona watu wanauana, kuchukiana na kujiua kisa dini-watu wa dini wanahangaika sana kumtetea Mungu wakati mwingine hata kuua, lakini Mungu mwenyewe muweza yote amejificha tu mahali pasipoonekana.
  • · Kwangu mimi lengo la maisha ni KUISHI. Just kuishi.
  • · Mema na mabaya ni vitu vinavyotambulika naturally, siamini kwamba dini inahitajika kutusaidia kutambua mema na mabaya.

Kuhitimisha naomba niseme kwamba binadamu tumeacha dini zichukue furaha yetu, tunazihangaikia sana mpaka tunajiumiza kwa kitu kinachoonekana hakina umuhimu.

Nawasilisha, nikiuliza "Why should we care about religions?",
Uko sawa kabisa lakini kwa akili za kibinadamu !! unamtafakari Mungu kwa kutumia utashi na maarifa ya kidunia hapo kamwe hutaweza kupata jibu. Kipofu wa kiroho atawezaje kuona uwepo wa Mungu!!. Ukimtafuta Mungu kwa njia sahihi hakika atajifunua kwako ndipo utaelewe dhumuni la wewe kuja hapa Duniani .
 
Pia naomba kuuliza wengi tunaamini Mungu ni mmoja tu lakini waislamu wamamwabudu kupitia mtume Mohamed na wakristu wanamwabudu kupitia Yesu kristo baadhi ya wahindi wanamwabudu kupitia ngo'mbe,je inawezekana Mungu akawaambia viumbe wake wafanye hivyo kiasi mpaka wanachukiana kutokana na imani zao kuwa tofauti au pengine wako zaidi ya mmoja?
 
Nilizaliwa nikiwa sielewi chochote kuhusu huu ulimwengu na maisha kwa ujumla, kadri nilivyozidi kukua nilifundishwa mambo mengi. Dini ni miongoni mwa yale ambayo nilifundishwa wakati nakua, lakini leo nimefikia mahali nimeaza kuona kwamba Dini ni swala amabalo nilikua nafundishwa kwa msistizo mkubwa , lakini ki uhalisia sioni umuhimu wake.

Katika mjadala huu ni jaribu kuziwasilisha fikra zangu kwa kutumia dini ya kikristo kama reference, kwa kua hiyo ndo nilibahatika kuwa na uzoefu nayo; nimekua na uzoefu nayo kwa kuwa ni random chance tu imetokea nikazaliwa kwenye familia ya kikristu.

Wazazi wangu na viongozi wa dini walinifundisha, kupitia dini, kwamba kuna Mungu aliyeumba kila kitu kilichopo na huyo Mungu anasifa zifuatazo:

  • Anaweza yote na anajua yote.
  • Ana upendo kuliko wote, yeye ni mwema kuliko wote.
  • Anachukia uovu, na atawachoma na kuwatesa milele wale walio mkosea.(kwa akili yangu hili kama linakinzana na sifa ya kuwa na upendo).
  • Yeye ana kila kitu hana uhitaji (lakini hili linakinzana na pale nilipofundishwa kwamba Mungu anahitaji sifa na kuheshimiwa, tena kuna wakati Mungu anaonekana ana wivu)
  • Aliumba kila kitu
  • Alimuumba shetani ambaye mabaya yote yanaunganishwa na yeye, alafu badae akamuumba Yesu atuokoe (This is one of tricky things that God is described to do on us) yaani Mungu anatuchezesha kama midoli.

Nilifundishwa sifa nyingi za Mungu, ambazo nyingi zinakinzana, nyingine nimeshindwa kuzikumbuka kwa sasa wakati naandika.

Katika dini yangu nilifundishwa(indirectly), kutokuwasikiliza watu wa dini nyingine kuhusu imani zao. Dini yangu ilinifanya niwatazame watu wa dini nyingine kwa mtizamo wa mashaka na kiasi flani cha chuki, na wakati mwingi niliamini wao wapo upande mbaya. Cha ajabu ni kwamba watu wadini nyingine nao walinitazama kwa mtazamo huo huo.

Dini zinajaribu kuniaminisha kwamba natakiwa kuishi maisha ya kujiandaa ili nipate maisha mazuri ya mbinguni baada ya kufa, kwa sababu bila kufanya ivyo nitaishi maisha ya taaabu milele.

Najua dini nyingine zina baadhi ya mitizamo inayofanana na hii, kwa sababu kabla sijaamua kuzipuuzia dini nimekua nikijaribu kuzifuatilia, ila nyingi zinaonekana zina mitizamo mingi ya kukinzana na mingi isiyoeleweka kiakili.

Nimefikia mahali nimeamua kufikiria bila kuongozwa na dini ambazo nimezaliwa na kuzikuta tu. Nimebadili mitazamo na kuwa na mitazamo ifuatayo.

  • · Ukweli ni kwamba sifahamu asili ya huu ulimwengu ni nini, kunawezekana kukawa kuna jibu la asili ya ulimwengu lakini mpaka sasa sijapata hata moja ambalo halina utata.
  • Kitu nnacho kinachopatana na akili yangu kuhusu baada ya kufa, ni kwamba baada ya kufa kutakua ni sawa na kabla ya kuzaliwa kwangu. Hainiingii akilini kuhusu swala la kuteswa milele au kupewa raha milele.
  • · Sioni umuhimu wa dini.
  • · Kama Mungu (creator) yupo, basi inaonekana hana interest ya kuwasilia na sisi na kutuweka clear. Watu wengi wa dini wameshindwa kulielewa hili, ndio maana tunaona watu wanauana, kuchukiana na kujiua kisa dini-watu wa dini wanahangaika sana kumtetea Mungu wakati mwingine hata kuua, lakini Mungu mwenyewe muweza yote amejificha tu mahali pasipoonekana.
  • · Kwangu mimi lengo la maisha ni KUISHI. Just kuishi.
  • · Mema na mabaya ni vitu vinavyotambulika naturally, siamini kwamba dini inahitajika kutusaidia kutambua mema na mabaya.

Kuhitimisha naomba niseme kwamba binadamu tumeacha dini zichukue furaha yetu, tunazihangaikia sana mpaka tunajiumiza kwa kitu kinachoonekana hakina umuhimu.

Nawasilisha, nikiuliza "Why should we care about religions?",
Habari zenu jamani? Kwanza kabisa niseme kuwa nilikuwa kama wewe hivyo uaminivyo. Nilikuwa hivyo hivyo. Kwa miezi kadhaa nyuma ningeweza kukuunga mkono kwa hii post yako. Ila siwadanganyi. Mungu yupo.

Kijana vipo vya kufanya navyo masihara ila si Mungu kamwe! Nataka yeyotw mwenye wazo la kusema hakuna Mungu abadilike mapema sana!
Kwenye Biblia twasoma:

Zaburi 53:1
Mpumbavu anasema moyoni, hakuna Mungu;

Naandika mpate kujua. Jehanam ya moto ipo, mbinguni kupo na Yesu ndiye njia ya kwenda Mbinguni. Kwenye Biblia twasoma:

Yohana 14:6
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Kwa kuwasaidieni ufahamu zaidi mnaoamini hakuna Mungu wala Mbingu wala Jehanam. Ingieni youtube.

Ingia link hii:

(hii ina part 1 na 2 huko youtube)

Na hii:

Wanaeleza vizuri walivyochukuliwa ya Yesu mwenyewe katika roho na kuoneshwa kuzimu na mbinguni.

Waelezea walimuona:
-Michael Jackson
-Papa John Paul wa pili
-Celena Quintanilla Perez
-Winehouse
-Na mengine mengi mtayasikia kwenye hizo video (nisije nikaleta uchochezi wa imani za dini tofauti ila ni heri msikie wenyewe kutoka kwenye hizo video mbili ambazo nime share links zake.

(Hizo si hadithi bali ni kweli)

Wapo kuzimu na wanapewa mateso makali sana na mapepo. Na pia wameeleza vizuri kuwa ni kwa nini watu hao wapo kuzimu badala ya Mbinguni/Peponi

Pia mnatakiwa kujua kua hakuna kitu kama R.I.P kwani hii ni faraja tu ya kufarijiana duniani.

Someni Biblia kwa makini wanadamu wenzangu. Kwa maana hakuna atakayeikimbia ghazabu ya Mungu. Na tena msidanganyike. Twasoma kwenye Biblia:

1 Wakorintho 6:9
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,

Na pia twasoma:

Ufunuo 21:8
Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

Jamani, sina dhiki ya hela, siumwi na wala sina tatizo lolote lile kiasi cha kusema nimehamua kumcha Mungu/kuokoka. Ila nilionja pendo lake. Kila niombapo usiku huwa ananipa ishara za ajabu sana.

Jamani ee, yupo yeye ajae someni neno la Mungu.

Yesu alikufa kweli na siku ya tatu alifufuka katika wafu. Siwezi nikawaambia Yesu ana huruma kiasi gani ila mkiniuliza nina ushuhuda.

Mwenye swali ataniuliza hapa au hata inbox kwa msaada zaidi wa kiroho.

Nawapenda na Mungu awabariki sana.
 
Mbulaaa......unautak auwendawizumu muda sio mrefu! AAcha kabisa kufikiri juu ya uwepo wa Mungu,..

Wewe kama unaamini hayupo kaa kimya..

Kama unaamini yupo, endelea kumwabudu na kumsifu milele!
Hawez kuwa chizi au mwendawazimi,hii niatter ya perception ,anavyopassive yeye co xawa na ww,if really god exist why dont he care about our problems,
Peoples are killing themselves
Diseases
Disasters
But he remains silent
What if u hear that bible was a myth,or fiction

NO ONE KNOWS LET US WAIT AND SEE ,EVERY ONE SHOULD STICK ON HIS BELIEF
#am out
 
Wanasayansi wamerubuni watu kwa uongo wa hiyo elimu ya UHAKIKI ambapo imewapa jibu kuwa hakuna Mungu kiasi wao wametujia na UONGO ukubalikao kuwa MTU katokana na SOKWE tena aliishi Olduvai,Arusha hawasemi akazaazaaje yaani kupata opposite sex ilhali hao SOKWE bado wapo na ikitokea mwanamke kajifungua SOKWE wanakuja tena kutaka kujua sababu Bado wataongopa kuwa DUNIA inajizungusha kwenye MHIMILI WAKE wakati haupo.
Ni waongo mno WANASAYANSI hufikia hatua kuwatetea WANAOSAGANA na KULAWITANA kuwa ni maumbile ya KISAYANSI.
 
Bwana deni embu soma Wikipedia ya Buddha then utajua dini ni man made,Buddha wrote all rules and laws of life which are almostly resemble to those of islams and christians,he just sit and meditate then comes out with a lot of rules and laws to govern life
 
Hivi kwanini NASA hawakutengeneza chombo cha kugundua Mungu yuko wapi ??!!!.. kazi kuchunguza masayari .. si watengeneze chombo watutafutie huyu Mkuu kakaa kipande IPI...
Kwa nn kuisubiri NASA ,wakati unaweza kuanza wewe
JIAMINI
 
Mkuu dini ni utaratibu wa maisha ambao amejiwekea au amewekewa mwanadamu ili kuzistahimili changamoto za mazingira yanayo mzunguka.

Ama kuhusu historia yako ya kuzaliwa na kukuzwa kwenye dini na kuanza ku argue uwepo wa dini ni moja kati ya upeo wa juu wa kifikra kuwa bado ipo haja kuwa huo utaratibu uliojazwa tangu ukiwa mtoto hauna uhalisia na mazingira tuliyomo.

Kuhusu sifa za muumba ulizozitaja ni za kweli .. ila muumba alituumba sisi binadamu ili tuweze kutumia akili zetu... tu mtafute.. tu staajabu viumbe vyake.. tunshukuru.. tupambane na changamoto za mazingira na tuzishinde bila kukata tamaa... huwa ukifanya hayo kwa kumtegemea yeye na sababu ya wewe kuwepo ulimwengu huwa anafurahi na wewe utafurahi na jamii itafurahi..
 
daah ebana den umetisha, ila kwa kiasi kdogo npo upande wako, mie nimezaliwa katika familia ya kikristu na nikiwa na mwaka 1 nkabatizwa kama mkatoliki, ila kuanzia miaka 4 nyuma mpaka saiv huwa nasaligi nyumban make nmekuja kuona dini zishakuwa business.
 
Back
Top Bottom