Mzee Wa Republican
JF-Expert Member
- Jul 20, 2013
- 1,666
- 847
Salaam sana wakuu,
Tunamshukuru Muumba wa mbingu na nchi kwa kutufikisha disemba hii 2021 ambapo tunapata nafasi mtawalia ya kutafakari kwa kina malengo tuliyojiwekea kwa mwaka 2021 huku tukijipanga kwa ajili ya mwaka mpya 2022. Binafsi nina lengo la kufanya savings ifike milioni 20 ifikapo mwaka 2022 mwezi Oktoba. Maandalizi kwa ajili ya kufanikisha lengo langu hilo nimeshayaanza kwani mpaka sasa nimeshafungua akaunti ya kufanya savings hiyo. Vile vile kuna kijikazi nakifanya (tofauti na kazi yangu rasmi ya mshahara) kwa hiyo nitakuwa na inflow fulani hivi ambayo kwa miezi tarajiwa mpaka Oktoba 2022 ninaweza kufikia kiwango hicho cha milioni 20.
Lengo kuu la savings hiyo ni kuwezesha ujenzi wa banda langu la kujifichia hapa jijini Dar es Salaam kwani maisha ya upangaji ni magumu na kwa vijana wengi tunajua kuwa wakati wa kutafuta nyumba zetu ni sasa ili kupunguza mzigo wa kodi ya nyumba pale utakapokuwa na familia maana sisi hatuna utegemezi wa kurithi mali za wazazi wetu.
Niko hapa mbele yenu ili nipate uzoefu kwa wale waliowahi kujiwekea malengo ya kufanya savings kwa kipindi fulani cha miezi na hata miaka wanipe uzoefu ni kwa namna gani walifanikiwa kufikia malengo yao sambamba na changamoto walizokutana nazo jambo linaloweza kuwa chachu ya mafanikio sio kwangu tu bali hata kwa wenzangu waliopo katika jukwaa hili kwani changamoto za savings hakuna asiyezijua na isitoshe hakuna mtu asiye na matumizi ya pesa ikiwepo kuruka mitego kadhaa ya maombi ya ndugu, jamaa, marafiki pamoja na watoto wa mjini (hasa wa kike) si mnajua wanavyovutia wakuu ";;;;;;. . . .
Naomba kuwasilisha wakuu . . .