Lengo la kuwa na saving ya milioni 20 ifikapo mwaka 2022 mwezi Oktoba

Lengo la kuwa na saving ya milioni 20 ifikapo mwaka 2022 mwezi Oktoba

Usiangaike kufanya saving. Kama una kiwanja anza kununua materials kama matofali, nondo, simenti na mchanga. Unaweza kuweka site au kuviweka kwa jirani ya site. Pia ukiweza kuanza uanze tu.

Mimi nina nyumba kadhaa na sehemu tofauti tofauti na sikuwahi kuanza kujenga nikiwa na milioni 10. Hata nikiwa na milioni mbili tu nachora ramani nalianzisha na baada ya muda zinaisha na nawapangisha raia zinazalisha naanza nyingine.

Kama una laki tano hapo kanunue tofali leo peleka site,nakuhakikishia mwezi Disemba utakuwa mbali zaidi ya hiyo milioni 24 unayotaka kusevu. Tofauti na hapo huwezi kukusanya hiyo hela labda ukope

Fanya nilivyokuelekeza utanishukuru baadae. Achana na savings
Huu ushauri ni mzuri na salama kuliko kuweka pesa kama pesa
 
Account itakayokupa riba bora zaidi kwa lengo lako ni kununua vipande vya Liquid Fund ya utt.

Unaiongezea fedha siku yoyote, hata kwa miamala ya simu. Utakapofikia kuzihitaji fedha zako unajaza fomu, within 3 working days unazipata.

Riba ni zaidi kidogo ya 11% per annum. Hupati riba za hivyo benki kwa hali za kawaida.

Watakuja wa kuponda riba hizo na kusema uzifanyie biashara fedha zako - lakini ulivyosema lengo lako ni kusave ili ujenge.

Unauzungumziaje mfuko wa BOND fund
 
Salaam sana wakuu,

Tunamshukuru Muumba wa mbingu na nchi kwa kutufikisha disemba hii 2021 ambapo tunapata nafasi mtawalia ya kutafakari kwa kina malengo tuliyojiwekea kwa mwaka 2021 huku tukijipanga kwa ajili ya mwaka mpya 2022. Binafsi nina lengo la kufanya savings ifike milioni 20 ifikapo mwaka 2022 mwezi Oktoba. Maandalizi kwa ajili ya kufanikisha lengo langu hilo nimeshayaanza kwani mpaka sasa nimeshafungua akaunti ya kufanya savings hiyo. Vile vile kuna kijikazi nakifanya (tofauti na kazi yangu rasmi ya mshahara) kwa hiyo nitakuwa na inflow fulani hivi ambayo kwa miezi tarajiwa mpaka Oktoba 2022 ninaweza kufikia kiwango hicho cha milioni 20.

Lengo kuu la savings hiyo ni kuwezesha ujenzi wa banda langu la kujifichia hapa mjini Dar es Salaam kwani maisha ya upangaji ni magumu na kwa vijana wengi tunajua kuwa wakati wa kutafuta nyumba zetu ni sasa ili kupunguza mzigo wa kodi ya nyumba pale utakapoikuwa na familia maana sisi hatuna utegemezi wa kurithi mali za wazazi wetu.

Niko hapa mbele yenu ili nipate uzoefu kwa wale waliowahi kujiwekea malengo ya kufanya savings kwa kipindi fulani cha miezi na hata miaka wanipe uzoefu ni kwa namna gani walifanikiwa kufikia malengo yao sambamba na changamoto walizokutana nazo jambo linaloweza kuwa chachu ya mafanikio sio kwangu tu bali hata kwa wenzangu waliopo katika jukwaa hili kwani changamoto za savings hakuna asiyezijua na isitoshe hakuna mtu asiye na matumizi ya pesa ikiwepo kuruka mitego kadhaa ya maombi ya ndugu, jamaa, marafiki pamoja na watoto wa mjini (hasa wa kike) si mnajua wanavyovutia wakuu ";;;;;;. . . .

Naomba kuwasilisha wakuu . . .
Usi-save. Mwisho mwa 2022 hio 22 million inaweza ikawa haina thamani. Vifaa vya ujenzi vinapanda bei mara mbili mfano mwanzoni mwa 2021, nondo ya 10mm ilikuwa tshs 15,000. December 2021 ikawa tshs 22,000. Sasa hapo uki-save na hii inflation utaumia. Kila ukipata hela iweke kwa ujenzi.. usisubiri uwe na hela nyingi.
 
Unauzungumziaje mfuko wa BOND fund
Bond fund iko structured kumfaa zaidi mtu aliye na kiasi fulani kikubwa, anaweka kwenye mfuko huo - halafu sehemu ya faida inatumika kumlipa kila mwezi au kila kipindi fulani anachochagua. Mfano anayestaafu aweza kuweka milioni 100 halafu akawa na income ya around 800,000 kila mwezi.
 
Una umri gani? Jack Ma alisema katika maisha yako, anza ujuzi au biashara ukiwa 20, 30 hakikisha una ujuzi wa kitosha wa unachokifanya na umeajiri watu. 40 hakikisha ulichoanzisha kina jitegemea bila wewe kuwepo kila siku. 50 hakikisha ulichoanzisha kina kulea.
Ni kweli kabisa,lkn maneno ya huyo jamaa sio dogma.
 
Elimu ya uwekezaji inahitajika sana. Wengi wetu hatuelewi kabisa mambo ya hisa, hati fungati, mambo ya UTT ndio kabisaaaa.

Natamani mitaala ingeboreshwa haya mambo na ujasiriamali (ijikite kwenye finance) yakapigwa hata kwa utangulizi tu.
Ni sahihi kabisa Mkuu,hiyo Elimu murua kabisa wengi hatuna.
 
Haya mawazo ya mzee ambaye hana nguvu za kufikiri wala kufanya kazi. Achana na millioni 100 kutengeneza 800k.
Kwa kijana mwenye nguvu za mwili na uwezo wa kufikiri vzri ukiwa na tsh mill 10 unaweza kutengeneza 1M net profit!
Bond fund iko structured kumfaa zaidi mtu aliye na kiasi fulani kikubwa, anaweka kwenye mfuko huo - halafu sehemu ya faida inatumika kumlipa kila mwezi au kila kipindi fulani anachochagua. Mfano anayestaafu aweza kuweka milioni 100 halafu akawa na income ya around 800,000 kila mwezi.
 
Haya mawazo ya mzee ambaye hana nguvu za kufikiri wala kufanya kazi. Achana na millioni 100 kutengeneza 800k.
Kwa kijana mwenye nguvu za mwili na uwezo wa kufikiri vzri ukiwa na tsh mill 10 unaweza kutengeneza 1M net profit!
Mkuu, uwe unaeleza pia risk ya kupoteza hiyo pesa yote - kwani si kila mtu mwenye nguvu anaweza kufanya biashara kwa mafanikio.

Pia hata wengi waliofanikiwa sana katika biashara na wana nguvu tosha, huweka sehemu ya fedha zao kwenye mifuko hii wakizingatia risk yake ndogo.
 
Savers are losers

1. Sasa hivi Vitu vimepanda Bei mara 100% toka uzi wako Uweke

2. Hela ulizotunza Zishashuka Thamani yake

3. Bati Na Cement vimepanda Bei

4. Mafuta Yamepanda Bei

Mil 20 ya Kipindi unaweka uzi ni mil 17-18 sasa hivi
 
Kweli iyo kabisa
 
Kweli kaka mambo yamekuwa magumu , Ngoja nimpigie Hangaya anioe hata 10000
 
Usi-save. Mwisho mwa 2022 hio 22 million inaweza ikawa haina thamani. Vifaa vya ujenzi vinapanda bei mara mbili mfano mwanzoni mwa 2021, nondo ya 10mm ilikuwa tshs 15,000. December 2021 ikawa tshs 22,000. Sasa hapo uki-save na hii inflation utaumia. Kila ukipata hela iweke kwa ujenzi.. usisubiri uwe na hela nyingi.
Hii pia inawahusu wale walioacha maboma yao site bila kuyapaua huku wakiendelea kusave ili kunununua bati,nawashauri nunueni bati taratibu mzihifadhi mahal i kwani bei inaongezeka kila mwezi
 
Back
Top Bottom